Makongoro Mahanga ashinda kesi ya uchaguzi jimbo la Segerea

Status
Not open for further replies.

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
Leo inangojewa kwa hamu kwa CCM na CDM kwani mpaka sasa ktk kesi za kupinga ubunge CCM ineshinda mechi za Arusha (Lema) pekee na wamepigwa chini Sumbawanga, Bihalamuro na Singida na leo inaelekea CDM kuendeleza ushindi. Wakati huohuo Ubungo na Igunga zangojewa. Ifahamike wizara ya sheria imezitaka mahakama kumaliza kesi zote tarehe 4/5/2012

Naelekea mahakamani kwa Updates zote. Kwa lugha ya Kiingereza au Kiswahili haijalishi

FINALLY: Makongoro Mahanga kashinda kesi!

Wanabodi,

Hukumu hii inatarajiwa kuanza kusomwa muda wa saa 4 kamili asubuhi ya leo.Pamoja na madai mbalimbali yaliyowasilishwa na mdai akiwakilishwa na wakili Peter P. Kibatala wa Trustmark Attoneys, hapa chini nibaadhi ya hoja za upande wa mlalamikaji:

1. Msimamizi Wa Uchaguzi alitangaza matokeo pasipo kujumuisha vituo 120 vya Kiwalani, 129 Vingunguti, 4 buguruni, 2, Tabata na 4 Kipawa

2. Vituo tajwa hapo juu, havikufanya mahesabu na majumuisho ya uhesabu wa kura (Fomu 21B)

3. Fomu ya kurekodi matokeo (21B) hazikusambazwa katika baadhi ya vituo na hivyo kuwafanya wahusika kuweka matokeo kwa kutumia karatasi za kawaida(plain papers) ambazo ni rahisi kufanyiwa forgery na ubaya wowote.

4. Afisa Mtendaji Kata ya Tabata - Imelda Kafanabo – alikamatwa na fomu batili zenye matokeo yasiyo halali (ushahidi wa video uliambatanishwa)

5. Mwananchi mwingine alikamatwa Anatoglu akiwa na fomu na mihuri isivyo halali ikiwa imempa(video iliambatanishwa ikimwonyesha mtuhumiwa akikamatwa)


6. Maboksi ya kuhesabia kura kutoka Kata ya Buguruni yenye namba 15134, 151305, 151083, 15144, 15109, 15129, 151302 yalikuwatwa yakiwa wazi, hayana lakiri.

7.
Mdai akiwa na wagombea wenzake wa Civic United Front (CUF) na Sauti ya Umma (SAU) walitoa malalamiko ya mdomo kuhusu kukosekana kwa kura kutoka kata za Vingunguti, Buguruni na Kiwalani. Pamoja na mapungufu hayo, Msimamizi wa Uchaguzi alitangaza matokeo kwa kusema kwamba "ameamriwa kutangaza matokeo mpaka kufikia saa 8 mchana siku ya tarehe 03/11/2010" na aliwakataliwa wadai fursa ya kuweka madai yao kwa maandishi.

8. Mahesabu ya kura kutoka katika vituo yalionyesha Mpendazoe kupata kura 56,962 na Mahanga 44,904.

Mdai ameomba yafuatayo:

(1) Matokeo yaliyotangazwa na kumpa Ushindi Milton Makongoro Mahanga yatambulikane kuwa ni batili(null and void)
(2) Mahakama itangaze uchaguzi wazi, huru na wa haki kwa jimbo la Segerea ufanyike
(3) Au vinginevyo, bila kuathiri mambo yoyote, Mahakama imtangaze Fred Mpendazoe kama mbunge halali wa jimbo la Segerea
(4) Haki yeyote ambayo mahakama itaona inafaa kumpa Mdai
(5) Gharama za Kesi


UPDATES:
Chadema nao wamepiga kambi hapa mahakamani na magwanda yao kama kawa...
Mahakamani ulinzi umeimarishwa sana. Nipo eneo la tukio nje na kwa kweli hakuna speaker kusikia kinachoendelea. Ila raia wamejitokeza kwa wingi na skafu za cdm zipo..
1. Bado kesi haijaanza
2. Hakuna speakers zilizowekwa nje kitu kinachopelekea kujua kinachoendelea ndani, walio ndani simu zimezimwa!
Jaji Profesa Ibrahim Juma ameshaanza kusoma hukumu kama ilivyotarajiwa na watu wengi wamezuiwa nje ya ukumbi wa mahakama
 
Leo inangojewa kwa hamu kwa CCM na CDM kwani mpaka sasa ktk kesi za kupinga ubunge CCM ineshinda mechi za Arusha (Lema) pekee na wamepigwa chini Sumbawanga, Bihalamuro na Singida na leo inaelekea CDM kuendeleza ushindi. Wakati huohuo Ubungo na Igunga zangojewa. Ifahamike wizara ya sheria imezitaka mahakama kumaliza kesi zote tarehe 4/5/2012

Naelekea mahakamani kwa Updates zote. Kwa lugha ya Kiingeleza au Kiswahili haijalishi

Kwani na Igunga cdm ilifungua kesi?
 
Mkuu rufaa ya Lema itaanza kusikiliWa lini?

Kwenye mahakama ya rufaa hakuna cha kusikilizwa mahakama ya rufaa inapitia rufaa iliyowasilishwa! halafu wanaangalia vifungu vinavolalamikiwa na wanapitia hukumu ya mahakama kuu na ushahidi wa pande zote mbili then wana rule out hakuna cha mtu kuitwa mahakamani au kupeleka ushahidi zaidi,. huwa ni kazi ngumu kidogo maana kumbuka hii ni mahakama ya juu kabisa hivo lazima ijiridhishe kuwa sheria imefuatwa na inakuwa na majaji wawili au watatu hivo inakuwa huru zaidi! tusubiri tu watatatoa hukumu!!
 
Baada ya muda nitatoka (sign out) kwenda kumpeleka mtoto wangu shule nikifika kazini nitakuwa hewani kufuatilia kinachoendelea mahakamani...... Huku Tabora jamaa zangu wa CHADEMA wanasubiria kwa hamu kuhusu hukumu hiyo....
 
Mnachonikera ni pale tu mnapoanzisha thread mkitoa matumaini ya updates alafu mnaishia uvunguni!!!

LEO MWENYEWE NAPIGA MTU BANI KWA UZEMBE......OLE WENU!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom