Makongoro Mahanga ashinda kesi ya uchaguzi jimbo la Segerea

Status
Not open for further replies.
3squere jitahidi kutuhabarisha kama ulivyoahidi na leo sitoki kwenye hii sredy mpaka kieleweke.
 
Ndo tunatokea maeneo ya segerea tunaelekea mahakamani kusiliza hukumu ya kesi ya kupinga ubunge wa makongoro kama kawahida simu yangu hiko full chagi full vocha kwa maupdate ya kufa mtu karibuni
---------UPDATE---------
Watu ni wengi sana waoelekea mahakamani
Still tune

Ushauri,
unapo update first page uandike time.
e.g -------update 08:39---------
 
Haya ndio alikuwa anayasema Matola jana,
hii nadhani ni thread ya 6!

Sasa ichaguliwe moja basi ili tupate update. Naomba hiyo itakayochaguliwa iwe sticky hadi hapo hukumu itakapotolewa.

Hivi hukumu inasomewa wapi nataka nami niwe shahidi.
 
Aliyepo mahakamani ajitambulishe ili tujue tunapata habari za uhakika kutoka kwa nani
 
Wanabodi,
Hukumu hii inatarajiwa kuanza kusomwa muda wa saa 4 kamili asubuhi ya leo.Pamoja na madai mbalimbali yaliyowasilishwa na mdai akiwakilishwa na wakili Peter P. Kibatala wa Trustmark Attoneys, hapa chini nibaadhi ya hoja za upande wa mlalamikaji:

1. Msimamizi Wa Uchaguzi alitangaza matokeo pasipo kujumuisha vituo 120 vya Kiwalani, 129 Vingunguti, 4 buguruni, 2, Tabata na 4 Kipawa2. Vituo tajwa hapo juu, havikufanya mahesabu na majumuisho ya uhesabu wa kura (Fomu 21B)3. Fomu ya kurekodi matokeo (21B) hazikusambazwa katika baadhi ya vituo na hivyo kuwafanya wahusika kuweka matokeo kwa kutumia karatasi za kawaida(plain papers) ambazo ni rahisi kufanyiwa forgery na ubaya wowote. 4. Afisa Mtendaji Kata ya Tabata - Imelda Kafanabo – alikamatwa na fomu batili zenye matokeo yasiyo halali (ushahidi wa video uliambatanishwa) 5. Mwananchi mwingine alikamatwa Anatoglu akiwa na fomu na mihuri isivyo halali ikiwa imempa(video iliambatanishwa ikimwonyesha mtuhumiwa akikamatwa)
6. Maboksi ya kuhesabia kura kutoka Kata ya Buguruni yenye namba 15134, 151305, 151083, 15144, 15109, 15129, 151302 yalikuwatwa yakiwa wazi, hayana lakiri. 7. Mdai akiwa na wagombea wenzake wa Civic United Front (CUF) na Sauti ya Umma (SAU) walitoa malalamiko ya mdomo kuhusu kukosekana kwa kura kutoka kata za Vingunguti, Buguruni na Kiwalani.Pamoja na mapungufu hayo, Msimamizi wa Uchaguzi alitangaza matokeo kwa kusema kwamba "ameamriwa kutangaza matokeo mpaka kufikia saa 8 mchana siku ya tarehe 03/11/2010" na aliwakataliwa wadai fursa ya kuweka madai yao kwa maandishi. 8. Mahesabu ya kura kutoka katika vituo yalionyesha Mpendazoe kupata kura 56,962 na Mahanga 44,904.

Kwa hoja hizi na ushahidi huo nadhani kama jaji amekwenda shule na anajua kazi yake barabara,hapa tunaanza kupiga jalamba la kuingia uwanjani kushangilia.Labda tusubiri had dakika ya 90 kujua mpira umeisha na matokeo yapo mkononi.
 
Haya ndio alikuwa anayasema Matola jana,
hii nadhani ni thread ya 6!

Yaani acha tu ndugu, mtu yuko barabarani anaanzisha thread, sijui leo kutakuwa na thread ngapi? Ushauri wangu tuchangie kwenye thread iliyokwisha anzishwa kupunguza usumbufu humu jukwaani.
 
Leo inangojewa kwa hamu kwa CCM na CDM kwani mpaka sasa ktk kesi za kupinga ubunge CCM ineshinda mechi za Arusha (Lema) pekee na wamepigwa chini Sumbawanga, Bihalamuro na Singida na leo inaelekea CDM kuendeleza ushindi. Wakati huohuo Ubungo na Igunga zangojewa. Ifahamike wizara ya sheria imezitaka mahakama kumaliza kesi zote tarehe 4/5/2012

Naelekea mahakamani kwa Updates zote. Kwa lugha ya Kiingeleza au Kiswahili haijalishi
...niweke kumbukumbu sawa,kesi ya kwanza CDM kushinda ni ya ILEMELA Mwanza...kwahiyo ubao wa matokeo sasa usomeke CDM 4 - 1 CCM...
 
Sasa ichaguliwe moja basi ili tupate update. Naomba hiyo itakayochaguliwa iwe sticky hadi hapo hukumu itakapotolewa.

Hivi hukumu inasomewa wapi nataka nami niwe shahidi.

Naona mods wameziunganisha,
hukumu ni pale Mahakama Kuu nadhani ni Sokoine Drive pale!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom