Majina ya waliopendekezwa kugombea EAC kutoka CCM

Huwa namkubali Hussein Mwinyi tu huyu ndiyo naamini anasimama kwa miguu yake na Elimu yake haina walakini. hawa wengine kama kina William Malecela walipaswa kuwa Mameneja wa Ngwasuma.
 
Wanachama
kadhaa wa CCM wamesikitishwa na majina ya wanachama waliopitishwa
kuwania ubunge wa Afrika Mashariki.Wamesema kwamba kitendo cha chama
chao kupitisha idadi kubwa ya majina ya watoto wa vigogo ni ishara
tosha kwamba chama chao kimegeuka kuwa cha kisultani.Pia wamesema
kitendo hiki kitazidi kuwaweka mbali na wananchi.Baadhi ya watoto wa
vigogo waliopitishwa ni mtoto wa Nyerere,mtoto wa Mwinyi,mtoto wa
Billali na mtoto wa Malecela.SOURCE:TANZANIA DAIMA.


nimelisoma tanzania daima na hakuna popote linapotaja wanachama kusikitika.
 
1. Mwinyi
2. Bilal
3. Malecela
4. Nyerere
5. Makame
6. Abdulaziz n.k
Hii ndo demokrasia Does matter who you are but who is behind you.
 
"Babu alikuwa mwalimu; baba na mama walikuwa walimu, mtoto ni mwalimu," hakuna kosa.
"Babu alikuwa daktari; baba na mama walikuwa madaktari, mtoto ni daktari," hakuna kosa.
"Babu alikuwa mwanasiasa, mama na baba walikuwa wanasiasa...," mtoto kuwa mwanasiasa kuna kosa gani?
 
Inawezekana mimi ni mbaguzi sana, kati ya hao watoto wa wakulima wachini waliosoma kwa kubangaiza ni wangapi?
Taja majina yao.
 
huo ni upotoshaji wa makusudi,walitangaza nafasi hizo na watu wamejitokeza kuchukua fomu na kuomba,kinachofuata ni mchujo wa wale wenye SIFA stahili kupitishwa bila kujali ni mtoto wa kigogo gani....hao ni wateule tu bado hawajachaguliwa,pia hata wakichaguliwa bado ni haki yao kama hakuna wenye SIFA zaidi yao.Mnataka tuwakatae ati kwa sababu ni watoto wa vigogo? basi hata ajira wasipate kwenye taasisi za serikali wala mashirika yoyote? HAPANA huo ni ufinyu wa FIKRA....Acheni TANZANIA DAIMA wafanye SIASA kwa vile ni kazi yao,Lakini Great THINKERS let us go beyond the SKY.....

Mkuu mie linalonipa hofu ni historia zao.. Jee wamewahi kushiriki kwenye shughuli zozote za kiungozi..? Haiwezekani hata umonitor hajawahi kuupata kuupata halafu leo agombee cheo kikubwa cha kisiasa..! Kwa hiyo unakuja kuona wanabebwa na wazazi wao kuingia kwenye siasa.. Kwa njia hii hatuwezi kumpata kiongozi bora na mwenye malengo mazuri na nchi yake.. Utakuwa ni utamaduni wa kulindana tu..
 
full nepotism

That's how it smells. Ukiangalia majina hayo unaanza kuwa na hofu, unaona kuwa baadhi ya watu hapa Tanzania kazi yao ni siasa tu. I wonder kama watu hao waliopendekezwa walipendekezwa kwa kigezo cha kuweza kuiwakilisha Tanzania, au kwa kuwa na uwezo wa kusimama kwenye jukwaa la siasa Afrika Mashriki, au ndio yale yale ya huyu ni mwenzetu mtoto wetu kijana wetu. We never learn, Kenya watakuwa wanachekelea tu.
 
Wanachama kadhaa wa CCM wamesikitishwa na majina ya wanachama waliopitishwa kuwania ubunge wa Afrika Mashariki.Wamesema kwamba kitendo cha chama chao kupitisha idadi kubwa ya majina ya watoto wa vigogo ni ishara tosha kwamba chama chao kimegeuka kuwa cha kisultani.Pia wamesema kitendo hiki kitazidi kuwaweka mbali na wananchi.Baadhi ya watoto wa vigogo waliopitishwa ni mtoto wa Nyerere,mtoto wa Mwinyi,mtoto wa Billali na mtoto wa Malecela.SOURCE:TANZANIA DAIMA.

Na hao ambao sio vigogo mbona hamuwaambii wajitokeze.
Watu wa ajabu sana hivi hata malaika akigombea watu watalalamika badala ya kuwa proactive.
Swali: mlitaka nani agombee?
 
Wanachama kadhaa wa CCM wamesikitishwa na majina ya wanachama waliopitishwa kuwania ubunge wa Afrika Mashariki.Wamesema kwamba kitendo cha chama chao kupitisha idadi kubwa ya majina ya watoto wa vigogo ni ishara tosha kwamba chama chao kimegeuka kuwa cha kisultani.Pia wamesema kitendo hiki kitazidi kuwaweka mbali na wananchi.Baadhi ya watoto wa vigogo waliopitishwa ni mtoto wa Nyerere,mtoto wa Mwinyi,mtoto wa Billali na mtoto wa Malecela.SOURCE:TANZANIA DAIMA.
Hilo ni kweli sasa kama wameona taizo kinachofuata ni kutafuta dawa!!! hatuwez kuendelea kwa staili hizo!!! wakati ni huu!!!
 
Mzee Makamba alipata kusema ukimkuta panya anakula Biblia Msikitini utashangaa, lakin kama ukimkuta anaila kanisani wala huwezi kushangaa (the same apply kwa Quran na Kanisa). Nadhani hawa vijana watakuwa wanafuata nyayo za wazazi wao, hata hivyo kwangu mimi si tatizo kama watakuwa wanasifa stahiki na wanafuata taratibu zote walizojiwekea bila kubebwa kwani nao wana haki hizo za kuchagua viongozi na kuchaguliwa

Hata hivyo ni vyema ikafahamika kwamba huko kwenye chaguzi zao za ndani, hawapigiwi kura na hao wazazi wao pekee bali wanachama wenzao, hivyo hakuna haja ya kumlaumu mtu mwingine bali wajilaumu wenyewe kwa kuiacha misingi yao ya awali kama watakuwa wamekiuka taratibu

Sioni sababu ya wewe kuwa na ujasiri wa kuwatetea hao watoto wa vigogo! je hujui kinachotokea kwenye chaguzi zao za ndani?? watu wanapewa pesa na mashinikizo ya hali ya juu na kumkatisha tamaa yoyote atakae jitokeza kupambana nae kwenye uchaguzi.Yote hayo yapo wazi.Mie nadhan wakati umefika wakae pembeni watafute na kazi nyingine zenye utalamu walio usomea!!! wao si wamesomea nje ya nchi!!! tabu ya nn??
 
Mie sijaliona gazeti, ila hapo juu wanadai habari imepotoshwa, sio kama ilivyo hapa. Sasa najiuliza:
Bado tunajadili?
Watoto wa vigogo nao ni watanzania tena wanabahati ya kupata habari kuhusu hio nafasi na wameomba tayari kama wengine wengi
je watanzania wengine tulisikia au ilikuwa siri?
Je hayo majina ni shortlist ya waliokidhi vigezo au ni list ya wote walioomba?
Hv wakati wakupiga kura, kuna chance hao wapiga kura wakamuacha mtoto wa 'mwenzao' wakampa mtoto wa machinga wasiemjua?
Je cv zilizowakilishwa zilihitaji experience ya uongozi? Siasa? Kufanya kazi za jamii?
 
Kumbe na wewe kibaraka umeona hilo eeh?
Cha msingi ni kuwachuja wote na kubakiza raia wa kawaida!
Hivi hakunaga kazi zingine za profession zao?

Na we umeonaa eeh, yaani they all wanna be politicians; Babu, Baba, Mama, Mtoto, Wajukuu... aint there anything else they can do apart from politics.. alafu wana claim 'TAIFA KWANZA'.. damn them. Kwa nini wasiende kwenye KILIMO KWANZA to show da way???&&&****%%$$$$ damn%%%$$$"""&***
 
Kama watanzania watakuwa makini, kamati kuu ya CCM imewasaidia kuonyesha sura halisi ya utawala wa kurithishana. Ukisoma kitabu cha The Prince cha Niccolo Machiavelli hutashangaa kinachofanyika Tanzania. Kimsingi Tanzania si nchi tena bali kusanyiko la watu wa hovyo wasioweza kufanya jambo lolote la maana wawe watawaliwa au watawala. Kuna makundi mawili. Waliwa na walaji. Kesho utasikia na wake zao wakigombea ubunge kama alivyoafanya Janet Museveni.
 
Back
Top Bottom