The Invincible
JF-Expert Member
- May 6, 2006
- 6,003
- 3,269
Mzee Mtei siku zote kumbuka kuwa kumsema mwenzio ni raha saaana na kusemwa wewe ni chungu mno.
Wewe Mwl hakukupa fursa ya kukusikiliza na badala yake ukatimuliwa (though wewe unadai ulishaamua kuacha kazi pia). Au nikuulize, je wakati unatimuliwa kulikuwa na demokrasia? Ulisikilizwa kama ulivyostahili? Je wale wanaotuhumiwa kwa ufisadi na kesi zao zipo mahakamani wanaposemwa kwenye majukwaa ya kisiasa unafikiri wanajisikiaje? (nchi yetu ni ya utawala wa kisheria kumbuka) Ungekuwa ni wewe unatuhumiwa tu (na moyoni unajijua hauko fisadi) unaposemwa hadharani utajisikiaje?
Tufikirie leo viongozi au wagombea wa vyama wanaanza kutuhumiana kwa tuhuma binafsi tutakuwa tanatathmini nini? Tuhuma ama hoja za kuleta maendeleo? Kama CCM walivyo na mapungufu hata Chadema pia mnayo, think about tribalism scandals, ufisadi wa Mbowe (two years ago), (au unataka kusema mliliona hilo ndiyo maana mkaamua Mbowe asigombee Uraisi?), uadilifu ktk maisha ya kindoa n.k. Kumbuka kwa kila mahali kuna aina ya watu tofauti tofauti, kuna wazuri na wabaya, wema na wasio wema, wezi na waibiwa, na kadhalika na kadhalika.
Unaweza ukawa mwanzilishi wa Chama ukifikiria kuwaletea watu wako mabadiliko ya kiuchumi kumbe wenzako ulio nao pamoja wanafikiria Chama hicho hicho kitawafanya wachumie matumboni mwao. Kama ilivyo CCM hata nanyi Chadema ni vivyo hivyo. Hata mabadaliko mnayoyasema yataonekana kwa siku 100 ni ndoto tu, its just a gear of bringing political change rather not solving core problems facing our country!
Usitudanganye sana Mzee Mtei! kuwa halisi, Sio wote tunakubaliana na wewe!
Tunajua mmejipanga wengi wa aina yako kama sisimizi. Hapa ni spray tu ya kuwafutilia mbali. Shwain.