Majina ya waliopendekezwa kugombea EAC kutoka CCM

Kumbe na wewe kibaraka umeona hilo eeh?
Cha msingi ni kuwachuja wote na kubakiza raia wa kawaida!
Hivi hakunaga kazi zingine za profession zao?

Kwani wanasoma? mazuzu wengi, wanalala na kusubiri certificate kama mwanaasha
 
Ben hii hongera yako unamaanisha kweli?

hongera ya nini wakt ameshka nafasi kubwa toka kipind cha mwalimu,aache apumzike ili kuwapa nafasi wengine....si yeye tu ktk taifa ili na mzee huyu anauchu sana
 
Huyu jamaa alichakachua mahesabu ya TTCL halafu matokeo yake tukalipwa kiduchu wakati wa ubinafsafsishaji na balance jamaa wakagoma kulipa kwa sababu eti mahesabu yalikaa vibaya!!

Uh?? Kama ni kweli Mndolwa alichakachua mahesabu ya TTCL na tukaishia kulipwa kiduchu basi hatufai maana atatusaliti kwa hao manyangau na hasa ukichukulia tiyari yuko kwenye bodi ya KCB yenye makao makuu kwa hao jamaa.
 
Hii kiboko........,duuuuuuuuuuu kumbe kupeana kama njuguuuuuuu..Kweli hakunaga kama watoto wa vgogo...kwa nn wasipewe raia wa kaida...Wakifika huko ndo kusema na wao kama Sioi waweze kusaidia familia zao na sio kuwatetea watanzania
 
Wanachama kadhaa wa CCM wamesikitishwa na majina ya wanachama waliopitishwa kuwania ubunge wa Afrika Mashariki.Wamesema kwamba kitendo cha chama chao kupitisha idadi kubwa ya majina ya watoto wa vigogo ni ishara tosha kwamba chama chao kimegeuka kuwa cha kisultani.Pia wamesema kitendo hiki kitazidi kuwaweka mbali na wananchi.Baadhi ya watoto wa vigogo waliopitishwa ni mtoto wa Nyerere,mtoto wa Mwinyi,mtoto wa Billali na mtoto wa Malecela.SOURCE:TANZANIA DAIMA.

Mzee Makamba alipata kusema ukimkuta panya anakula Biblia Msikitini utashangaa, lakin kama ukimkuta anaila kanisani wala huwezi kushangaa (the same apply kwa Quran na Kanisa). Nadhani hawa vijana watakuwa wanafuata nyayo za wazazi wao, hata hivyo kwangu mimi si tatizo kama watakuwa wanasifa stahiki na wanafuata taratibu zote walizojiwekea bila kubebwa kwani nao wana haki hizo za kuchagua viongozi na kuchaguliwa

Hata hivyo ni vyema ikafahamika kwamba huko kwenye chaguzi zao za ndani, hawapigiwi kura na hao wazazi wao pekee bali wanachama wenzao, hivyo hakuna haja ya kumlaumu mtu mwingine bali wajilaumu wenyewe kwa kuiacha misingi yao ya awali kama watakuwa wamekiuka taratibu
 
Hili ni tatizo kubwa sana katika mfumo wa uongozi katika chama cha mapinduzi na mimi nashangaa wadau kama kweli tunahitaji ustawi wa ccm tuanze kwa kupinga kwa nguvu zetu zote huu mtindo wa babazao kuwapa vijiti watoto zao na tuanzie kwa nape kwani ndiyo anajitahidi sana kuchafua watu ambao ni selfmade politician ili wabaki wao na vizazi vyao vya nyoka tunasema noooooo way!!!
 
mmmh! mkuu unampa hongera ya nini wakati hii ni hatua ya awali sana! nafasi zenyewe kama sikosei ni NANE tu

Kuchukua tu fomu anastahili hongera,kuonakana na kupita katika mchujo mkali anastahili hongera kubwa zaidi.......

Ben hii hongera yako unamaanisha kweli?
Majibu yako hapa chini mkuu EDSON........
Great thinkers amempa hongera kupitishwa na NEC a journey start with first step! Edson wewe pia ni katika wale wanaoamini siasa za chuki? I mean zile za kwanini Zitto ana urafiki na January? kama ndio basi watu kama nyie mkipata tu madaraka............................................
 
Niliongea jana nikatukananwa kwenye hii tabia inayoanza kuchipa wa kurithishana uongozi wakati waarabu sasa unawatesa, ila sisi tumeona ndiyo dili, ukweli ni kwamba hiitabia tunayoanza sasa itakuja kulitesa taifa, huo ni ukweli
 
Na kwa aina hiyo ya wabunge tusitegemee kwamba nchi ina wakilishwa kwenye bunge la East Africa, hapo wanafuata fedha, period.
 
huo ni upotoshaji wa makusudi,walitangaza nafasi hizo na watu wamejitokeza kuchukua fomu na kuomba,kinachofuata ni mchujo wa wale wenye SIFA stahili kupitishwa bila kujali ni mtoto wa kigogo gani....hao ni wateule tu bado hawajachaguliwa,pia hata wakichaguliwa bado ni haki yao kama hakuna wenye SIFA zaidi yao.Mnataka tuwakatae ati kwa sababu ni watoto wa vigogo? basi hata ajira wasipate kwenye taasisi za serikali wala mashirika yoyote? HAPANA huo ni ufinyu wa FIKRA....Acheni TANZANIA DAIMA wafanye SIASA kwa vile ni kazi yao,Lakini Great THINKERS let us go beyond the SKY.....
 
Back
Top Bottom