Makamba aibuka

Kumbe chama huwa kinakuja na mbinu za kushinda na sio sera za kulivusha taifa katika mabalaa! Hii kali, na apo ayo manano yametoka kwa aliyekuwa mtendaji mkuu wa chama. Mungu ibariki Tanzania.
 
hahahahhahhaaaa the spinning pro., aliwakomesha kweli hao waandishi wa habari!

Mimi namuona huyu Makamba kama msaliti wa CCM kwa kuweka wazi kuwa CCM ni chama cha kisanii na uwongo dhidi ya wapiga kura. Yaani unawadanganya wananchi ili wakupigie kura?. Kwa vyovyoye ilivyo CDM hata ingesema itatoa mfuko wa Cement bure bado haiwezi kuonekana kuwa ilikuwa inadanganya kwani haijapewa nafasi ya kuonesha kuwa imeshindwa kwa kuwekwa madarakani. 2015 bila chakachua ya +51% CCM will lose.

Siasa si mchezo wa uhuni wa kudanganya watu bali ni mchezo wa kuonesha watu kuwa unafanya kila liwezalo kuhakikisha maisha ya wananchi yanaboreka, kwa CCM imeshindwa yote.
 
Yule kibabu aliyepata kuwa katibu mkuu wa CCM Luten Yusuf Makamba ameibuka baada ya kimya cha mda mrefu na kuwaasa watanzania waache kufikiri kwamba wanaishi peponi kwa kulalamika kila siku kuwa maisha ni magumu na badala yake wafanye kazi kwa bidii kwani hata huko peponi nako kuna kazi.

Vilevile amewataka waache kumlalamikia Rais J.M.Kikwete kwamba kashindwa kuyafanya maisha yao kuwa bora,kwani hilo si jukumu la rais Kikwete bali ni jukumu la kila mwananchi kunyanyua maisha yake bila kuitegemea serikali au Rais J.M.Kikwete.Alipoulizwa ni kwa nini wakati wa kampeni rais Kikwete alitoa ahadi ya maisha bora kwa kila mtanzania wakati anafahamu kuwa huo sio wajibu wake.

Makamba alidai kuwa siasa ni mchezo na kila mchezo una mbinu na hiyo ilikuwa mbinu ya rais kikwete na chama chake ili aweze kuchaguliwa kwani hata ahadi alizokuwa anatoa Dk.Slaa ya mfuko wa cement kuwa 5000/=kwa mfuko haiwezekani bali ni mbinu ya mchezo wa siasa.

SOURCE;Gazeti la Jambo Leo ukurasa wa 4.

My take; Mzee umri unamtupa mkono vibaya mno kama kweli haamini kama kazi kubwa aliyonayo rais wa nchi ni kuboresha hali ya maisha ya watu wake.

mzee makamba karudi kuwapigia wanaye debe....... hamjui bila wanaye tanzania haiendelei?
 
Makamba alidai kuwa siasa ni mchezo na kila mchezo una mbinu na hiyo ilikuwa mbinu ya rais kikwete na chama chake ili aweze kuchaguliwa

hahaaaah Makamba ndie mwanaccm mwenye akili kuliko woote ni role model wa wengi katika chama kile

166649_193157790700856_100000199094899_825364_4376743_n.jpg
 
Kutamka kuwa 'Watanzania waaache kulalamika na kufanya kazi' ni kuwadhalilisha. Je ina maana kuwa Watanzania ni wavivu? Ninaamini kuwa Watanzania ni wachapakazi mno na ndio maana wameweza kustahimili shida zote hizi zinazowakabili kwa miaka yote. Wamelea na kusomesha watoto wao na kujipatia riziki zao kila siku, wamejenga nyumba zao bila mikopo n.k bila msaada wowote.

Kuna siku nilikuwa nasafiri kwenye ndege kuelekea Ulaya, pembeni yangu alikaa Mmarekani. Katika mazungumzo yetu alibainisha kuwa ilikuwa ni safari yake ya kwanza kuja Tanzania. Nilipomuuliza ni kitu gani ambacho atakikumbuka kuhusu Tanzaniai, akasema kuwa kitu alichoona ni kuwa hajaona watu wanaofanya kazi sana kama Watanzania na wanafanya kazi hizo katika mazingira magumu.

Mtu anafanya kazi akiwa na malengo fulani. Kama yale malengo yake hayafanikiwi kutokana na juhudi za kazi zake, inabidi akae chini afikirie kwa nini hafanikiwi. Kuendelea kufanya kazi tu bila kutathmini matokeo ya kazi unayofanya si sahihi. Watanzania wanatathmini juhudi zao, kama wanaona hawayafikii malengo yao 'wanalalamika'. Katika hilo kulalamika ni sahihi. Ni mtumwa tu ndie asiyelalamika akifanyishwa kazi. Lakini hata akichapwa mjeledi, kilio chake cha maumivu ni kulalamika.
Yeye Makamba ndie mvivu kwa maana binti yake alikuwa anamuombea kaka yake dolari 2 million kwa ajili ya kampeni za ubunge kwa shemejie,sasa hapo inaonyesha Makamba na Co walivyo wavivu
 
Please JF....si kila HABARI NI HABARI....
Makamba is NOT NEW, has NO NEWS, & NO VIEWS, he is LONG TIME CONFUSED HIMSELF, lost mentally luckly still alive, hajui anasema nini, na nani, wapi, nyakati gani regarding life trend ya leo, HUYU KHERI YA LYATONGA MREMA, Makamba 101% kibabu kimechanganyikiwa, kazi yake KUOA TU WANAWAKE.... vacuum headed Makamba.... na tunakuwa maskini kuongozwa na watu kama hawa, HANA MISSION, VISION, he is MATONYA OF POLITICS...atuambie KWANINI ALIKIMBIA UALIMU.?

Yule kibabu aliyepata kuwa katibu mkuu wa CCM Luten Yusuf Makamba ameibuka baada ya kimya cha mda mrefu na kuwaasa watanzania waache kufikiri kwamba wanaishi peponi kwa kulalamika kila siku kuwa maisha ni magumu na badala yake wafanye kazi kwa bidii kwani hata huko peponi nako kuna kazi.

Vilevile amewataka waache kumlalamikia Rais J.M.Kikwete kwamba kashindwa kuyafanya maisha yao kuwa bora,kwani hilo si jukumu la rais Kikwete bali ni jukumu la kila mwananchi kunyanyua maisha yake bila kuitegemea serikali au Rais J.M.Kikwete.Alipoulizwa ni kwa nini wakati wa kampeni rais Kikwete alitoa ahadi ya maisha bora kwa kila mtanzania wakati anafahamu kuwa huo sio wajibu wake.

Makamba alidai kuwa siasa ni mchezo na kila mchezo una mbinu na hiyo ilikuwa mbinu ya rais kikwete na chama chake ili aweze kuchaguliwa kwani hata ahadi alizokuwa anatoa Dk.Slaa ya mfuko wa cement kuwa 5000/=kwa mfuko haiwezekani bali ni mbinu ya mchezo wa siasa.

SOURCE;Gazeti la Jambo Leo ukurasa wa 4.

My take; Mzee umri unamtupa mkono vibaya mno kama kweli haamini kama kazi kubwa aliyonayo rais wa nchi ni kuboresha hali ya maisha ya watu wake.
 
Ishu ni kwamba watanzania tumezidi kulalamika kwamba JK ni tatizo wakati sio kweli!! Mtu ni mfanyakazi wa serikali, shifti yake ni ya mchana, unamkuta saluni saa tano asubuhi siku ya kazi, anafanya scrub huku anamlaumu rais kishenzi!!!! Anamaliza scrub anaenda lunch akiwa huko anapanga mkakati wa jinsi ya kupata cha juu kwenye manunuzi ya computer za idara yake, akitoka huko anaenda kusaini kwa keshia pale kazini kwake alipwe posho ya kukaa kwenye kikao ambacho hakuchangia chochote (wazo lolote). Muda wa kazi umeisha anarudi nyumbani. Sasa anamlaumu raisi wa nini? hiyo hali nzuri anaipataje kwa kulipwa kwa kutofanya kazi? si anaiibia nchi huyo? rais anajengaje uchumi imara kwa watu wake ambao kazi yao ni kuiibia serikali (kujiibia wenyewe)? Tuna tatizo la kiuongozi kwa sababu tu serikali imeshindwa kudhibiti watu wasilipwe bila kuzalisha, full stop. Kila mtu anataka kupata pesa za bure, bila kufanya kazi. na mahali pekee unaweza kuiba kirahisi siku hizi ni serikalini!!! tukitaka maendeleo watanzania wote tubadilike kimtazamo kwanza. bila hivyo hata tukipata rais gani haina maana. Vitu vikuu ambavyo ndiyo msingi wa maendeleo wa taifa lolote na ambavyo vimetumika na mataifa yaliyoendelea zaidi kufika hapo yalipo ni:

1. Maadili. 2. Uaminifu. 3. Uwajibikaji. 4. Kuheshimu sheria. 5. Kuheshimu haki zako na watu wengine.
6. Kupenda kufanya kazi. 7. Kupenda kuweka akiba na Kuwekeza. 8. Kwenda na wakati

Hii imekuwa proved kwenye tafiti mbalimbali za kujaribu kutafuta suluhu ya umaskini uliokithiri huku kwetu. Hizi ni kanuni kuu za maendeleo ambazo hazitekelezwi mojamoja bali zinaenda pamoja. Tunahitaji viongozi wanaoweza kutubadili tukazifuata kwa ukamilifu. Itaendelea.
 
Wenzake wanasema uzee dawa kwake yeye nachokiona ni kuzeeka vibaya,na waswahili wanasema kama kwenye ujana ulikuwa ni mnafiki ukiwa mzee utakuwa mchawi ndio nacho kiona kwa huyu mzee.
 
Watanzania bana full of intimidations and all that; hivi kwa ni nini huwa tunakuwa wepesi kuweka hoja pembeni na kuattack mtu hili jukwaa bana linatumiwa tofauti kabisa manake Siasa ni kuvumiliana imagine unamwambia mtu wakati wake unakuja sasa we unazungumzia wakati unakuja ilhali yeye ameshakuwa?? Kwani yeye kasema atakaa hapo maisha yake?? Embu tuwe strict kwenye hoja bana. Niwatake radhi wanajamvi manake na mimi imenipasa nitoke nje ya mada kwa ajili ya kupeana ushauri....
Sasa hapo Kigwangala unaemtetea katoa hoja gani ya kujadiliwa? Kasome tena alichoandika huyo mbunge wako ili ujilidhishe kama ni hoja au *****!
 
Ishu ni kwamba watanzania tumezidi kulalamika kwamba JK ni tatizo wakati sio kweli!! Mtu ni mfanyakazi wa serikali, shifti yake ni ya mchana, unamkuta saluni saa tano asubuhi siku ya kazi, anafanya scrub huku anamlaumu rais kishenzi!!!! Anamaliza scrub anaenda lunch akiwa huko anapanga mkakati wa jinsi ya kupata cha juu kwenye manunuzi ya computer za idara yake, akitoka huko anaenda kusaini kwa keshia pale kazini kwake alipwe posho ya kukaa kwenye kikao ambacho hakuchangia chochote (wazo lolote). Muda wa kazi umeisha anarudi nyumbani. Sasa anamlaumu raisi wa nini? hiyo hali nzuri anaipataje kwa kulipwa kwa kutofanya kazi? si anaiibia nchi huyo? rais anajengaje uchumi imara kwa watu wake ambao kazi yao ni kuiibia serikali (kujiibia wenyewe)? Tuna tatizo la kiuongozi kwa sababu tu serikali imeshindwa kudhibiti watu wasilipwe bila kuzalisha, full stop. Kila mtu anataka kupata pesa za bure, bila kufanya kazi. na mahali pekee unaweza kuiba kirahisi siku hizi ni serikalini!!! tukitaka maendeleo watanzania wote tubadilike kimtazamo kwanza. bila hivyo hata tukipata rais gani haina maana. Vitu vikuu ambavyo ndiyo msingi wa maendeleo wa taifa lolote na ambavyo vimetumika na mataifa yaliyoendelea zaidi kufika hapo yalipo ni:

1. Maadili.2. Uaminifu.3. Uwajibikaji.4. Kuheshimu sheria.5. Kuheshimu haki zako na watu wengine.
6. Kupenda kufanya kazi.7. Kupenda kuweka akiba na Kuwekeza.8. Kwenda na wakati

Hii imekuwa proved kwenye tafiti mbalimbali za kujaribu kutafuta suluhu ya umaskini uliokithiri huku kwetu. Hizi ni kanuni kuu za maendeleo ambazo hazitekelezwi mojamoja bali zinaenda pamoja. Tunahitaji viongozi wanaoweza kutubadili tukazifuata kwa ukamilifu. Itaendelea.

rais analaumiwa kwa kutochagua waendeshaji wazuri mawizarani ambao wangehakikisha watusmishi hawachezi wakiwa makazini kwao. Unadhani ukiwa na katibu mkuu makini nani ataondka kwenda saluni? ukiwa na waziri kama magufuli nani anaenda kucheza? Rais lazima alaumiwe kwa maana ni hovyo
 
Wewe inakusaidia nn waandishi wa habari wakikomeshwa? Mtu mzima ovyoo

Aisee..this is not facebook. Hawa viongozi wanoingia humu wakajaza pumba watambue kuwa humu wanakaa watu wenye uelewa mpana sana tofauti na facebook..waondoe maneno ya kitototo humu.., Heri kule kwao status zao zinaonekana kwa marafiki tu..lakini humu ni public.
 
Babu Makamba vip?
Watu wanaleta cement toka mashariki ya mbali inafika hapa kwa 9000 kwa mfuko sembuse yetu kuuzwa 5000 kwa mfuko!
Alafu jipumzikie kwa amani tuu!
 
hivi kila siku tunaposema kuna ombwe la uongozi hamuamini,sasa limejitokeza tena jingine tena toka kwa mwakilishi wa wananchi napo mnasemaje kama si ombwe la fikra?

WISDOM IS BETTER THAN SILVER & GOLD IN THE BRIGDE
 
hahahahhahhaaaa the spinning pro., aliwakomesha kweli hao waandishi wa habari!

Unamuita pro... nini mana yake au ndo Profesa wa CCM?

Musaidie kutueleza sababu zilizomfanya afukuzwe ualimu. Mpaka leo hajasema lolote.
Au nayo ni mbinu ya kutukomesha?
 
Hivi kuna watu mmetumwa hapa JF kunishughulikia ama basi mnanichukia tu? Mbona hata hoja nyingine hazina maana mnaanza tu kunitukana...acheni hizo, fanyeni bidii kidogo ya kufikiri! Sasa mimi kusema nimefurahishwa na majibu ya kisiasa ya Mzee Makamba ni kosa? Kweli alifanya spinning kwenye maneno yake na alifanya vizuri

Nasema aliwakomesha si kwa nia mbaya, ni kwamba hakuwapa kile walichokitarajia, aliwakwepa...

Ntogwisangu ndg yangu kumbe wewe ni mtu wa MUCHS enzi zile, sasa matusi na kashfa zote unazonirushia ni za nini? Wewe si brother yangu kabisa, hauoni hata aibu unavyonishughulikia hapa jukwaani bila sababu ya msingi? Mimi sikuchukii wala sikumaind bali nakuhurumia na kukuombea upate uelewa...hivi haujawahi hata kuona ni jinsi gani nime-dedicate maisha yangu katika kuikoa fani yetu ya udaktari? Umenisikitisha sana kwa kweli! Kuwa fair, hata kama hutaki kunisifia (ambacho sikuombi ufanye) basi walau usinikashifu, maana mimi hata kama ningekujua nisingekukashfu kwa kuwa wewe ni ndg yangu. By the way, nilikuwaga siendi kuoga Lukuledi, nilikuwa naenda kuoga Kagera, nalala Pangani (kwa mchumba wangu - ambaye leo hii ni mke wangu na mama wa watoto wangu). Nilikuwa nahangaika tu na maisha wala hayo si mambo ya kushabikia kaka, ni umaskini tu wa kwangu binafsi na wa nchi yangu ndiyo maana nilikosa mahala pa kuishi nikalazimika kuishi chuoni kwenye chumba cha mchumba wangu!
 
Wewe inaonekana umeingia bungeni bila kutafakari na kujua kwamba public service inataka mtu kuji conduct in an exemplary fashion. Kama ulikuwa na kauli za rejareja za kijiweni ukishaamua kuwatumikia watu unaziacha. La sivyo utaonekana hufai.

Kumwita Makamba "master spinner" si kumsifia, ni kumtukana. Ni kusema Makamba ni mtu fulani kawekwa pale kupinduapindua maneno.

Kuangalia haya mambo kama "kawaweza waandishi wa habari" "kawapatia" unaonyesha akili za kitoto, za kufikiri haya masuala ni ya ligi za "kushindana" na "kupatiana" wakati watu wanaongelea vitu vya msingi kuhusu hali ya watanzania.

Kusema "hakuwapa kile walichotarajia, aliwakwepa" bila aibu, kunaonyesha hujakomaa kisiasa na huamini katika siasa za uwazi. Unaamini katika siasa za kuspin na kukwepa maswali magumu.

Wewe na huyo Makamba wote akili zenu fupi, ndiyo maana wewe unamsifia.

Kwa sababu mtu mwenye kufikiri kwa marefu na mapana ataona alichosema Mkamba pale kimemvua nguo Kikwete. Makamba kasema kwamba Kikwete si mtu serious, hakuwa na nia ya kumaliza matatizo ya Watanzania aliposema ataleta "maisha bora kwa kila Mtanzania" bali Kiwete alikuwa anatumia maneno matamu tu kupata kuchaguliwa, lakini hana nia hiyo.

Wewe ndio unaona huyu ni mtu wa kusifiwa huyu?

Huyu anayempaka bosi wake matope ndiye mtu wa kusifiwa?

Wewe nawe unatetea siasa za ulaghai? Kwadanganya wananchi ili uchaguliwe ilhali huna nia wala uwezo wa kutatua matatizo?

Huyu mzee wanaomtetea wanasema "senile" tayari if you know what I mean. Hata wanawe wenyewe huwaoni kuja kumtetea hapa publicly. Lakini utaona wapambe nuksi. Bongo hatuna meritocracy kwa hiyo watu wanatafuta kupanda ngazi kwa kujikombakomba tu.

Why? Hat huyo rais mwenyewe hana merit, kapanda ngazi kwa kujenga image ya "kijana mzuri". Lahaula!

The irony here is that Makamba is probably right. He is a fool. He is a fool who does not know that what he is saying is the truth that is exposing the emperor as being naked. Now, this is a convoluted way of getting at the truth, for a court jester to out his master like this, and a pretender to join the bandwagon just because of his boiling bile twards the press, this is quite revealing.

One has to wonder if these jokesters have the nerves to declare this type of despicable discourse in public, what type of obscene obliteration do they plan in private?
 
Back
Top Bottom