ADVOCATE NEWBOL
Member
- May 21, 2011
- 33
- 11
Spika Makinda anasema kwamba, "Baada ya hotuba ya bajeti kusomwa Bungeni, Bunge haliwezi kuibadilisha kitu." Spika kwa lugha nyingine anasema, Bunge halina kazi ya kufanya, na kwa nini walipwa kukaa Dodoma kikao cha bajeti wakati hawana cha kufanya? Siamini, na ndiyo maana nimeshtuka sana na kauli hiyo ya Spika. Spika huyu tena kwa mara nyingine amejidhirisha waziwazi yeye mwenyewe, tena kwa hiari yake binafsi pasipo kulazimishwa wala kushawishiwa na mtu yeyote, kwamba hajui kitui: si kitu huyu. Kanyaboya, ni spika mjima katika karne ya 21 kwa sababu hajui kazi ya Bunge. Nampa dosi murua ya Sheria, ngoja nimuelimishe.
Kwanza tujiulize je, hotuba ya bajeti nini? Hotuba ya bajeti ni maombi ya serikali (executive) kutoka kwa Bunge (parliament) kwamba serikali inaomba fedha kwa ajili ya matumizi iliyoyaainisha na, katika kufanikisha hilo, serikali hiyo2 inaomba pia Bunge liiruhusu itoze kodi na kukopa ili kupata fedha hizo (tazama Ibara za 137 na 138 za Katiba ya sasa ya Tanzania 1977).
Katika bajeti, Bunge nalo sasa lina mamlaka ya kikatiba ya (a) kurekebisha maombi hayo fedha ya serikali kwa kuyapunguza au kuongeza nk, na (b) kukataa kabisa maombi yote hayo ya serikali na kuiagiza ilete maombi mapya (tazama Ibara za 90 na 139 za Katiba).
Kwa kweli hii ni hatari kabisa, kama Spika kiongozi wa mhimili huu muhimu wa Bunge hajui mamlaka ambayo Bunge linayo dhidi ya serikali. Hatari. SIYO KWELI KWAMBA HOTUBA YA BAJETI IKISHAKUSOMWA BUNGENI, BASI, BUNGE HALINA LA KUFANYA: MAMA MAKIND, MBALI NA KUKARIRI KANUNI ZA BUNGE AMBAZO ZINATOKANA NA IBARA YA 89 YA KATIBA, SOMA KATIBA ITAKUSAIDIA KTK KAZI ZAKO...