Maji ni huduma ambayo Serikali inafeli vibaya mno, uhaba na mgao karibu kila mkoa japo mabilioni yanatumika. Rais Samia anashindwa wapi?

Wana JF mnaoishi sehemu zenye uhaba wa maji, hebu tuelezeni basi sehemu zenu ni zipi na hampati maji kkwa ukawaida
Mimi mpaka nimeamua kuita wachimbaji wa Borehole drilling na nimepata maji matamu bila chumvi.

Sasa hivi natengeneza swimming pool ili niwe najipoza huku nikiburudika na Bia bardiii.

Maisha mafupi sana haya.

Na huenda nikafungua kiwanda cha maji siku za usoni nataka kuvuta mkopo wa Kiisilamu wenye riba nafuu iliyofichwa fichwa.
 
Mimi mpaka nimeamua kuita wachimbaji wa Borehole drilling na nimepata maji matamu bila chumvi.

Sasa hivi natengeneza sweeming pool ili niwe najipoza huku nikiburudika na Bia bardiii.

Mkuu umeula! Nimefikiria sana juu ya hilo. Hivi gharama zikoje, na wanapima kabla ya kuchimba kama maji yako wapi na watachimba kina gani?
 
1.8 mills hiyo gharama kina ni mita hamsini (inategemea bed rock ya eneo uliloko)
Imewachukua siku mbili kupima ili kupata maji yasiyo na chumvi.

Nimeweka tenki la 1000 ltrs na linajaaa mpaka yanamwagika.

Tanzania tuna rasilimali nyingi sana ila know how to ndio inahitajika.
 
hii ni ghrama ya jumla, yaani kupima point ya kuchimba, kuchimba, casing, piping na sealing? Upo Dar?
 
Mkuu, unajua ni kiasi gani cha maji yanakwenda kuishia baharini na kwenye maziwa? Na pia, kuwa na miradi ya Hydo hakuzuii kusambaza maji kwa matumizi, kwa kuwa bado unaweza kutumia maji downstream ya HEP. Hydo hazi-consume maji, zinayapitisha tu kwenye turbines na infact yanapotoka kwenye turbine yanakuwa na pressure kubwa tu. Kwa hiyo kitu kimoja hii serikali ingekuwa ni ya mainjinia wangefanya kila mradi wa HEP unakuwa chanzo cha kusambaza maji, downstream the turbines

Angalia picha hii ya Mtera

Ikiwa kina cha maji kinapungua unafikiri nini kitasukuma hizo turbines ili umeme uzalishwe? Hapo nilikuwa nazungumzia wale wanaolalamika kuhusu umeme.

Mito mingi na mabwawa maji yamepungua kama sio kukauka kabisa kutokana na uhaba wa mvua, mwisho wa siku lazima kuwe na migawo ya maji
 
Mkuu kuchukua maji downstream ya turbines hakupunguzi kina cha maji ya HEP
 
Mimi mpaka nimeamua kuita wachimbaji wa Borehole drilling na nimepata maji matamu bila chumvi.

Sasa hivi natengeneza sweeming pool ili niwe najipoza huku nikiburudika na Bia bardiii.

Maisha mafupi sana haya.

Na huenda nikafungua kiwanda cha maji siku za usoni nataka kuvuta mkopo wa Kiisilamu wenye riba nafuu iliyofichwa fichwa.
Unaishi wapi mkuu? Nakuuliza hivi kwa sababu maeneo mengine ukichimba kisima maji yana chumvi kali sana hata wanyama wenyewe hawawezi kunywa asee
 
Unaishi wapi mkuu? Nakuuliza hivi kwa sababu maeneo mengine ukichimba kisima maji yana chumvi kali sana hata wanyama wenyewr hawaezi kunywa asee
Tafuta professionals kwenye Borehole drilling business wengi ni wababaishaji kabla ya kuanza kazi muulize maswali ya kitaalamu kama anajua vitu kama Bedrock na kama anavipimo vya kisasa vya kujua maji yasiyo na chumvi yako umbali gani.
 
Mkuu kuchukua maji downstream ya turbines hakupunguzi kina cha maji ya HEP
Nazungumzia uzalishaji wa umeme mkuu sizungumzii kuchukua maji downstream (outflow)

Nazungumzia ikiwa kwenye intake pale kwenye reservoir maji yamepungua sana

Tuseme mfano mto unaoleta maji kwenye hydropower plant kina kimepungua sana au kukauka turbines hazitaweza kuzungushwa kuzalisha umeme
 
Tafuta professionals kwenye Borehole drilling business wengi ni wababaishaji kabla ya kuanza kazi muulize maswali ya kitaalamu kama anajua vitu kama Bedrock na kama anavipimo vya kisasa vya kujua maji yasiyo na chumvi yako umbali gani.
Sawa asante kwa ufafanuzi
 
Tatizo la maji ni shida ya muda mrefu. Serikali haijaona umuhimu wa kupambana na hii hali kwa sababu ikifika uchaguzi wale wale ambao hawapati maji wanawachagua viongozi wale wale walioshindwa kuwapatia maji licha ya ahadi lukuki!
Umuhimu wa katiba mpya unapaswa uangalie hii hali. Kuwe na kifungu cha kubadilisha mfumo wa elimu yetu ili mwananchi afundishwe jinsi ya kupambana ha hali ili aweze kuishi. Mitaala ifundishe mbinu zote za uvunaji maji yawe ya mvua, ardhini, maziwa au ya baharini! Tukikaa kusubiri serikali twafa!
 
Nazungumzia uzalishaji wa umeme mkuu sizungumzii kuchukua maji downstream (outflow)

Nazungumzia ikiwa kwenye intake pale kwenye reservoir maji yamepungua sana

Tuseme mfano mto unaoleta maji kwenye hydropower plant kina kimepungua sana au kukauka turbines hazitaweza kuzungushwa kuzalisha umeme
Mkuu huwa kuna hesabu zinafanyika, sio wanaweka tu. Na kumbuka si wakati wote kunakuwa na matatizo ya level ya maji kwenye dams. Na pia sio HEP zote ni reservoir, kuna zile tunaita run of the river ambazo hazihitaji kina cha maji
 
Tanzania tunazo zipi mkuu?
 
Tanzania tunazo zipi mkuu?
Zote mbili

1665140058856.png
 
Kwenye makazi yao ambayo ni maeneo tengefu yani maeneo ya watu wazito huwa huduma yoyote haikosekani so sidhani kama watakuelewa
 
Back
Top Bottom