The Lastdream
JF-Expert Member
- Jan 23, 2024
- 1,971
- 4,572
Salaama?
Leo nilkuwa napitia picha za zamani, nikakutana na picha ambayo ilinifanya nilie kwa furaha, mwanamke shupavu, aliyejaa tabasamu usoni akiwa na beseni lake nyuma akiwa amebeba mtoto aliyefungwa na kanga. Hakika nimekumbuka mbali sana.
Mimi kipindi nakua mzee wangu alikuwa mlevi sana, stori moja ambayo naikumbuka yenye historia kubwa ni siku moja nilipotaka kwenda chooni.
sasa pale tulipokuwa tukiishi pembeni kulikuwa na nyumba ya jiran ilikuwa na mbwa lakini mbwa wale walikuwa hawana matunzo wanarandaranda tu, usiku huo nakumbuka mama anajifuta machozi baada ya kupokea kipondo kutoka kwa mzee hapo mzee kashalewa, akimaliza kumpiga anaamua aondoke, sikumbuki muda sahih ila giza ilkuwa kubwa nikamuambia mama nahitaji kwenda chooni kukojoa.
Akawasha chemli na palikuwa kuna kimvua kimetoka kunyesha, sasa tumetoka nje maana choo kipo nje hatua kadhaa kutoka nyumba, ni vile vyoo vya shimo. Basi kipindi tunatoka wale mbwa wa jirani wakamuona sijui walifikiri nini! Walikuja ghafla wakiwa wanataka kuja kuninga’ta mama akanibeba wale mbwa walikuwa wawili wakamvaa kwenye mguu wakaanza kumnga’ta basi nikaanza kupiga kelele na mama akipiga kelele.
Jirani wa nyumba ya pembeni akawa anaongea dirishani we toka. Tukaanza kuona majirani wanatoka mbwa wakakimbia ila damu alishaanza kuvuja bimkubwa.
Ikabidi usiku ule majran waje kugonga kumbe mzee hayupo, wakambeba mpaka hosptali.
Kwa kweli siku ile huwa haifutiki kabisa kwenye maisha yangu, sasa nimekua mkubwa nilipokuwa mtoto nilikuwa nikiongea nitakusaidia mama nikiwa mkubwa. Hakika nadhiri ile sijaacha, hata kama nikipata elf5 namtumia mama 2500 unaona jinsi anavyoshukuru, wale ambao wanawatumia wazazi wao watakuwa wanaelewa hii hali na jinsi unavyojhisi.
MAMA NI TUNU YENYE THAMANI.
Embu share kisa chako na mama yako tuwaenzi mama zetu?