Makamu wa Rais ana kazi gani?

Ili kuelewa mkorogo huu wa Makamu wa Rais itakupasa urudi miaka ile siasa za vyama vingi ziliporudishwa katika siasa za Tanzania na Muungano.
Mwanzoni, Rais wa Zanzibar alikuwa automatic anakalia kiti hicho ya Makamu wa Rais na alikuwa anawakilisha maslahi ya Zanzibar katika Muungano.

Tulipofuta utaratibu huo wa Zanzibar kuwa Makamo wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano ndio tumejikuta na Makamu wa Rais ambaye kama ulivyosema katika kutahadharisha "yupo yupo tu ili kuaccomodate Muungano" lakini hawakilishi Zanzibar au maslahi ya Zanzibar katika Muungano.

Jambo baya ambalo linachochea Zanzibar kulalama na kuutupia madongo Muungano ni ile kumfanya Rais wa Zanzibar kuwa ni (Mjumbe )Waziri asiye na wizara maalum katika Baraza la mawaziri wa muungano.

Ukiangalia kwa undani ,tunaweza kusema kuwa Muungano tuliuvunja siku ile tuliyomfanya mwakilishi mkuu wa upande Zanzibar kuwa hana sauti yoyote katika Muungano.

Neno ulilolitumia "ku-accomodate Muungano" lisomeke funika kombe, au kutia changa la macho ili Muungano uzidi kuonekana kuwa ni kichekesho tu. Ni kweli kama ilivyo leo, Nafasi ya Makamu wa Rais ni ukiritimba tu, cheo ambacho kinafuja fedha za walipa kodi.

Inapotokea watu kuanza kuona Serikali ya Muungano haipaswi kuwa na sura ya Kimuungano basi ujue watu wameanza kufuta tongo, watu wameanza kutoka usingizini na kuona mazingaombwe na ombwe la Muungano usio Muungano.

Hiki cheo kuna haja kufutwa ili iwezeshe kuundwa kwa serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar tayari ipo na kuunda serikali ndogo ya Muungano ambayo, Rais wa Tangayika na Rais wa Zanzibar watatawala kama co-presidency ya Muungano na baraza dogo la wizara za muungano.
Hakuna urafiki wa watu wa tatu na ukanawiri, kwa kiasi kikubwa marafiki mkiwa watatu, ni lazima mumsengenye mmoja wenu. Kwahiyo serekali tatu ni mgogoro zaidi, cha kufanya wenzetu wa Zanzibar waache roho mbaya, au ubinafsi. Tuwe tuna serekali moja tu.
 
Muzee ya Mikasi!!!!

scicors.jpg
Mkasiiii
 
Kabla ya kuanza kwa mfumo wa vyama vingi, makamo wa rais alikuwa Rais wa Zanzibar, lakini kwa kuhofia chama kingine kishika madaraka Zanzibar, rais wa Zanzibar ni nobody kwenye set up ya muungano, hivyo sasa Makamo wa rais yupo yupo tuu standby just in case anything happens kwa rais!. Ofisi yake inashughulikia mambo ya mazingira na muungano. Kwa sasa kazi kubwa ya makamo, ni kumwakilisha rais.

P
Hiki cheo kingefutwa tu, hakina kazi. Kuna kipindi kama sio 2013 au 2014 JK alikuwa nje halafu kuna kiongozi aliharibu huku. Ikabidi makamo amsubiri JK hadi arudi ndio amfukuze.
Kumbe makamo licha ya ukubwa wa jina lake, hana hata ubavu wa kutengua uteuzi uliofanywa na rais.
 
Back
Top Bottom