Mama mkwe kamtorosha Mke wangu, nifanye nini niko njia panda

Habarini za usiku wapendwa

Naomba kwa wenye ufahamu na mambo haya wanijuze nifanye nini kwasababu niko njia panda iko hivi mke wangu tulikosana kidogo akaenda kwao amekaa wiki mbili nimeenda kwa lengo la kuona mtoto lakini cha ajabu walipo pata taarifa kwamba naenda tu Mama mkwe amemtorosha mke wangu na wote hawatoi ushirikiano simu hawapokei wala kujibu sms yani ni kama hawataki mawasiliano kabisa na wakati tuna mtoto pamoja

Naomba msaada kwa mwenye uzoefu na mambo haya

Tuliza wenge, chukua mke mwingine mbichi siyo single mother lakini.

Huyo aliyetoroshwa atajikuta amerudi kuwa na mke mwenzake alafu ajihudumie mwenyewe.

Koma kumtafuta tena, hata kama unaumiya, usimpigie Simu wala kutuma sms tena. Wewe ndo unampa turufu dhidi yako kwa kufanya hivyo. Hapo unaandaliwa mazingira ya kufanywa zezeta. Wanawake ni watu wajanja sana, kuwa makini.
 
Nashukuru kwa kunifumbua macho mkuu hii inaweza ikawa kweli kwasababu itaonekana mimi ndio mwenye uhitaji kuliko yeye
 
Hao Mimi ningewapa somo Moja la kukaa kimya wasingeamini kabisa.Hata apige nani wa kwao sipokei mtu akibadili namba napokea namsalimia kistaarabu namwambia hebu kata nikupigie hapo anakula block,Hadi dawa iwaingie utaona wanafunga safari wao bila kuitwa.Halafu wakija usiruhusu kikao kabisa waambie yameisha mwambie mkeo aingie ndani apike ama akufulie nguo.Sasa na wewe jaribu kuwa mwanaume usithubutu kufungua mdomo kuuliza Kwa nini aliondoka na kukufanyia hivo.Kumbuka Hawa wa kwetu ni wanawake wa kiswahili.
 
Habarini za usiku wapendwa

Naomba kwa wenye ufahamu na mambo haya wanijuze nifanye nini kwasababu niko njia panda iko hivi mke wangu tulikosana kidogo akaenda kwao amekaa wiki mbili nimeenda kwa lengo la kuona mtoto lakini cha ajabu walipo pata taarifa kwamba naenda tu Mama mkwe amemtorosha mke wangu na wote hawatoi ushirikiano simu hawapokei wala kujibu sms yani ni kama hawataki mawasiliano kabisa na wakati tuna mtoto pamoja

Naomba msaada kwa mwenye uzoefu na mambo haya
Wewe huna dhambi yoyote, mtoto mtafahamiana mbele kwa mbele, fanya mambo mengine kaka, maisha ni zaidi ya haya uliyoandika.

Umewekwa kwenye kamati na haujui kamati ina lengo gani, wewe cha kufanya endelea kuishi kama hakijatokea kitu, mtoto siku zote atamtafuta baba yake, hata afichwe vipi ukweli utajulikana.
 
Kijana tulia tuliii acha kupiga simu wala kutafuta. Hapo wanakuchezea kwa kuwa wamekuona huna msimamo na unawahitaji so wanakuchezea.

Piga buyu halafu kama ukiweza uwe unaingiza hata demu nyumbani unapoishi taarifa watazipata na kurudi kwa speed ya V8. Mlete hata ndugu yako wa kike ambaye mtaani hajulikani wambea watampa taarifa kuwa una mwanamke mwingine watarudi kasi sana

Hii mbinu nimekupa ya kibaharia mno tulitumia sana sisi wakongwe wa zamani
 
Nashukuru sana kwa kua na mm kwenye wakati huu mgumu hakika inabidi tu nifanye maisha mengine
Wewe huna dhambi yoyote, mtoto mtafahamiana mbele kwa mbele, fanya mambo mengine kaka, maisha ni zaidi ya haya uliyoandika.

Umewekwa kwenye kamati na haujui kamati ina lengo gani, wewe cha kufanya endelea kuishi kama hakijatokea kitu, mtoto siku zote atamtafuta baba yake, hata afichwe vipi ukweli utajulikana.
 
Kausha mradi unajua yuko kwao endelea na mambo mengine,wakimchoka/akichoka atarudi mwenyewe.

Sent from my TECNO BE6 using JamiiForums mobile app
Mimi kama mama mkwe yuko na mwanae na mjuku hapo wala hata siangaiki kujisumbua maana yuko salama nyumbani, mtoto akikua atamtafuta baba.

Lakini mzee kwanini akimbiwe? Mbona hajatupa sababu za kukimbiwa
 
Hao Mimi ningewapa somo Moja la kukaa kimya wasingeamini kabisa.Hata apige nani wa kwao sipokei mtu akibadili namba napokea namsalimia kistaarabu namwambia hebu kata nikupigie hapo anakula block,Hadi dawa iwaingie utaona wanafunga safari wao bila kuitwa.Halafu wakija usiruhusu kikao kabisa waambie yameisha mwambie mkeo aingie ndani apike ama akufulie nguo.Sasa na wewe jaribu kuwa mwanaume usithubutu kufungua mdomo kuuliza Kwa nini aliondoka na kukufanyia hivo.Kumbuka Hawa wa kwetu ni wanawake wa kiswahili.
Chukua hii mkuu bonge la idea. Au kama vipi potezea jumla matapeli hao, alikuja kwenye ndoa kukutapeli tu kaona hutapeliki kaamua kusepa. Piga kimya
 
Habarini za usiku wapendwa

Naomba kwa wenye ufahamu na mambo haya wanijuze nifanye nini kwasababu niko njia panda iko hivi mke wangu tulikosana kidogo akaenda kwao amekaa wiki mbili nimeenda kwa lengo la kuona mtoto lakini cha ajabu walipo pata taarifa kwamba naenda tu Mama mkwe amemtorosha mke wangu na wote hawatoi ushirikiano simu hawapokei wala kujibu sms yani ni kama hawataki mawasiliano kabisa na wakati tuna mtoto pamoja

Naomba msaada kwa mwenye uzoefu na mambo haya
Kama Mama kama mtoto....hawana akili wote endelea na maisha yako na utafute kipoozeo kingine.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom