Maji hakuna, kufurahisha Mzungu/Globalist!

Kijakazi

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
6,409
8,911
Huu unaoitwa ukame ni wa kutengeneza ili kumfurahisha globalist, Tanzania haijawahi kukumbwa na uhaba wa maji kwa kiasi hiki.

Sababu za huu unaoitwa ukame ni kuendana na Mkutano wa Global Warming unaofanyika huko Misri ili Globalist apate kuwaaminisha watu kuna global warming, hata Mlima Kilimanjaro wanachoma makusudi kutesa watu, lkn hakuna ukame Tanzania, hawa watu ni pure evil!
 
Mlete mzungu, mlete mzungu🐒

images - 2022-11-02T162951.646.jpeg
 
Huo ukame unaotajwa, tuutegemee kutokea siku zijazo lakini hadi muda huu bado hali ni ya kawaida tu. Tathmini yangu ni kisima changu cha mita 15 kilicho chimbwa kwa mikono... Bado hakijapungua ujazo wake kufikia ukame wa mwaka 2009/10.
Tutegemee mvua za vuli zinazoweza kuleta madhara kwenye baadhi ya mikoa.
 
Unamaanisha wazee wa agenda 2030? hawa wapo kwenye utekelezaji wa ule mpango wa kujidhihirisha kwa mpinga Kristo na kupandikiza ile namba.
 
Si useme tu wao ndio wanaozuia mvua na kuongeza kiasi cha joto dunian kupitia mitambo yao ya kishenzi.

Ukame, uhaba wa mvua, mafuriko, ugaidi, vita, njaa, movement za wakimbizi, mitifuano ya kisiasa haya yote , hayajawai kutokea kwa bahati mbaya

Kama viongozi wetu wangekuwa wema sana wangekuwa wanaweka wazi Mikataba wanayosaini na hayo wanayoyajadiri mikutano ya UN.

Hata kupanda kwa hali ya maisha si jambo la bahati mbaya, bali washenzi wachache wanaoamua mustakabari wa maisha uende vipi ili waweze kuwacontrol watakavyo.

Kama siku tukiyajuwa yale tusiyoyajua kuhusu nchi zetu, i swear wengi wetu tutawakana viongozi wetu hata utaifa wetu,

Sir100 mpaka anamaliza uongoz nchi itakuwa imeharibika vya kutosha, wachache wanafaidi na wengi wanaumia.

Siku zote ukiwa upande wa kweli lazima uchukiwe.
 
Hakuna cha globalist wama mamake na nini,hapa mchawi mkubwa ni CCM tu tena na bado kama hatutasema ifike mahali hiki chama kongwe kipumzishwe tutazungukia hpohapo mpaka yesu arudi hao jamaa hawanaga maarifa wala maono ya miaka hata 10 mbele wao huwaza namna ya kudhibiti akili kubwa zenye viashiria vya kuja kuwafunika baadae,juzi walisema umeme tutauza nje ya nchi leo hatuna hata wa kuvhomelea
 
Ni kama huwa husomi au hufanyi utafiti au umri wa akili Yako ni mdogo au hushughulishi ubongo wako! Kusema kwamba Tanzania haijawahi kukumbwa na ukame unakua unaonesha hali hiyo ya uvivu wa kufikiri,
Tanzania imewahi kukumbwa n LA NINA pamoja na El NINO kwa vipindi tofauti tofauti rejea ukame mkubwa uliokumba nchi mwishoni mwa miaka ya 70 na mwanzoni mwa miaka ya 80 lakini pia hali mbaya ya ukame katikatikati ya miaka ya 90.
Na mwanzoni mwa miaka ya 2000.
Majio sio Fedha ili useme yanafichwa ndani au mfukoni Ili kuihujumu nchi!

Sisi sote ni mashahidi kwamba mvua zimechelewa kunyesha na hata kama zikinyesha ni kwa kiwango kidogo!
Tatizo ni Nini?
1. Kuongezeka kwa idadi ya watu na shughuli za kibinadamu
- Shughuli za kilimo na ufugajI Ili kukidhi mahitaji ya binadamu ya kila siku zimechangia watu kuvamia au kusogelea vyannzo vya maji kama mito nk
-Shughuli za kibinadamu zimechangia ukataji wa miti Hovyo kw ajili ya kupata maeneo ya kilimo na ufugaji na kuendelea kuifanya nchi jangwa
-Umaskini, wananchi wengi wa Tanzania ni maskini kiasi kwamba hawawezi kumudu kupata nishati rafiki kwa mazingira kama umeme na gesi kwa ajili ya kupikia Hivyo kumpeleka uvunaji wa misitu kwa ajili ya Kuni na mkaa huku kukiwa hakuna mpango wa kupanda miti mingine!
2. Rushwa na tamaa ya kujilimbikizia Mali!
Wapo watu wanaotumia ushawishi wao wa kifedha na kimamlaka kutumia rasilimali za maji kwa manufaa Yao binafsi ikiwemo kuchepusha maji ya mito kwa ajili ya kufanya shughuli za kilimo na ufugaji wa samaki! Jambo hili hufanya maji kupungua au kukosekana kabisa katika lower streams!
3. Viongozi wasiokuwa na Dira Wala maono.
Swala la ukosefu au uhaba wa maji au ukame sio jipya katika nchi hii, lakini tmekosa viongozi wanaotazama mbali jinsi ya namna Bora ya kukabiliana na changamoto hii kwa kuweka mipango ya muda mfupi na muda mrefu pamoja na mipango ya kidharura mathalani uchimbaji wa mabwawa katika maeneo yasiyo na mito au vyanzo vya uhakika vya maji Ili kuvuna maji ya mvua na kuyatumia katika kipindi kama hiki!
Hakuna approach yoyote katika suala Zima la kutunza mazingira na kucontrol shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo na ufugaji pamoja na utunzaji wa vyanzo vya maji!
4.Global Climatic Change (Mabadiliko ya tabia ya nchi)
Kama u mfuatikiaji mzuri wa mambo, Dunia inakabiliwa na tatizo la mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na athari ambatano Mojawapo ikiwa ni upungufu wa mvua za wastani kwa mwaka au ukame kabisa katika maeneo ambayo awali yalikua yakipata mvua za kutosha kwa mwaka, lakini mvua zisizo za kawaida ambazo huambatana na mafuriko na atahri zake!

_kwa hali tuliyo nayo serikali inapaswa kuwajibika badala ya kutoa visingizio kwani iliapswa kuchukua hatua za muda mrefu Ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa maji Kama tunahokutana nayo, miradi ya maji inayoimbiwa kila siku mapambio na kumtaja Rais imekua Chaka la upigaji pesa kwani mingi maji hutoka tu siku ya uzinduzi na mbwembwe nyingi pamoja na wakati wa kampeni au ziara ya kiongozi!
 
Inawezekana kuna maeneo hakuna ukame kabisa,lakini yapo maeneo kuna ukame wa kutisha. Tembelea maeneo ya Shinyanga haswa kishapu ujionee mwenyewe, hali ni mbaya sana, pamoja na uwepo wa maji ya lake Victoria kwenye maeneo machache na yenyewe siyo ya uhakika na ni aghali sana. Tembelea minada ya mifugo utawaonea huruma wafugaji. Kiuhalisia upo ukame mkubwa.
 
Back
Top Bottom