Makinda na Bunge la kelele za taarifa, mwongozo.

Yaani limedharauliwa, watu wanapiga makelele ile mbaya.
Sababu ni nini, je ni jinsia ya kiongozi ndio chanzo au kuongoza bunge kumemshinda?

Chanzo ni hicho nilicho-bold kwa red colour...na nimewai kupost CV yake hapa JF itafute hiyo thread utaipata CV yake and then utajua kwanini kuongoza kumemshinda....
 
Makinda tofauti na mtangulizi na bosi wake wa zamani SS anasumbuliwa na mambo mawili: kulipa fadhila ya waliompa uspika kwa siyo tu kuzima hoja za wapinzani ambao wamekuwa mwiba mkali kwa serikali, lakini pia kuwashughulikia wafuasi wa sita (ikumbukwe kwamba sita alionekana ni chanzo cha mijadala mikali iliyopelekea kuibuliwa mambo mengi ya ufisadi na hataLowasa na wenzake kujiuzulu kwani yeye aliruhuru mijadala badala ya kuizima kama anavyofanya huyu mama). Pili itakumbukwa kwamba huyu mama hata nia yake ya kuwania uspika alimficha hata bosi wake Sita kwa hiyo alikuwa anamzunguka, hivyo anataka kuonyesha kwamba anaweza, hasa ikizingatiwa kwamba kigezo kikubwa kilichotumika kumuondoa Sita kwenye Kinyang'anyiro ni jenda (kuwa na spika wa kwanza mwanamke). Hata hivyo hililimemsumbua sana kwani Makinda kwam hulka ni mtu mwenye jazba na pia kama alivyowahi kutamka sita kipindi cha uspika wake 'hana ngozi ngumu' na akikwaruzwa kidogo damu inatoka (hawezi kuhimili mikiki mikiki ya wabunge machachari na wenye hoja zilizosheneni takwimu na zilizofanyiwa kazi!!). Hivyo uaona kwamba ukichanganya mambo haya yote na ukweli kwamba bune hili pia limeingiza vijana ambao ni wasomi lakini pia ambao wamechoshwa na porojo za miaka nenda rudi bungeni (mfano:....kutokana na uwezo mdogo wa serikali... [huku wengine wanatanua]...mpango kabambe wa serikali...litaingizwa kwenye bajeti ijayo n.k.; unapata jibu moja tu: wabunge wengi (hata wa CCM) wameshaanza kumchoka na kumdharau kwa kuliongoza bunge vibaya. Mtakumbuka alivyoanza kwa spidi kudadilisha baadhi ya kanuni nzuri tu za bunge ambazo ziliundwa kipindi cha Sita e.g. sakata la kiongozi rasmi wa kambi ya upinzani bungeni. Pia ameshindwa kudhibiti kile kinachoitwa...'muongozo wa spika'...kiasi kwamba bunge limekosa mvuto kabisa kutokana na mbunge anayetoa hoja kuwa interrupted hata pale anapozungumza hoja ya msingi; also ameendekeza sana kitu kingine kinachoitwa...'thibitisha kauli yako/futa kauli'...halafu wakati huohuo mbunge akileta ushahidi na akigundua kwamba serikali itaumbuka anaukalia!!! e.g sakata la Lema VS Pinda. Kwa hiyo wabunge sasa kwanza wanajua kwamba hayuko stable na anatabia ya kuzima kila hpoja ya maana ili awabebe waliomuweka pale so wengine waaamua kumfanya awe frustrated (wanawasha vipaza sauti wakati mwingine anaongea; wanazomea - angalia leo wakati Pinda akiliomba bunge wakarekebishe bajeti ya madidi na nishati-). Pia kuna mawaziri na wabunge wa ccm ambao wanachangia pia hali hii kwa kuleta maneno ya kejeli na dharau halafu spika hachukui hatua yoyote: Warizi Lukuvi aliwahi kumwita mbunge wa Iringa mjini (CMD) 'mchungaji uchwara' lakini mwenyekiti wa kikao siku hiyo Jenista Mhagama badala ya kumkemea waziri akamwacha tu. Mwisho kama mwenendo huu hautabadilika sitashangaa ikitokea huyu mama kushindwa kabisa kuliongoza bunge hili; na hata Sita anajua sana weakness zake (kumbuka wakati wa sakata la ripoti ya Mwakyembe Sita alikuwa anasafiri na alimkabidhi vyote lakini alimwambia ripoti hiyo ya Richmond imsubiri mpaka arudi!!).
 
Kwa ujumla kazi ya mbunge ni kuwakilisha hoja za wananchi bungeni kwa maana ya kupatiwa ufumbuzi na si kutetea hoja za serikali....

Ni vyema wabunge wajue ni wajibu wao na tija kuainisha mapungufu yanayojitokeza ktk utekelezaji wa mipango ya serkali na kutoa mapendekezo kwa lengo la kuboresha na si kutoa sifa tu na kuzungumzia yale ambayo serikali imekwishafanya. Ni kutokana na tabia hii hususani kwa wabunge wa chama tawala kumeipelekea serikali kwa mwaka hata mwaka kutofanya maboresho ktk hoja za msingi na kusababisha hoja hizo kujirudia mwaka hata bila kupatiwa ufumbuzi mfano mishahara hewa, upatikanaji wa nishati ya uhakika, kuchelewa mishahara/mafao ya walimu, utoaji wa mikopo ya elimu ya juu, usimamizi wa maliasili za nchi mfano madini, wanyama pori nk.

Iwapo wabunge wataendelea kujadili hoja kisiasa ziadi kwa maana ya wabunge kuwajibika kwa vyama vyao na si kuwajibika kwa wananchii na kufumbia macho mapungufu yanayoonekana wazi basi ni wazi kuwa maswala ya aibu kama ya kukosa umeme wa uhakika na mengine mengi kama wananchi maeneo ya migodini kuuwawa au mazingira yao kuchafuliwa yataendelea kujitokeza na kutupeleka pabaya zaidi.

Lengo langu hapa ni kumuasa Spika Makinda kuhakikisha kuwa wabunge wanajikita katika hoja kwa lengo la kuboresha....si sahihi kuwaacha wabunge wachangie anyhow...ni kutokana na hilo unakuta mbunge anapewa nafasi kuchangia wakati hana hoja toka kwa wananchi na anaishia kutoa kauli za kulaani migomo labda ya wanafunzi, kusifia viongozi wa serkali au vyama vyao, au kujadili mtu....hii si sahihi kwa muda wanaopata wabunge.

Ni kutokana na usimamizi wa Spika mwisho wa siku hoja za mawaziri zitajadiliwa kwa maana ya kuboresha na si kusifiwa tu....sidhani kama Mawaziri wanapotoa hoja wanazileta kwa maana ya kusifiwa jinsi zilivyo andikwa au kuwasilishwa.

Kutokana hapo juu nakushauri Spika kutoentertain yafuatayo:

Wabunge kutoa salamu kila wanaposimama
Wabunge kusifia uwasilishwaji hoja
Wabunge kupongeza watoa hoja (Mawaziri) kwa kutoa hoja
Wabunge kutojikita katka hoja husika
Swala la kuunga mkono hoja 100 kwa 100 wakati mbunge bado anatoa mapungufu ktk hoja husika - mbunge ajuea anaunga mkono nini?
Mawaziri kutoa majibu yasiyo na mashiko wakati kila mtu anaona wazi kuwa Waziri ameshindwa kijibu hoja husika (mfano Waziri Pereira)
Kutowalinda wasemaji kutoka chama tawala pale wanapotoka
Kuto-entertain mwongozo wa spika kwa maana ya kuua hoja mbalimbali kunakofanywa na mawaziri ambao kimsingi wana uwezo mdogo sana
............
...........

Nimalizie kwa kusema kuwa ni kutokana na Bunge kushindwa kufanya kazi yake vizuri ya kuisimamia serikali kunasababisha serikali kutokuwa makini ktk utekelezaji wa majukumu yake na mwisho ni seme kuwa mapungufu yote yanayojitokeza serikalini ktk utekelezaji wa shughuli zake Bunge la Tanzania nalo pia linahusika moja kwa moja. Hivyo ni wazi kabisa kuwa mwisho wa siku utendaji wa Spika ktk kuliongoza bunge kunachangia kujenga au kubomoa maendeleo ya nchi moja kwa moja.
 
habari za siku nyingi ndugu zangu? leo hii kagame kaulizwa swali na wanafunzi wanyarwanda wanaoishi ulaya na marekani, kuhusu msimamo wake kwa yale yanayojiri libya, kiukweli amijigongagonga sana na matokeo yake akasema kua ni bora ufunge mlango wa nyumba yako mapema kab;a mwizi hajingia, na kama akiingia uwe tayari kukabiliana nae,
je ****** yeye msimamo wake ni upi? asanteni sana nawasilisha
 
heading yako na ulichokiandika haviwiani. rekebisha kisha wasilisha tena
 
jamani labda vidole vyake vinatumia umeme... si unajua tena labda walishakata na vidole vika korrupt. msameheni
 
habari za siku nyingi ndugu zangu? leo hii kagame kaulizwa swali na wanafunzi wanyarwanda wanaoishi ulaya na marekani, kuhusu msimamo wake kwa yale yanayojiri libya, kiukweli amijigongagonga sana na matokeo yake akasema kua ni bora ufunge mlango wa nyumba yako mapema kab;a mwizi hajingia, na kama akiingia uwe tayari kukabiliana nae,
je ****** yeye msimamo wake ni upi? asanteni sana nawasilisha

cjui tufanyaje? ingewezekana mods wangekuwa wanapitia kwanza threads kuona subsitance contained there in, haina mashiko ni kutoiweka kabisa. huku ni kujaza nafasi tu humu
 
Back
Top Bottom