Maisha ya ndoa

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Mar 10, 2022
17,796
32,151
Hellow

Maisha ya ndoa yana changamoto nyingi sana japo kuwa kuna wakati matatizo yanasababishwa na pande zote mbili

Kwa upande wa mwanaume vitu vinavyo pelekea wao kuleta migogoro kwenye ndo ni mwanaume kutokana a jamii ilivyo mshape na kuonekana kuwa ndio final say au mtoaji maamuzi kwenye familia na pia ni kiongozi wa familia kuna muda mwanaume anakosea au mkewe anaweza kuona kuwa hapa mumewe anaingia chaka anaona madhara mbeleni anapojaribu kutoa ushauri na mwanaume anachukulia ushauri ule nikama amedharuliwa kuwa hana akili anakuwa mkali sana na ndipo tatizo linazaliwa.

Mwanamke anaona yeye hana humuhimu kwenye kufanya maamuzi kwa upande wa familia na matokeo yanapokuja kuwa mazuri mwanaume anavimba kichwa kuwa ameweza ila yanapokuja kuwa mabaya anakuwa mnyonge na pindi mkewe anapojaribu sasa kumfikirisha lile wazo alilo lipendekeza mwanaume huyo anaweza kuwa mkali maradufu sana.

Kwa upande wa mwanamke mwanamke jamii imemtengeneza kuwa mnyonge kwa mwanaume kwahiyo kuna muda huwa anakosea sana lakini mwanaume anapo jarib kumshiirikisha mkewe mke anajiona aanaonewa kwasababu yeye mwanamke na kuamua kwenda kusema nje ya ndoa kuwa ananyanyaswa na mumewe.

Lakini pia mwanamke yeye ameandaliwa kuwa mlezi wa familia kwahiyo inapokuja swala la malezi ya watoto na familia kwa ujumla inapoonekana kuwa mtoto amekengeuka lawama zinaenda kwakwe na baba kujitoa kwe ye janga ilo ila ukweli ni kwamba jukumua la malezi kwa watoto no la wawili mke na mume kuwashape watoto wao vile wao wanatka nakutengeneza rules ambazo ni relevant kwenye malezi ya watoto.

Mwisho hakuna njia sahihi ya kutumia ili ndoa yako iwe na amani ilaamfanye mkeo au mumeo wale rafiki yako maisha ya ndoa utayafurahia ugali kwenye ndoa hausaidi chochote.
 
Atumie akili
Shida mkuu inanzia hapo kwa upande wako unajiona uko sawa ndio maana kila mtu tunatofautiana kwenye mtazamo fikra na kila kitu so kwa mtazamo wako au experience yako ya ndoa ni tofauti na mwingine kwako unaweza ukaona upo sawa ila ukijaa kuleta changamoto yako kila mtu ataichambua kwa uelewa wake na experience yake
 
Ndoa ni photocopy jinsi kila mmoja alivyomuona baba na mama yake walivyoishi,so usioe bila kuchunguza asili yao.
 
Shida mkuu inanzia hapo kwa upande wako unajiona uko sawa ndio maana kila mtu tunatofautiana kwenye mtazamo fikra na kila kitu so kwa mtazamo wako au experience yako ya ndoa ni tofauti na mwingine kwako unaweza ukaona upo sawa ila ukijaa kuleta changamoto yako kila mtu ataichambua kwa uelewa wake na experience yake
Tuitimishe kwa kusema.... kijana hujaoa huwezi kuzungumzia mambo ya ndoa basi mtu mwenye akili timamu hawezi akakuelewa,wewe ongelea issue za mabachela utaeleweka vizuri sana,.
 
Tuitimishe kwa kusema.... kijana hujaoa huwezi kuzungumzia mambo ya ndoa basi mtu mwenye akili timamu hawezi akakuelewa,wewe ongelea issue za mabachela utaeleweka vizuri sana,.
Ninyi ndio mnao Watisha vijana wasio kwa kuwapa picha mbaya juu ya ndoa japo ndio kuna ndoa ngumu kutokana kila mtu ana tabia yake pia kwenye mahusiano kabla ya ndoa kuna kuwa na maigizo ila wapeni vijana picha nzuri juu ya ndoa
 
Back
Top Bottom