Makamba asema amefunga mdomo

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Na Waandishi Wetu, jijini Habari LEO

ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba, ambaye alijiuzulu wadhifa huo hivi karibuni baada ya kukitumikia chama na Serikali kwa miaka 50, amesema imetosha na anafunga mdomo.Akizungumza leo asubuhi kwa njia ya simu, Makamba amesema ameongea vya kutosha na anawaheshimu viongozi waliopo madarakani kwa hiyo sasa anawapisha wengine nao waendelee kuongea.

“Kwa sasa sina la kuongea. Nimeshaongea sana katika miaka yangu 50 ya kuitumikia Serikali hii. Sasa inatosha,” amesema Makamba.

Makamba aliyasema hayo mara baada ya kupigiwa simu na ili aweze kufafanua zaidi kuhusu suala lililoibuka ndani ya CCM la kujivua gamba na mwelekeo wake baada ya kustaafu wadhifa huo.

Hata hivyo, mara kwa mara Makamba aliendelee kusisitiza kuwa hana kauli kwani hivi sasa amefunga mdomo na ahitaji tena kuzungumzia suala lolote.

Hivi karibuni safu ya viongozi wa chama hicho walijiuzulu katika mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM uliofanyika mjini Dodoma.

Kujiuzulu kwa viongozi hao kulitokana na chama hicho kudaiwa kwenda mrama kutokana na utendaji wao kuwa mbovu pamoja na ushauri.
 
Huyo mzee ndiye aliyeharibu ccm hasa tabia yake ya kulea makundi ndani ya chama ,hii zmabi itamtafuna had mwisho
 
Angeendelea kutoa pumba zake!maana ni commedian mzuri wa kuchekesha
 
utu uzima dawa ndio maana anamua kunyamaza maana akiongea neno lolote sasa hivi litatafisiriwa ndivyo sivyo. bora afunge kapu lake mzee watu
 
Awe emsii wa harusi nk ni kazi nzuri na inalipa na anaiweza

:happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy::happy:
 
Ni vizuri akae kimya, kwasababu alishindwa kutambua kwamba viatu alivyopewa vinampwaya. Kama utendaji wake ungekuwa umetukuka nafikiri angekabidhiwa rungu kusimamia zoezi zima la kujivua gamba. Vile vile ni vizuri akae kimya kwa sababu huwa ana tabia ya kuzungumza mambo akikosa umakini na kusababisha kauli zake kuchukuliwa na kuzidi kudidimiza chama chake.Kwa msingi huu nafikiri AMESHAURIWA KAMA SIO KUSHURUTISHWA kukaa kimya.
 
Siyo kwamba kuna namna 'wamemfunga' mdomo? Basi wamshauri atafute super glue augundishe kabisa.
 
Huyo makamba ameropoka sana alafu kagundua alikuwa anauzwa mwache mjinga kagundua ni mjinga:israel:
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom