Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,423
- 31,458
Kama JMK kafanya mengi ya maana kwa maana ya maana, basi Nyerere atakuwa amefanya ya maajabu. Ni kutoka ukoloni tukiwa na Pangani tu, na Kibajeti finyu aliwekeza katika umeme kuliko mwingine yoyote aliyefuata. Kibajeti finyu aliacha vyanzo ambavyo vilimsaidia JK akiwa mwanafunzi hadi kuwa Rais. JMK amewekeza wapi kwa maana ya kuwekeza. Jenereta Nyerere alinunua tuna ushahidi(mpango wa maendeleo 1963).FaizaFoxy;2274623]Kitu ambacho nadhani unashindwa kukikubali ni kuwa, Kikwete kafanya mengi ya maana kwenye suala la umeme.
Alipochukua nchi kakumbana na mambo mengi sana, na kwa kibajeti chetu finyu afanye mangapi kwa pamoja?
Akiichukua nchi alikuwa ndani ya serikali kwa miaka zaidi ya 20 kama waziri wa fedha, Nishati na Mambo ya nje, zote zikiwa wizara zenye uhusiano na nishati kama resource, policy maker au katika contract kama za IPTL.Hana excuse yoyote.Katika priorities alizokuwa nazo, hili la umeme lipo na hajalisahau, utakumbuka kwamba, alipochukua urais nchi ilikuwa kizani. Akafanya haraka haraka iletwe mitambo ya emergency, matokeo tunayajua, na kwa bahati nzuri zikanyeesha mvua nzuri sana tukawa hatuna haja hata ya kuiwasha hiyo mitambo
Matokeo hatuyajui kwasababu hatukuona umeme, ni matokeo gani mazuri yaliyotokana na mitambo ya emergency?
Nakumbuka wilaya ya Ulanga na Kilombero kuna ma DC walipoteza kazi kwa kuficha ukweli wa njaa katika wilaya zao, Lowassa atakuwa shahidi wangu. Kwa nchi kama Tanzania kujua watu waliokufa kwa njaa sio jambo la kuaminika hata kidogo. Hanang walipelekewa chakula wakati fulani baada ya BBC kutangaza, sasa serikali hiyo itawezaje kusema hakufa mtu tukaamini.Ukame ule alioukuta Kikwete uliambatana na njaa kali sana, Kikwete akasema hafi mtu hapa. Akafanya kila njia na kweli hakufa mtu kwa njaa ile. Bahati nzuri sana mvua ile iliyojaza mabwawa ya hifadhi kwa ajili ya umeme, ilitusaidia kwa miaka minne mfululizo, na kina cha maji kilikuwa kizuri tu, sasa fedha inayohitajika sana sehemu zingine, ikaanza kutumika huko, kwenye mashule, mabarabara, ma university na mitambo ya umeme iliyokuwepo Ubungo ilionekana kuwa itatosha kabisa kama kuna tatizo
Njaa inaweza kuua kwa njia mbili. 1) Haraka kwa kukosa mlo 2) kwa matokeo ya muda mrefu. Kukiwa na njaa watoto wataathirika kwa marasmus na Kwashiokor, ikitokea maradhi kama surua au kuhara basi huharakisha vifo vyao. Ingawa atakuwa amefariki kwa surua, lakini kitaalamu inasemwa amefariki kwa complication of measles as a results of severe malnutrition, hapa unaona njaa inavyoua in long term. Kusema hakufa mtu you need more than just saying it.
Wawekezaji wa kichina pale kariakoo hawawezi kuleta ongezeko lolote la maana katika nishati. Wawekezeji wote wakubwa katika sekta ya madini inayotumia umeme mwingi waliingia wakati wa Mkapa. Kama yupo mwekezaji waliyeletwa na JMK tufahamishwe.Kilichotokea baada ya hapo ni wimbi la wawekezaji, wimbi la matumizi ya umeme yasio ya kawaida na umeme ukawa unahitajika na unaongezeka kwa 14% kila mwaka. Kikwete akaagiza mitambo kama mahitaji ya maongezeko, ghafla tumekumbwa na ukame, mitambo ambayo iliagizwa ku cover ongezeko la kawaida la kila mwaka ndio inatumika kujaziliz umeme ambao haufuliwi kwa ajili ya kupungua vina vya maji kwenye mabwawa. Hapo jamani ni nani wa kumlaumu? ingekuwa hajafanya kweli, mimi ningekuwa wa kwanza kumlaumu.
Ni JMK alikuwa waziri wa mambo ya nje kwa miaka 10, ongezeko la wawekezaji alipaswa alijue kwasababu mikataba yote alishiriki 100%. Kama angechanganya na maarifa ya uwaziri wa nishati hili lisingekuwa tatizo, kusema ukame ni kisingizio cha kushindwa kutumia maarifa na ulaghai wa mikataba ya nishati ambayo yote ina mikono yake. Lakini JMK anajua tatizo la mabwawa ya umeme au ana hisi? ni huyu alituambia tatizo ni mtera kujaa matope, na wafugaji bonde la usangu, sasa ukame je anajua tatizo hasa!!
Haya yote yana play book, hakuna mradi hata mmoja kati ya uliyotaja unaotokana na ubunifu wa serikali ya JMK, in fact alipaswa kufanya haya akiwa waziri wa fedha, nishati na mambo ya nje.Kumbukeni kuna sababu ambazo zinakuwa nje ya uwezo wa yeyote awaye, lakini kizuri ni kwamba Kikweye hata kwa hilo hajasema hapana hapa ndio mwisho, kawekeza kwenye mkaa wa mawe, kawekeza kwenye upepo na sasa anahuisha umeme wa steigler.
Amejenga vyanzo vingapi katika national level. Amewekeza 50MW wapi? kama ni ununuzi wa jenereta je hiyo ni renewable energy source and is it sustainable. Hebu tuambie ziko wapi ambazo tutasema hizi ni za JMK hakutumia ubunifu wa mtu mwingine.Data zinaonesha average yake ya kuwekeza kwenye umeme kwa mwaka ni way above wote waliomtangulia. Wakati wenzake waliwekeza wastani wa 7.5MW kwa mwaka yeye anawekeza 50MW kwa mwaka, hilo nii kubwa sana na kasema itaongezeka kufikia uwiano wa 200MW kwa mwaka kabla ya kumaliza muda wake. Its a big achievement uki compare na wote waliopita. Na vilevile akabadilisha sheria ya monopoly kwenye umeme ili wafuaji binafi waweze kuwekeza na matokeo tunayaona