Elections 2010 Maisha ya Dr. Slaa ndani ya TBC1

Wakuu zangu sikumwelewa vizuri mzee huyo wa kwanza alipokuwa akisema urithi wa majina ya JK. Nimesikia kurithi majina ya Mchagga, hapo wenzangu mmeelewa vipi?..
 
Vaticano hivi kwanini unakuwa na mawazo potofu kiasi hicho kuwa mbunge kwa miaka 15 sio kujinufaisha mwenyewe alitumwa na wananchi wa karatu kuwatumikia hivyo hizo pesa ama mshahara wake huwasaidia wale wasiojiweza na kuleta maendeleo jimboni kwake. Nikuulize swali moja tu Mwl. Nyerere (RIP) alikaa IKULU kwa 25 hakuna kiongozi alie kaa muda mrefu hivyo IKULU hapa Tanzania na alikuja kujengewa nyumba na JWTZ baada ya kungatuka.

Je Mwl hakuweza kujenga hekalu la kuishi kwa muda wote huo hadi aje kujengewa nyumba na jeshi. Alikuwa na uwezo wa kujenga hata nyumba 100 lakini alikuwa na mapenzi ya dhati kwa wananchi aliokuwa anawatumikia hivyo hakuona busara kujilimbikizia mali alikuwa ni mwananchi wakawaida tu. Hivyo basi ni sawa na Dr. Slaa kuishi maisha ya wakaida kama wananchi wengine.

Pili usiingize mambo ya UDINI swala la Mzee wake Dr. Slaa kuishi kwenye nyumba ya matope ni maisha ya kawaida kwa wananchi wa Tanznania. Kila Mtanzania ametokea kwenye nyumba za Matope na Nyasi hii ndi asili yetu.

Nyerere alikuwa na nyumba Magomeni na Msasani. Ni "Mtanzania gani wa kawaida" alikuwa na nyumba za beach house Msasani?

Tena hiyo nyumba ya Msasani tulitapeliwa. Kwanza wakati anang'atuka na kuzunguka nchi nzima kwenda kuaga huku akipokea kila aina ya zawadi aliizuia nyumba ile kwa serikali ambapo serikali nayo ilimrudishia baada ya kuinunua kama zawadi ya kulitumikia Taifa. Hapo bado hatujazungumzia nyumba aliyojengewa na JKT. Kuna anayekumbuka nyumba ile iligharimu fedha kiasi gani?
 
Huwa sipendi kujibu hoja za kijinga lakini kwa hii acha nivunje mwiko. Kila anayelipwa milioni tano anapaswa kumjengea baba yake nyumba? na wale wasiopata hizo jee? Hoja ya msingi ni ile ya kuhakikisha vifaa vya ujenzi vinaweza kupatikana kwa bei nafuu ili kila mtanzania aweze kujijengea makazi bora kama ilani ya Chadema isemavyo.
TBC wametumia hila ambayo badala ya kumbomoa Slaa imemjenga, kwani anaposema atahakikisha waTZ wanaweza kupata makazi bora hata yeye katika familia yake yanamgusa,sio wale wanaosema zahanati zitakuwa na dawa za kutosha familia zao zinatibiwa nje hata kwa mafua tuu. Slaa ameonyesha kuwa yeye ni mpigania haki za watu wote sii familia tuu na yeye si FISADI.

Kwa hiyo tukachague viongozi wenye maradhi na ujinga kwenye familia zao kwa sababu "hata yeye katika familia yake yanamgusa". Bora hata usingevunja huo mwiko ulioudai.
 
Nimeamini mashabiki na wafuasi wengi wa Dr. Slaa na Chadema hapa jamvini hamko objective. Michango yenu dhahiri inaegemea upande wa Dr. Slaa. Kwa taarifa yenu hamumjengi mgombea wenu, hata kwa wale watu walioanza kufurahishwa na utendaji wa Dr. Slaa wameanza kuwa na mashaka juu ya aina ya watu waliomzunguka.

Naamini kama ambavyo Kikwete alivyozungukwa na genge la wahuni na mafisadi, hata Slaa pia kazungukwa na watu wa aina hiyo hiyo...tofauti tu ni kwamba hawajapata bado opportunity ya kufanya ufisadi wao.

Kuna baadhi ya mambo, ingawa hayamfanyi Dr. Slaa hakose sifa za kuwa Rais bora, lakini ni dhahiri amechafuka kimaadli!!

Mkubali msikubali!!
 
Wakuu mie nna mtazamo tofauti kidogo, kama kweli nyumba ya babaake Slaa haifai kuishi then wa kumlaumu si Dr. Slaa bali ni serikali ya CCM ambayo imeshindwa kuwapatia watz maisha bora ambayo ni pamoja na makazi bora ya kuishi.

Yes makazi bora ya kuishi ni jukumu la serikali kuhakikisha kuwa uchumi unakuwa na kuspill over poverty reduction kwa kila mtanzania. Hilo CCM wameshindwa si kwa huyo mzee tu bali kwa watanzania wengi.

Having said that tutumie nafasi hii kuwatoa wezi madarakani ili hawa wazee na watanzania wote kwa ujumla waweze kupata maisha bora zaidi.

CHAGUA DR. SLAA, CHAGUA CHADEMA.
 
Wakuu labda mimi niko nyuma lakini wapi Slaa alimtukana mtu? Naomba ni elimishwe kama nimekosea...:confused2:
 
Kwani katika hayo mahojiano, Baba wa Dr. Slaa amelalamika kuwa mtoto wake hajamjengea nyumba? Amelalamika kuwa nyumba anayokaa si nzuri?
 
Kwani katika hayo mahojiano, Baba wa Dr. Slaa amelalamika kuwa mtoto wake hajamjengea nyumba? Amelalamika kuwa nyumba anayokaa si nzuri?

Nimefurahi sana, Najua walidhani kwamba kwa kumuonyesha babayake Dr. Slaa anakaa nyumba ya tope, watanzania watamchukia, hooo.. ona sasa, hii imezidi mpa credit shujaa wetu!

Mkimaliza tuwekeeni basi hayo ma mansion ya msoga mliyo andalia wafalme wa Tanzania ili tuwapigie makofi kwamba kweli mnajali koo zenu lol!
Ila msisahau kutuandalia maelezo sahihi ya jinsi mlivo pata mabilioni ya kujenga hayo mahekalu, make karibia tunairudisha nchi yetu kutoka mikononi mwa mafisadi, ambapo utawala a sheria na haki utachukua nafasi yake.
 
Slaa ni dume la mbengu.

Hata wewe usipojali Mke wako, SHURTI amchukue na amuonyeshe raha ya kuwa na mwanaume kweli na si kama Vaticano na kundi lake, jamaa wenye vibamia. Ondokeni mkalielie huko pembeni na vibamia vyenu.

Mie hata kama akichukua na wake zenu, bado ntampigia tu kura. MWAKA HUU HATUDANGANYWI.

Sintampigia KURA Dr. Slaa mara pale mtu akija na kusema "huyu jamaa ni kiongozi DHAIFU."

Mzinzi ndiye safi kabisa kwani mawazo yakizidi anaenda kupumzika. Mtu wenu alikuwa anafaa sana maana na yeye kwa Wanawake mamamamaaaaa!!!!! Ila Yeye tatizo ni MZIRAY.

MUMKOME kama mlivyokoma mitindi za ............................
 
Anahojiwa Baba yake. Anaishi kwenye nyumba ya tope licha ya mwanawe kuwa bunge for 25 years,

Anaepnda sana kujisomea.

Anaongea kiswahili cha shida but ina mashaka na slaa kugombea hasa kutukanana

Hata watoto wa Nyerere wakati wanasoma walikuwa wanadandia lifti za watoto wa mawaziri wakati baba yao ni rais. Tena wengine wamesomeshwa na misheni wakati baba yao ni rais. Nyerere nyumba ya maana kajengewa na jeshi wakati ameshang'atuka kwenye urais. Kwa hili CCM wanafikiria kuwa ni kashfa kumbe ndo wamempigia debe Slaa bila wao kujua. Slaa tunakuombea mwaka huu ni mwisho wa kutawaliwa na majingili wa uchumi wetu.
 
hamjui vyombo vya habari hasa chama tawala viko kuharibi sifa za watu? mimi sioni kwa nini walaumu eti baba yake anaishi kwenye nyumba ya udongo, hivi kweli tunazaa watoto watusaidie au wajisaidie wenyewe? kama uwezo wa babake ulikuwa wa kujenga nyumba ya tope basi na aendelee kuishi humo.

SLAA kaza buti wangu, tuko pamoja hata kama hutashinda umeonyesha ungangali na kwamba unakubalika.
 
eee! Mungu wa kweli wewe uwawekao wafalme wa dunia nakuomba usikie kilio cha wa tz waliao usiku na mchana, kama ulivyo wapa mfalme daudi watumishi wako baada yakumkataa, sauli tunakuomba umsaidie mwanao dr. Slaa mtumishi wako anaetoa wakati na nafsi yake hata kufa kwa taifa lake tanzania kuwaokoa wanyonge mil.45 ambao wamekuwa wakilia baada ya nchi kutekwa na kikundi kidogo sn ambacho kimeweka pembeni maadili mema yaliyowekwa na mtumishi wako mwalimu na dr. Nyerere, kumbuka hakuna wakusikiliza kio chetu ila wewe mungu wa kweli, tunajua wazi wanauwezo wakila kitu kama vile majeshi yasiyoonekana kwa macho lkn wewe unanguvu zaidi ya hayo, hatutaogopa bali tutakutegemea siku zote, mjalie afya na maono kwa ajli ya watu wako.
Tusome 2nyakati 20.1-26 hatuna sababu yakupigana tunae mungu anaesikiliza kilio cha watu wake.


mungu ibariki tz, mungu mbariki mtumishi wako dr. Slaa

amen
 
Ni mtanzania kama watanzania wengine..Hayo ndio maisha bora kwa kila mtanzania. Kuishi kwake kwenye nyumba ya udongo nani wa kulaumiwa kama si serikali. Angeishi kwenye nyumba mfano wa hekalu ccm wasingekosa cha kusema 'Dr. Slaa alikuwa mwizi.' Dr. Slaa kaza buti sisi tunakuombea kila la heri waache wenye kuchokonoa mambo hata yasiyo wahusu. TBC mkahoji wazazi wa JK,Lipumba na wengineo mbona Dr. Slaa peke yake kama si uhuni ni nini?

Mshahara wa 12m x 12 = 144m kwa miaka 5 tu inatosha kumjengea baba yake nyumba! Sometimes tusitetee ukwepaji wa majukumu. Mimi sipati 12m ila nimeweza kumjengea mama yangu nyumba nzuri kijijini kwetu yeye kashindwa nini?? Isitoshe ana misamaha ya kodi kibao...
 
Hata watoto wa Nyerere wakati wanasoma walikuwa wanadandia lifti za watoto wa mawaziri wakati baba yao ni rais. Tena wengine wamesomeshwa na misheni wakati baba yao ni rais. Nyerere nyumba ya maana kajengewa na jeshi wakati ameshang'atuka kwenye urais. Kwa hili CCM wanafikiria kuwa ni kashfa kumbe ndo wamempigia debe Slaa bila wao kujua. Slaa tunakuombea mwaka huu ni mwisho wa kutawaliwa na majingili wa uchumi wetu.

Na wewe ulipewa hiyo lifti ya mawaziri waliyokuwa wanapewa watoto wa Nyerere? Kuna lies halafu kuna damn lies.:mad2:
 
Back
Top Bottom