nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
Na Waandishi Wetu, jijini Habari LEO
ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba, ambaye alijiuzulu wadhifa huo hivi karibuni baada ya kukitumikia chama na Serikali kwa miaka 50, amesema imetosha na anafunga mdomo.Akizungumza leo asubuhi kwa njia ya simu, Makamba amesema ameongea vya kutosha na anawaheshimu viongozi waliopo madarakani kwa hiyo sasa anawapisha wengine nao waendelee kuongea.
Kwa sasa sina la kuongea. Nimeshaongea sana katika miaka yangu 50 ya kuitumikia Serikali hii. Sasa inatosha, amesema Makamba.
Makamba aliyasema hayo mara baada ya kupigiwa simu na ili aweze kufafanua zaidi kuhusu suala lililoibuka ndani ya CCM la kujivua gamba na mwelekeo wake baada ya kustaafu wadhifa huo.
Hata hivyo, mara kwa mara Makamba aliendelee kusisitiza kuwa hana kauli kwani hivi sasa amefunga mdomo na ahitaji tena kuzungumzia suala lolote.
Hivi karibuni safu ya viongozi wa chama hicho walijiuzulu katika mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM uliofanyika mjini Dodoma.
Kujiuzulu kwa viongozi hao kulitokana na chama hicho kudaiwa kwenda mrama kutokana na utendaji wao kuwa mbovu pamoja na ushauri.