Siwezi kuwashangaa saaaana katika hili maana ni uhuru wenu kuongea, kuhusu hili la Muhongo, mimi ninasimama kutamka hadharani kua ilivyoripotiwa na hilo gazeti la udaku si kweli, Muhongo hakukataa kusafiri na hiyo economy class, na alisafiri siku hiyo hiyo.
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni kwa hili Muhongo hana kosa hata kidogo, hivi kwa akili yako kuna umuhimu wa kupitia dubai ulale huko wakati hapo Algeria ni karibu tu, tena tunapaswa kumpongeza kwa kuonesha uzalendo wake maana hakutaka kuharibu fedha ya serikali kwa kumgharamikia malazi ya hapo dubai ambapo atakuwa kama mtalii tu na hivyo kugoma na baadae alipatiwa ndege ambayo ilimuwezesha kufika huko alipokua akienda siku hiyo hiyo, yule ni msomi bhana sio kama.....
ha ha ha ha ha! msomi asiyejua mitaji ya biashara inapatikanaje?