Elections 2010 Makamba atinga jimboni Bumbuli leo na ufanya vikao vya siri.....

How outhentic is this information? Mbona the whole of last week, huyo Mama alikuwa Johanesburg...imewezekanaje akawepo Jbg na Bumbulu at the same time? Sina uhakika na hiyo mikutano mingine unayoongelea, lakini kwa huo wa Mama ni UONGO..nathibitisha hilo... Again, inanifanya nitilie mashaka na the rest of the story.. Hebu tupatie uthibitisho wa watu unaowaongelea na vikao unavyoripoti ni sahihi..

Tupe proof ya mama kuwa Jburg. How authentic is the Joburg journey
 
" LIKE FATHER LIKE SON" kwa mtazamo ni vipi Makamba anatofauitana na Januari? Naitamani siku ile ya kutoa hukumu ya vipingamizi vya wana CCM, naitamani siku hiyo nione Makamba atafanyaje juu yake na Januari wake?
 
Hapa na yeye atatoa kama ya Kubwa: Ame kwenda kumsaidia mtoto kifamilia na si kichama.....! Na fedha alizotoa si za kuhonga bali kuwasaidia wana kijiji wenzie.. Mwenye kesi ya Kuhonga atakuwa mwanae endapo atatoa fedha ili achaguliwe na si Mzee Makamba kwani yeye hagombei lolote pale..!!!
 
Bado kuna watu wanaendelea kutengeneza tabaka la kwamba wao ni watawala tuuu..
Huu sio usultani..afu dogo kabebwa Ikulu kaona hapafai bora ubunge..hivi Januari hata akienda bungeni unategemea ajenge hoja gani ya kumsaidia mwananchi???
Hakuna ataendeleza yaleyale Naunga mkono hoja 100 kwa 100..
Bumbuli amkeni anza kuwanyoosha hawa...
 
Hawa watoto wa viongozi watashikwa mikono mpaka lini? hata kama ni vilaza vipi. Hawawezi kutafuta njia zao wenyewe mpaka wategemee baba zao. Inakera ka nini vile. Halafu litasimama mbele za watu na kujidai. Hovyooooooooooooooooooooooooooo

Mangi, hivi wewe ukigombea/uitangaza nia, baba yako au mama yako hatakusaidia?
 
Mangi, hivi wewe ukigombea/uitangaza nia, baba yako au mama yako hatakusaidia?

Kwa nafasi ipi aliyonayo mama??? koz hapa si swala la mzazi kumsaidia mwana...swala ni demokrasia...Sasa kama yeye Makamba ni katibu wa ccm na anampigia debe mwanae sasa swali Makamba atamchukuliaje mwana ccm mwingine mwenye nia kama ya Januari??? au tayari yeye januari keshapitishwa kuwa mgombea pekee kwa tkt ya ccm jimbo la Bumbuli??? kama makamba asingekuwa na influence kwa wagombea wengine katika chama cha mapinduzi thats well n good...but he shud understand who is within ccm
 
Mangi, hivi wewe ukigombea/uitangaza nia, baba yako au mama yako hatakusaidia?

Dah!

Sasa kama dokta unashindwa kuona tatizo dogo kama hili utaweza kweli kuona matatizo makubwa huko mbeleni ukishakuwa na madaraka ndugu yangu?

Tatizo lililoko hapo ni conflict of interests; nitakueleza.

Kwa mangi, mimi na wewe, ni kweli hamna tatizo kabisa kama mama na baba zetu watatusaidia katika kampeini kuwania ubunge. Lakini kwa Januari makamba kuna tatizo kubwa sana kufanyiwa kampeini na baba yake kwa vile atakuwa anajivua neutraily anayotakiwa kuwa nayo kwa wagombea wote kutokana na madaraka yake kama Katibu mkuu wa CCM, ambaye ndiye mlezi wa wagombea wote equally.

Kuna fundisho moja kuwa "great power comes with responsibility;" hiyo responsibility ndiyo inayomzuia makaba asimfanyie kampeini mgombea yeyote hata kama ni mwanae kwa vile ana great power ndani ya CCM. Kiona ulazima wa kumpigia kampeini mwanawe basi ni lazima ajivue madaraka aliyokuwa nayo ndani ya CCM.


Watu wasiojua maana ya conflict of interests ndio wakishakuwa na madaraka wanayatumia kwa ajili ya kusaidia ndugu zao tu na kusahahu raia wengine.
 
Kwa muda mrefu kumekuwa na rummors hapa JF kwamba January Makamba anatarajia kugombea ubunge katika jimbo la Bumbuli. Hatimaye leo kaweka mambo hadharani. Mcheki kwenye link hii
 
Well done January! I think he is a hard working person and his involvement in Tanzania politic circuits makes him be even more qualified for the sought after role. Namtakia mafanikio mema kwenye kampeni.

Steve Dii
 
Mimi nimekunwa na point moja. Kwamba ameamua kuandika kitabu juu ya Bumbuli na mustakabali wake katika lugha ya Kiingereza akiwalenga wale wanaoishi nje ya Bumbuli na Tanzania, na baadaye ndipo kitafsiriwe kwa Kiswahili kuwalenga Watanzania na wakazi wa Bumbuli wasiojua king'eng'e. A very telling point.
 
Ninamkubali huyu kijana kwa uwezo wake wa kupangilia mambo. Though sina uhakika sana kama anaweza kwenda bungeni na kutetea maslahi ya Taifa against system iliyopo ilihali na yeye ni mwanachama wa hiyo system.
 
Kila la kheri Januari, ila ni kwa vipi hutatumia wadhifa wa baba yako na ushawishi wa nafasi yako kuwa karibu na Mkuu wa nchi kufanya kampeni chafu zidi ya wagombea wenzako, kuna ripoti kuwa wazee wako wanakukingia kifua, nachelea kusema kuwa you are not qualified with in the principles of natural justice, hujasema bado wala kubainisha ni kwa vipi hilo halipo na halitatokea ili ufikie malengo yako on merit na si kwa influence za 'wazito' waliokuzunguka, otherwise hongera kwa uamuzi wako.
 
Ninamkubali huyu kijana kwa uwezo wake wa kupangilia mambo. Though sina uhakika sana kama anaweza kwenda bungeni na kutetea maslahi ya Taifa against system iliyopo ilihali na yeye ni mwanachama wa hiyo system.

Hili nadhani ndilo swali kubwa wengi wetu tunalojiuliza. Iweje mtu ambaye ana-hang na ku-dine na wengi wanaopelekea Taifa letu liendelee kusota hapo hapo awe tofauti?! Tuwapinge vipi wahenga wengi na usemi wao wa mtoto wa nyoka ni nyoka?! Maswali ni mengi...mwenye jibu ni January pekee!
 
Mimi nimekunwa na point moja. Kwamba ameamua kuandika kitabu juu ya Bumbuli na mustakabali wake katika lugha ya Kiingereza akiwalenga wale wanaoishi nje ya Bumbuli na Tanzania, na baadaye ndipo kitafsiriwe kwa Kiswahili kuwalenga Watanzania na wakazi wa Bumbuli wasiojua king'eng'e. A very telling point.

....mmmmh, is this a case for patriotism or nationalism?!
 
Itakua ngumu kwake kutoka kwenye kivuli cha baba ake na raisi anayefanya nae kazi kwa karibu. Hata iweje ushindi wake utaonekana ume changiwa kwa kiasi kikubwa na watu waliomzunguuka. Hato weza kuji tofautisha nao wakati huu wa kampeni kwa sababu na amini kama binadamu ata tumia advantages zote alizo nazo apate huo ubunge kwanza ndiyo mengine yafuate.

Kama aki "bahatika" kushinda ubunge hukumu yake itakua hiyo miaka mitano ata kayo kuwa nayo kuji tofautisha na kivuli kikubwa kinacho mfunika. Ita chukua muda na kazi kweli kufanya hivi. Kwa kiasi fulani naona advantages alizo nazo kama mtoto wa fulani ndizo zitakazo kuwa disadvantages zake kwenda mbele.

Uzuri ni kwamba hao ambao sasa hivi wana mkingia kifua hawata baki madarakani milele. Baba yake si raisi mstaafu kwa hiyo sidhani kama atakua na advantages za wakina mtoto wa Karume na Mwinyi pindi mzee wake Makamba aki toka madarakani. Kwa maana hiyo iwe isiwe lazima merit zake zi "kick in" at some point kwa maana bila hivyo hato fika mbali kisiasa.

So far I give him the benefit of the doubt. He seems like a smart fellow. Sitaki kumhukumu kiharaka haraka kwa sababu ya jina lake la mwisho. Ngoja tumuone kati ya sasa na kampeni ata leta nini mezani. Mtu hawezi kujificha rangi zake za kweli kwa muda mrefu.
 
....mmmmh, is this a case for patriotism or nationalism?!
Steve,
Point yangu ni kwamba kama audience yake ya kwanza ni Watanzania, angeandika Kiswahili. Baadaye, kama wale wa nje wanataka kujua falsafa yake na matatizo ya Bumbuli kuna muda wa kutosha kufanya tafsiri kwa Kiingereza. Lakini hapa naona wa nje ni muhimu zaidi ya wa ndani.
 
Back
Top Bottom