Majanga: Waziri Muhongo Asusia Ndege, Kisa, Kakosa Daraja La Kwanza

WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amegoma kusafiri na Watanzania wenzake kwenda nchini Algeria kwa daraja la kawaida baada ya kukosa daraja la kwanza, hivyo kuahirisha safari yake kwa siku moja, Tanzania Daima limebaini.

Profesa Muhongo ambaye amekuwa akionyesha dharau kwa Watanzania mara kadhaa, aligoma kusafiri katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam Jumapili ya Novemba 24, 2013, saa 10.45 akiwa na wenzake tisa kwenda kwenye safari ya kikazi nchini Algeria alikoenda baadaye.Moja ya kauli ya dharau iliyotolewa hivi karibuni na Waziri Muhongo ni pale aliposema wafanyabiashara Watanzania wana uwezo wa kuwekeza kwenye soda na juisi badala ya gesi na pia aliwahi kuwashambulia viongozi wa dini kwa kuwaita waongo.

Uchunguzi wa Tanzania Daima uliofanyika kwa siku kadhaa sasa, umethibitisha kwamba Muhongo alikuwa aondoke na ndege ya shirika la ndege la Emirates namba EK 726 kutoka Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere kupitia Dubai kwenda Algeria akiwa na tiketi ya daraja la kawaida bila kujua kabla ya kufika uwanjani hapo na kisha kuanza kumfokea kila aliyekuwa anamsemesha.

“Tiketi yake na wenzake kumi ilikuwa ni Economy Class (Daraja la Kawaida), lakini akakataa akitaka asafiri kwa First Class (Daraja la Kwanza). Alibembelezwa na wenzake na wafanyakazi wa Emirates na wale wa Uwanja wa Ndege lakini akagoma huku akifoka na wenzake wakataka kuahirisha safari.

Ikawa tena ni sisi kuwaomba wasafiri ili Bwana Mkubwa (Muhongo) atafutiwe nafasi kwa daraja analotaka.
“Walimbembeleza wakamwambia kwa kutumia ‘millage’ ya safari zake watambadilishia akiwa ndani ya ndege na kumuweka daraja la kwanza lakini alionekana ameshakuwa mkali na hakuwa anamsikiliza yeyote.“Baadaye tulifanikiwa kuwashawishi wenzake kuendelea na safari na yeye sijui aliondoka na ndege gani tena maana wakubwa wetu wana mambo sana,” anasema ofisa mmoja uwanjani hapo.

Taarifa za awali kuhusu sakata hili, ziliripotiwa siku hiyo katika mtandao wa jamiiforums.com zikieleza kwamba kitendo cha Waziri Muhongo cha kususia safari hiyo, kiliwakera baadhi ya wasafiri wakiwamo raia wa kigeni ambao walishangazwa na hatua hiyo ya kiongozi wa nchi maskini inayotegemea misaada kulazimisha kusafiri kwa daraja la kwanza, daraja ambalo viongozi wa mataifa makubwa hawaruhusiwi kusafiri bila sababu maalumu.

Taarifa hiyo kwenye mtandao wa JamiiForums. Com iliripotiwa hivi: “Kweli viongozi wa nchi hii wanatia aibu, wakati mawaziri wa Uingereza wanakataa First Class, hapa kwetu kimetokea kioja. Waziri wenu wa Nishati na Madini (Muhongo) ambaye anazidi kutulaza na joto na giza leo amewaacha hoi Watanzania pale alipofika mpaka Airport na akiwa anaboard akakuta anawekwa sehemu ya abiria wa daraja la kati, baada ya kuambiwa hayuko First Class akagoma na kutoka nje ya mlango. Wakati hayo yakiendelea kumbe ana wenzake zaidi ya tisa wako economy na wawili Bussiness Class, ghafla nao wakaanza kushuka.

“Hapo ndipo hekima za mmoja wa wahusika wa Airline (Emirates) akawaomba hao waende ili yeye akabadilishe aje kesho yake.” “Jamani kweli First Class inakushushia aibu hivi Profesa na bado unasema maisha magumu Tanzania!? Inaonekana zile buti za bora ulizivalia ukiwa form V na haya ndio madhara yake, mnapewa vyeo wakati maisha yalishawapiga; mnatafuta muafaka na Yesu mkiwa madarakani,” anaeleza mtu aliyewasilisha mada husika akijulikana kwa jina la Basiasi.

Basiasi alihoji sababu ya abiria wenzake ambao nao walikuwa wakisafiri kikazi kutaka kushuka na kusababisha hasara kwa serikali au wafadhili waliokata tiketi hizo. Kwa utaratibu wa kawaida abiria anayeahirisha safari baada ya kuwa ameshaingia ndani ya eneo la kusafiria (boarding) anaweza kupoteza kabisa tiketi au kulipishwa fedha nyingi zinazoweza kuwa sawa na kununua tiketi mpya.

“Hebu kuweni wastaarabu, sasa wale watu tisa walitaka kuwashusha kwa nini na kama wamekwenda, mlishindwa kuwaambia wabaki mpaka mkaanza kuleta aibu uwanjani? Inaonekena ndege mmeanza kupanda uzeeni; najiuliza kivipi unaletewa tiketi hata kama na ‘travel agency’ halafu unashindwa kuuliza au kukagua mpaka unaenda uwanjani na unapewa ‘boarding pass’ bado unashindwa kukagua ipi ‘bussiness class’ na ipi ‘first class’!” anahoji Basiasi. Abiria mmoja aliyenukuliwa na Jamiiforums alisema kwa waziri wa nchi kama Uingereza anatakiwa kutoa maelezo ya sababu za kusafiri na daraja la kwanza (first class) ikiwa atalazimika kufanya hivyo, vingine viongozi husafiri kwa madaraja ya kawaida.

Wakati Waziri Muhongo akisusia ndege kwa kukosa nafasi ya kusafiri na daraja la kwanza, baadhi ya mawaziri wanaofanya ziara mikoani na kusafiri kwa ndege, hulazimika kuyaagiza mashangingi yao kutoka Dar es Salaam hadi katika mikoa wanayokwenda kufanya ziara hizo hata kama yatatumika kwa siku moja.

Muhongo ni janga la taifa...Hata kwenye msiba wa baba yake mzazi alikuwa halali msibani, yeye alikuwa anachapa usingizi Musoma Hotel kwa kipindi hicho ndo ilikuwa hoteli kubwa na ya kisasa ya kitalii pale Musoma (five star hotel) iliyokuwa ikimilikiwa na Shirika la Reli... Ni kawaida yake kujiona ni matawi ya juu, sasa kama kwa msiba wa baba yako unashindwa kulala msibani ambapo ni nyumbani kwenu, wewe unatanua na mkeo mzungu hotelini si hiyo ni laana!
 
Watanzania acheni wivu wa kike na mjadili hoja baada ya kupata upande wa pili.

MUHONGO alikata ndege baada ya kuambiwa inapita DUBAI na wanalala DUBAI.
KWA HALI YA DUNIA HII KWENDA ALGERIA MPKA ULALE NJIANI???
WATU TUNAENDA CHINA MAREKANI HATULALI NJIANI IJE KUA ALGERIA?\
MUHONGO ALISEMA HAWEZI LALA DUBAI KWA SAFARI YA ALGERA
AKABADILI NDEGE AKAPANDA KLM AKAFIKA ALGERIA SIKU HIYO HIYO NA ALIPANDA Economy Class
KWA WALE WALIOWAHI KUPITIA DUBAI WANAWEZA KUSEMA. HASA KIPINDI HUKI CHA SIKUU DUBAI NI SHIDA SANA SEHEMU YA KULALA NI SHIDA. SASA MLITAKA MUHONGO AWAFRAHISHE AKALALE DUBAI? ACHENI UJINGA
wambeke umbeya huu umesababishwa na tatizo moja kuu. Hivi Mh hakuangalia tiketi yake kabla ya kwenda airport? Au hao wanaoshughulika kuandaa safari za Mh hawakujua hili wakamtahadharisha mapema kabla hajaenda airport. Kwa mujibu wa taarifa hii alisha check in. Hii maana yake ni kuwa kubadilisha kwa safari hiyo kulikuwa na gharama kubwa. Was this necessary?
 
Yaani mleta uzi alipolitaja tu gazeti fulani nikajua kusudi ya habari hiyo, hata kama ni kweli prof.muhongo alifanya hivyo kama mleta habari alivyoandika lakini bado utendaji kazi wa hilo unatia shaka, mbona viongozi wengi wa cdm wanaotuhumiwa kwa kashfa mbalimbali huwa hawaandikwi? mbona kashfa anazotuhumiwa slaa hazichapwi kwenye gazeti hilo? Hilo gazeti limeanza kuwa la udaku!!
 
Alijisahau kidogo kwamba ndege ikianguka au kupata shida angani hakuna cha first class au economy class wote huwa wanakufa sawa,sasa angeshauriwa on those lines am sure angejitambua,au vipi akodishe hustler mbona ziko nyingi sana kama anaona atachafuka akikaa na wavuja jasho.

Kuanguka kwenye ndege kimahesabu ni rare sana(probabilitywise)kuliko kwenye usafiri wa gari au bodaboda..Samahani..ni taarifa tu..tuendelee na ya Muhongo.
 
Hili jamaa lishamba kumbe!? Prof unafanya mambo ya kise... Tatizo miprof ya kibongo inafikiri kwa kutumia pumb.u badala ya ubongo. Limeniboreje?
 
Haya yote yanasababishwa na Watanzania wenyewe kwa kukichagua chama kile kile chenye viongozi wenye tabia zilezile na mfumo mmbovu wa uendeshwaji wa chama kile kile ,naam Watanzania vumilieni maana mnakivuna kile kile mlikipanda wakati wa uchaguzi.
 
Kuanguka kwenye ndege kimahesabu ni rare sana(probabilitywise)kuliko kwenye usafiri wa gari au bodaboda..Samahani..ni taarifa tu..tuendelee na ya Muhongo.

Kwa hiyo ndege huwa hazianguki mkuu ?
 
Yaani mleta uzi alipolitaja tu gazeti fulani nikajua kusudi ya habari hiyo, hata kama ni kweli prof.muhongo alifanya hivyo kama mleta habari alivyoandika lakini bado utendaji kazi wa hilo unatia shaka, mbona viongozi wengi wa cdm wanaotuhumiwa kwa kashfa mbalimbali huwa hawaandikwi? mbona kashfa anazotuhumiwa slaa hazichapwi kwenye gazeti hilo? Hilo gazeti limeanza kuwa la udaku!!

Wala hulazimishwi kuamini habari za gazeti la Tanzania Daima ,tunamzungumzia huyu waziri Muhongo kwa tukio ambalo alishalitenda tayari ya Dk. Slaa yanaingiaje huku?.Umeshasema Slaa ana tuhuma sasa tuhuma ndio ukweli?Usiendeshwe na hisia ,sote tunakilaani kitendo alichokifanya Waziri huyu kwa sababu hizi pesa anafuja hapa ni kodi zetu sisi sote bila kujali wewe ni ccm mimi ni Chadema au la!!?.
 
kweli viongozi wetu ni waajabu kweli na ukiaangalia background zao ni shida tup?? ilakilicho mtokea sadam huseni ndicho kitakacho watokea wakina profesa muhongo?
 
Watanzania acheni wivu wa kike na mjadili hoja baada ya kupata upande wa pili.

MUHONGO alikata ndege baada ya kuambiwa inapita DUBAI na wanalala DUBAI.
KWA HALI YA DUNIA HII KWENDA ALGERIA MPKA ULALE NJIANI???
WATU TUNAENDA CHINA MAREKANI HATULALI NJIANI IJE KUA ALGERIA?\
MUHONGO ALISEMA HAWEZI LALA DUBAI KWA SAFARI YA ALGERA

AKABADILI NDEGE AKAPANDA KLM AKAFIKA ALGERIA SIKU HIYO HIYO NA ALIPANDA Economy Class
KWA WALE WALIOWAHI KUPITIA DUBAI WANAWEZA KUSEMA. HASA KIPINDI HUKI CHA SIKUU DUBAI NI SHIDA SANA SEHEMU YA KULALA NI SHIDA. SASA MLITAKA MUHONGO AWAFRAHISHE AKALALE DUBAI? ACHENI UJINGA

Mmmh, inamaana hadi anafika airport alikuwa hajui ndege yake inapitia wapi?
Well na KLM ni Dar all the way to Amsterdam, inatoka saa 5 usiku na kufika Amsterdam Asubuhi, hiyo KLM ya kutoka Dar na kufika Algeria kwa siku hiyo hiyo aliitoa wapi.
Siku nyingine jipange kabla ya kujaribu kudanganya watu.
 
Umbea huu, watz fanyeni kazi

Tatizo sio Umbea ni mfumo wa utawala serikalini hakuna kuokoa fedha kadri iwezekanavyo!shughuli za utawala ni ghali zaidi kuliko za maendeleo!

Sasa nchi masikini Ina ruhusu first class Nchi tajiri zinazoserve pesa kutusaidia haziruhusu FC !huu weusi wetu balaa!!
 
TUMEZIDI MAJUNGU JAMANI! UNAFIKI WA CDM MSIUHAMISHIE CCM. MSITOE HABARI KABLA YA KUIBALANCE, FANYENI KAZI ACHENI UVIVU WA KUFIKIRI VISOKOLOKWINYO.
Watanzania acheni wivu wa kike na mjadili hoja baada ya kupata upande wa pili.

MUHONGO alikata ndege baada ya kuambiwa inapita DUBAI na wanalala DUBAI.
KWA HALI YA DUNIA HII KWENDA ALGERIA MPKA ULALE NJIANI???
WATU TUNAENDA CHINA MAREKANI HATULALI NJIANI IJE KUA ALGERIA?\
MUHONGO ALISEMA HAWEZI LALA DUBAI KWA SAFARI YA ALGERA

AKABADILI NDEGE AKAPANDA KLM AKAFIKA ALGERIA SIKU HIYO HIYO NA ALIPANDA Economy Class
KWA WALE WALIOWAHI KUPITIA DUBAI WANAWEZA KUSEMA. HASA KIPINDI HUKI CHA SIKUU DUBAI NI SHIDA SANA SEHEMU YA KULALA NI SHIDA. SASA MLITAKA MUHONGO AWAFRAHISHE AKALALE DUBAI? ACHENI UJINGA

MUHONGO alikata ndege baada ya kuambiwa inapita DUBAI na wanalala DUBAI.
KWA HALI YA DUNIA HII KWENDA ALGERIA MPKA ULALE NJIANI???
WATU TUNAENDA CHINA MAREKANI HATULALI NJIANI IJE KUA ALGERIA?\
MUHONGO ALISEMA HAWEZI LALA DUBAI KWA SAFARI YA ALGERA

AKABADILI NDEGE AKAPANDA KLM AKAFIKA ALGERIA SIKU HIYO HIYO NA ALIPANDA Economy Class
KWA WALE WALIOWAHI KUPITIA DUBAI WANAWEZA KUSEMA. HASA KIPINDI HUKI CHA SIKUU DUBAI NI SHIDA SANA SEHEMU YA KULALA NI SHIDA. SASA MLITAKA MUHONGO AWAFRAHISHE AKALALE DUBAI? ACHENI UJINGA[/QUOTE]
 
Watanzania acheni wivu wa kike na mjadili hoja baada ya kupata upande wa pili.

MUHONGO alikata ndege baada ya kuambiwa inapita DUBAI na wanalala DUBAI.
KWA HALI YA DUNIA HII KWENDA ALGERIA MPKA ULALE NJIANI???
WATU TUNAENDA CHINA MAREKANI HATULALI NJIANI IJE KUA ALGERIA?\
MUHONGO ALISEMA HAWEZI LALA DUBAI KWA SAFARI YA ALGERA

AKABADILI NDEGE AKAPANDA KLM AKAFIKA ALGERIA SIKU HIYO HIYO NA ALIPANDA Economy Class
KWA WALE WALIOWAHI KUPITIA DUBAI WANAWEZA KUSEMA. HASA KIPINDI HUKI CHA SIKUU DUBAI NI SHIDA SANA SEHEMU YA KULALA NI SHIDA. SASA MLITAKA MUHONGO AWAFRAHISHE AKALALE DUBAI? ACHENI UJINGA

Wivu wa kike wakati sisi ndio walipa kodi? Are you serious? Yaani Prof. mzima anathubutu kusema hakutaarifiwa kuwa Emirates itapita Dubai? Au hakujua kama kuna kulala Dubai? Weka ushahidi hapa mabadiliko hayo waliyafanya wakati wa ku-board, hali ambayo ingepelekea Emirates kulipa gharama za kubadilisha tiketi pamoja na usumbufu. Na ni nani alilipa gharama za kubadilisha/kununua tiketi mpya? Kumbuka, pesa anayotumia Waziri kusafiri na kubadili tiketi hovyo ni ya walipa kodi wa nchi hii. Kama wewe ni mlipa kodi utaelewa nachokisema. Hawa mawaziri hujisahau kuwa pesa wanazotumia tunakatwa kwenye mishahara (a brutal 30%) na maeneo mengine. They are insensitive to this bare fact. Hii ni pamoja na wewe kwa kuwa watu wakihoji matumizi unasema ni wivu wa kike.

Je, wewe ni msemaji wa Muhongo? Na nini faida ya ziara hiyo kwa nchi?
 
Je umemuhoji Waziri kusikia analipi la kusema????naona habari hii ni ya upande mmoja tu tunaomba umuhoji waziri tujue analipi la kusema
 
Mmm hii kali anyway mimi namsifu Wasira kwani siku ya Jpili natoka Mwanza baba wa watu alikaa kwenye zile siti za mbele pembeni wala hakutaka kumsumbua mtu pamoja na uwaziri wake .Big up Wasira mfundishe mwenzio ajishushe kidogo tu asinge kufa au kukonda wote tu binadam

Tatizo ndege zote za Mwanza - Dar hazina first class baada ya Boeing za Precision air na ATCL kuchukuliwa na wenyewe otherwise hata yeye angejitupa first class
 
Back
Top Bottom