Mama na mwanae wana mshambulia muoaji

April26

JF-Expert Member
Jul 14, 2020
1,403
2,119
Mshikaji ananisimulia tukiwa kwenye daladala, dahh bro mambo yamenifika hapa..... Nimevumilia lakini nimeshindwa.

Mke wangu ambae ninae unajuwa hatujawahi funga ndoa ila tuna mtoto mmoja na tuna miaka 2 lakini familia yake wananifahamu wengi tu japo sijawahi kufika home kwao kabisa,,ni mzee wake tu ndo sijaonana nae ila mama mkwe nimeishi nae kwangu kama miezi miwili,,,,,,,MIMI......EHNHEE....

Sasa bhana imekuwa ni vulumai huku na huko hasa nikiwa sina hela analeta fujo pasipo sababu ili tu anitukane na kunisema vibaya hadi anafikia kusema ni kama ndiye anaelea mtoto peke ake hadi nashangaa.

Mwanzo tuliwahi kukwazana nikamwachia chumba na sebule akashindwa kulipa nikarudi nikalipia kwingine nikamchukua tukaishi nikajuwa kajifunza,,,,tumekaa upepo wa kipato ulivyoyumba tabia ikaendelea naona alisahau kama nilimkimbia.

MIMI......NDIYOO!!!.....imekuwa ni kawaida yeye kunisema na kunizodoa na mama mkwe wangu, nimekuwa nikimshirikisha baadhi ya matatizo ya mwanae lakini naona kabisa najichoresha tuu.

Hapa nina mwezi na nusu nimemkimbia tena na napokuwa mbali nae amani tele, sikuwa namsaliti mwanzo lakini now nimeanza kupiga mademu wengine aisee!!! Simuonei hata huruma japo kuna muda napatwa na upendo sana juu yake hadi nakwenda nilipomuacha nalala ila sifanyi nae kitu.......pale bro ni kwangu kodi nimelipa mimi so sometimes napamiss tu kwa kuwa kuna vitu vyangu na mwanangu pia,,,,MIMI DUUH.......

Kwa hiyo bro mwezi huu wa pili kodi inaisha na hajui ninapoishi na sina mpango wa kulipa kodi pale, kuna muda hadi najihisi nimeoa mkosi na pia nashukuru hata SIJAFUNGA NAE NDOA sijui ingekuwaje?

Mama mkwe ndie anaempa kiburi mwanae anadai nikienda kwao hilo tatizo litaisha etii........labda hatuna baraka za wazazi. Nikawaza nisije kwenda ndo nikatoka ni ndondocha kabisa,,,,tukachekaa

Lakini ukumbuke mzazi wake (mama mkwe)mwenyewe na dada yake waliwahi kunambia ni tabia zake za mdomo na dharau tangu utotoni huwa yuko hivo eti nimvumilie,,,,yaani bro nikiwa sina hela shida nikizipata nikampa za matumizi sometimes hapiki nikiuliza ananambia wakati sina hela nilikuwa natumia za nani so anachukuwa hela na pesa ya milo mitatu atapika mara moja tu ananambia pesa imeisha. Yeye ana kajibiashara sehemu anaingiza sio kipato kikubwa. Mimi ni mpambanaji kama unavyonijuwa, ila hawa watu wa huko kaskazini daaah.

Sasa bro nimeamua kukaa nae mbali,. SITAKI TENA KUOA JAPO NAMPENDA NITAVUMILIA NITAPONA TU HII DEPRESSION,,,,,UONGO BRO???

Mwisho wa simulizi baada ya kukalibia kituo anachoshuka yeye,nikamwambia kaa na msimamo huo huo utakuja kufa,,,,akasema mambo ni mengi mengine siri yangu bro ila inaniuma sana.

Daah!!

Binafsi sita OA.
 
Mshikaji ananisimulia tukiwa kwenye daladala, dahh bro mambo yamenifika hapa..... Nimevumilia lakini nimeshindwa.

Mke wangu ambae ninae unajuwa hatujawahi funga ndoa ila tuna mtoto mmoja na tuna miaka 2 lakini familia yake
Subiri vijana na kampaini yao wafike hapa
 
Huyo rafiki yako angekua karibu yangu angechezea banzi kali sana! Hana misimamo ya kiume
JamiiForums427229294.jpg
 
Easy in,easy out

Hapo ndo lala ya kuishi na mwanamke bila ndoa kilichobaki ni kulea watoto wako mwanamke piga chini...

Mfano hai wa jinsi ya kuishi na wanawake wa kizazi kipya
 
Easy in,easy out

Hapo ndo lala ya kuishi na mwanamke bila ndoa kilichobaki ni kulea watoto wako mwanamke piga chini...

Mfano hai wa jinsi ya kuishi na wanawake wa kizazi kipya
Hawa wanawake wa kisasa wanataka hivi tuu.

Nowdays hizi matukio zimekuwa nyingi sana eti.
 
Back
Top Bottom