Makongoro Mahanga ashinda kesi ya uchaguzi jimbo la Segerea

Status
Not open for further replies.
Leo inangojewa kwa hamu kwa CCM na CDM kwani mpaka sasa ktk kesi za kupinga ubunge CCM ineshinda mechi za Arusha (Lema) pekee na wamepigwa chini Sumbawanga, Bihalamuro na Singida na leo inaelekea CDM kuendeleza ushindi. Wakati huohuo Ubungo na Igunga zangojewa. Ifahamike wizara ya sheria imezitaka mahakama kumaliza kesi zote tarehe 4/5/2012

Naelekea mahakamani kwa Updates zote. Kwa lugha ya Kiingereza au Kiswahili haijalishi
Watu wengi tuna-overlook hukumu ya Kigoma Mjini iliyofunguliwa Ally Mleh (CDM) akipinga ushindi wa mgombea wa CCM, Peter Serukamba nakumbuka ilitupiliwa mbali, na kesi ya Mkosamali wa NCCR jimbo la Muhambwe.
 
Kwahiyo mkuu wangu na hukumu ya Lema uliwekewa humu na ukaisoma kabla haijasomwa Mahakamani?

Hakuna aliyedai kuwa nayo.... tungemtaka aiweke humu ili tumuamini... swala la kujua hukumu itakuwaje particularly kwa aliyefuatilia Maendeleo ya kesi ni logic zaidi kama una ufahamu wa sheria (not neccessarily a lawyer) inakuwa rahisi zaidi kutabiri hukumu na ukawa correct.... Naamini hakuna anayeweza kuwa na hukumu hata kama ingeandaliwa state house kama ya Lema inavyodaiwa bado sio rahisi kuwa mikononi mwa mtu mwingine.... otherwise uniambie wewe ndio profesa Juma Jaji, wa kesi hii maana hivi avatar nazo zina mambo yake....otherwiae nadhani haya tuyaache turudi kwenye mada mliopo mahakamani updates ni muhimu.
 
Moja ya sababu za JK kuchelewa kufanya kile anachokiita mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri ni pamoja na hukumu ya leo.

JK hataki kuonekana mbaya nia yake ni wengine wajipunguze wenyewe kumuondolea lawama, ukumbuke Makongoro Mahanga alikuwa ni mwanachama mwaminifu na muhimu kwenye kundi la wanamtandao na mtiifu kwa Lowasa.

Hukumu iko very clear Makongoro is out pasi na shaka yoyote.

Ndio maana hapo mwanzo ulisema hukumu tayari ulikuwa nayo tangu juzi? Tuwekee basi humu hiyo hukumu tuisome.
 
Ulinzi mkubwa hivi huwa unaashiria nini? Wasiwasi wa nini tena?

mmeona madhara ya kuunganisha thread, ona sasa tunategemea update kutoka kwa wachangiaji badala ya muwasilisha hoja. wekeni utaratibu iwe option kwa the same news kuwa accesed from different reporter kama anakuwepo. UHURU WA KUHABARISHANA.
 
Huenda ushahidi ukaonekana wazi machoni pa watu lakini jaji asione hilo by the way mahaka zetu hazitabiriki ndugu zangu ni kama kurusha coin.
 
naona hata update hakuna ila ni kelele tu.....nimemkumbuka ISANGO gafla.....ila jiandaeni sana hasa wewe Matola
 
Last edited by a moderator:
Wakuu mimi nimeamka na uchovu wa jana wa kusherehekea kutokupanda kwa mishahara! Hapa Arusha tunasubiri kwa hama sana Updates kutoka huko mahakamani.

Na Updates zilizopo hapa Arusha ni kua ile kesi ya kumvua ubunge muheshimiwa Lema wao wenyewe CCM baada ya kutafakari kwa kina ili isiikubali ile rufaa ya Chadema hapo awali eti ni kua wamekaa na kutafakari na wakaiomba mahakama ikubali rufaa ile na katika kusikiliaza rufaa hiyo basi mahakama ikubali na kuurudisha ubunge wa Lema kuepusha garama za uchaguzi huku wakijua kua hawatashinda hata kama Chadema wakasimamisha jiwe! Kwa hiyo Update nilizonazo ni kua Lema lazima ubunge wake arudishiwe.
 
Usiongee kitu usichokijuwa, Katibu wa CCM mkoa wa Dar es salaam alishakuja jimboni kwetu Segera kuwaambia CCM wenzake wajiandae kwa uchaguzi mpya. hukumu iko wazi Makongoro is out, kila mwana CCM wa kweli ambaye yuko deeply analifahamu hili fika.

Wanalijua ila mpaka waambiwe kwa mahakama
 
nikumbushe kidogo mkuu kuhusu kesi ya Ilemela kama hautajali!
...hiyo kesi ilifunguliwa na vilaza wa magamba kupinga ushindi wa mbunge wa Chadema mh Hines Kiwia mbunge wa jimbo la Ilemela Mwanza,wakili wa mh Kiwi(mb) alikuwa jembe mh Tundu Lisu(mbunge)...
 
Wakuu tulio Arusha tunawategemea mlio kunakosomwa hukumu ya Kesi ya kupinga uchaguzi jimbo la Segerea tafadhali wandugu na madada wa huko msituangushe.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom