Intelligence Justice
JF-Expert Member
- Oct 23, 2020
- 3,068
- 3,515
Wana jukwaa
Kama kichwa cha mada kinavyojitanabahisha hapo juu, wananchi Dar wanahangaika kupata maji mapaka wanathubutu kuchimba visima vya kienyeji katikati ya vijito vilivyojaa uchafu na vinyesi huku DAWASA hawajali chochote wakati mto Ruvu una maji ya kutosha kusambaza.
Dar inategemewa chanzo cha maji yasiyo na chumvi kutoka mto Ruvu na ina mashine zake Ruvu juu na Ruvu chini lakini cha kushangaza inakaribia wiki tatu sasa maji yamekuwa ya shida sana huku wakiuziwa na wajanja usiku wa manane shilingi 1,000 hadi 2,000 kwa dumu moja la ujazo wa lita 20.
Wananchi wanatoa rai kwa mamlaka ya maji DAWASA pamoja na wizara ya maji kushughulika na kero hii mapema kabla majnga hayajaanza kuibuka kifamilia na kijamii.
Ilidaiwa kipindi fulani kuna chanzo kingine kimeanzishwa huko Mkuranga, Pwani lakini jitihada hizo hazionekani na na viwanda vya kutengeneza maji kila kukicha wanapandisha bei mfano huko Kigamboni na Mapinga bei za maji ni juu kuliko hata maji yanayotengezwa Bonite bottlers Kilimanjaro!
Mchango wa maoni yenu wadau ni mhimu kwa wakati sahihi.