Elections 2010 Maisha ya Dr. Slaa ndani ya TBC1

Katika hili Dr. Slaa kachemka na ina onyesha alivyo mbinafsi!! Hebu fikiria, anashindwaje kumjengea a simple and decent house baba yake mzazi wakati;
1. Analala na kimada kwenye apartment kwa miezi zaidi ya 6 sasa,

2. Ni mbunge kwa miaka 15

3. Na anamiliki mashamba makubwa ambayo anayaendesha kibiashara kwa zaidi ya miaka 20

4. Amekuwa akipata kiinua mgongo baada ya kumaliza vipindi vya miaka mitano mitano ya ubunge ambayo ni kiasi cha Tsh. mil 40 mara 3= Mil 120

Kumbukeni wadau a decent house in Karatu can cost around Tsh. 2 mil only (which is a fuel allowance for one month only that he gets as MP)

5. Na vitu vingine nisivyovijua ambavyo vinamuongezea kipato

Kama hawezi kuwa responsible kwa baba yake wa damu kwa kumsaidia kuondokana na maisha ya kifukara kupindukia, atawezaje kumjali bibi yangu aliye Mmbanyambipile kule tukuyu anaishi kwenye nyumba ya udongo?????

I fully support regime change in this country, lakini hivi vitu kama kutembea na mke wa mtu (hata kama alikuwa hajui alipaswa kufanya due diligence ili kujua mwanamke anamchumbia ana vikwazo vyovyote?) na hili lililoibuliwa na TBC1 ni moja ya vitu vitakavyompunguzia kura sana Dr. Slaa!!

Ushauri wa bure: Unapoamua kufanya ama hata ukiwa na dream ya kufanya kazi ya siasa unatakiwa at least uishi maisha ya kiadilifu kwa sababu wapinzani wako watatumia mapungufu yako kama vigezo vya kuwashawishi wapiga kura kama wewe hufai.

Wana JF acheni kumremba Dr. Slaa hata pale anapochemka dhahiri, wenye akili wataona mnapiga porojo kama anazopiga Mh. Makamba!!
 
Vaticano hivi kwanini unakuwa na mawazo potofu kiasi hicho kuwa mbunge kwa miaka 15 sio kujinufaisha mwenyewe alitumwa na wananchi wa karatu kuwatumikia hivyo hizo pesa ama mshahara wake huwasaidia wale wasiojiweza na kuleta maendeleo jimboni kwake. Nikuulize swali moja tu Mwl. Nyerere (RIP) alikaa IKULU kwa 25 hakuna kiongozi alie kaa muda mrefu hivyo IKULU hapa Tanzania na alikuja kujengewa nyumba na JWTZ baada ya kungatuka.

Je Mwl hakuweza kujenga hekalu la kuishi kwa muda wote huo hadi aje kujengewa nyumba na jeshi. Alikuwa na uwezo wa kujenga hata nyumba 100 lakini alikuwa na mapenzi ya dhati kwa wananchi aliokuwa anawatumikia hivyo hakuona busara kujilimbikizia mali alikuwa ni mwananchi wakawaida tu. Hivyo basi ni sawa na Dr. Slaa kuishi maisha ya wakaida kama wananchi wengine.

Pili usiingize mambo ya UDINI swala la Mzee wake Dr. Slaa kuishi kwenye nyumba ya matope ni maisha ya kawaida kwa wananchi wa Tanznania. Kila Mtanzania ametokea kwenye nyumba za Matope na Nyasi hii ndi asili yetu.
 
Brooklyn,
Hata Mwalimu hakujenga kwa miaka zaidi ya 20 alookuwa Rais wa Nchi hii. Wakati mwingine kujenga ni kipaji au tabia
 
Mnakukumbuka nyumbani kwa aliyekuwa Makamu wa Rais, Mrehemu Dr Omar Ali Juma kule Pemba? Huyu bwana alishakuwa WK kule Zanzibar kabla ya kuwa makamu wa Mkapa. Wasafi wapo. Dr Slaa anaweza kuwa mmoja wao ukiondoa ukiwete wake kwa akina mama.
 
Punguzeni ujinga nyie kama mnakauwezo wajengeeni Wazazi wenu nyumba.Sisi ni Waafrika lazima tuwaondolee umasikini wazazi wetu..Kuna mijitu mingi tu na ina utajiri mkubwa lakini wazazi wao hapa Kyela wanaishi nyumba za udongo lakini dar imejenga maghorofa.Hiyo ni tabia ya uchoyo.Sijuhi Karatu,kwa wana Kyela wenzangu hizi nyumba za udongo zinawatesa wazee wetu.
 
Paukwa...... Pakawa ....mnaangalia lakini hamuoni!!! Yanasemwa lakini hamsikii ni nani hao????????????????????
 
Mi naona tofauti. Unawezaje kuwa Mbunge kwa miaka miwili ushindwe kumjengea baba yako a decent house?? Weye mbona usikae kwenye maisha duni? Haiwezekani, kuna tatizo. Naomba wana Jamii Forum msiegemee upande mmoja. Sio kila mtu anamwona Dr Slaa kama next president!!Msinisulubishe. Me mwenzenu, jamani, mkongwe. Angaliaeni msije pata pressure ya ghafla.

Mkongwe waumri au JF?
Kelly
user-online.png
Junior Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
Join DateThu Sep 2010Posts2Thanks0Thanked 0 Times in 0 Posts Rep Power0
 
Anahojiwa Baba yake. Anaishi kwenye nyumba ya tope licha ya mwanawe kuwa bunge for 25 years,

Anaepnda sana kujisomea.

Anaongea kiswahili cha shida but ina mashaka na slaa kugombea hasa kutukanana

hiyo ndiyo definition ya uzalendo.
 
Nadhani kuwa madarakani si kujinufaisha bali ni kutumikia wananchi kwa ujumla. Kuhusu kumjengea babaye nyumba zaweza kuwepo sababu nyingi, moja ninayokuwa nayo ni mtazamo wa mzazi mwenyewe mfano kuna jirani yetu mmoja anakaa majuu miaka kama twenty na home ni Biharamulo (Nyakatuntu kijijini) kwetu TZ kila akitaka kumjengea babaye nyumba, mzee anakataa katakata kwamba hana shida na nyumba akaayo ambayo ni ya udongo. Huu ndo ukweli kwamba amejaribu MARA nyingi in vain.

Sasa kwa mliotazama hicho kipindi je babaye rais mtarajiwa Slaa alikuwa akionesha kuumia au kuonesha kutelekezwa na mwanaye? Mwalimu Nyerere alikuwa madarakani miaka over twenty lakini hakujenga Mansion kule Butiama na kwa walokuwa wakubwa miaka hiyo nadhani mnakumbuka ile nyumba alokuwa anaishi mamaye Nyerere. Hadi Nyerere anastaafu alilazimishwa na Jeshi kujengewa.

Ndiyo ni vizuri kuwa na nyumba nzuri lakini pia tukumbuke kuwa kubwa ni kutumikia watu kwa ujumla. Ni mambo mazuri mangapi Baba wa taifa alitufanyia achilia mbali mapungufu katka utendaji? Nendeni jimboni kwake Slaa muone ni visima vya maji vingapi amewajengea wananchi kwa pesa ambayo si ya serikali? Na mengine mengi.

Ukiangalia mafisadi ni juzi tu wameingia madarakani usishangae kuwa tayari wanamiliki mahoteli ya kitaliii kule Arusha ya star 5 au 4 na wameanza kujenga renting apartments kule Masaki na Oyesterbay na kwingine, usishangae kuona tayari wana zaidi ya 30% ya hisa katika makampuni ya madini na tayari wanafanya biashara ya kuuza magogo haramu ya mbao kutoka DRC, ukiambiwa tayari wanapanga kununua jengo Kule Manhattan NY na wako katika hatua za mwisho usishangae, lakini mbaya zaidi usishangae kuwa wameshiriki katika kukiua kiwanda cha matairi cha General tyre kule Arusha na hao hao wana hisa over 20% katika kiwanda cha matairi cha YANA PAMOJA na Firestone kule Nairobi Kenya.

Nadhani kama ni ujamaa basi Slaa anafaa kuitwa mjamaa halisi si hawa wanaohubiri ujamaa na kujitegemea kisha wanaishi ubepari na unyonyonyaji!
 
hiyo ndiyo definition ya uzalendo.

Hapa tukubali kuwa kuna okosefu wa uwajibikaji. Naamini kujenga nyumba nzuri hakuhitaji pesa nyingi ila inahitaji utambuzi kuwa mtu anahitaji makazi bora na si bora makazi. Fursa za kujenga nyumba nzuri alikuwa nazo na bado anazo. Benki nyingi zinatoa mkopo kwa kutumia mshahara kama dhamana. Tatizo hapa ni vipaumbele vyake vikoje!!!!!!! Kwa mtindo huu sishangai kusikia anaishi nyumba za wageni. Hii ni kasoro kubwa na mhusika anatakiwa kuitambua na kujitambua ili irekebishwe tena haraka sana.
 
Katika hili Dr. Slaa kachemka na ina onyesha alivyo mbinafsi!! Hebu fikiria, anashindwaje kumjengea a simple and decent house baba yake mzazi wakati;
1. Analala na kimada kwenye apartment kwa miezi zaidi ya 6 sasa,

2. Ni mbunge kwa miaka 15

3. Na anamiliki mashamba makubwa ambayo anayaendesha kibiashara kwa zaidi ya miaka 20

4. Amekuwa akipata kiinua mgongo baada ya kumaliza vipindi vya miaka mitano mitano ya ubunge ambayo ni kiasi cha Tsh. mil 40 mara 3= Mil 120

Kumbukeni wadau a decent house in Karatu can cost around Tsh. 2 mil only (which is a fuel allowance for one month only that he gets as MP)

5. Na vitu vingine nisivyovijua ambavyo vinamuongezea kipato

Kama hawezi kuwa responsible kwa baba yake wa damu kwa kumsaidia kuondokana na maisha ya kifukara kupindukia, atawezaje kumjali bibi yangu aliye Mmbanyambipile kule tukuyu anaishi kwenye nyumba ya udongo?????

I fully support regime change in this country, lakini hivi vitu kama kutembea na mke wa mtu (hata kama alikuwa hajui alipaswa kufanya due diligence ili kujua mwanamke anamchumbia ana vikwazo vyovyote?) na hili lililoibuliwa na TBC1 ni moja ya vitu vitakavyompunguzia kura sana Dr. Slaa!!

Ushauri wa bure: Unapoamua kufanya ama hata ukiwa na dream ya kufanya kazi ya siasa unatakiwa at least uishi maisha ya kiadilifu kwa sababu wapinzani wako watatumia mapungufu yako kama vigezo vya kuwashawishi wapiga kura kama wewe hufai.

Wana JF acheni kumremba Dr. Slaa hata pale anapochemka dhahiri, wenye akili wataona mnapiga porojo kama anazopiga Mh. Makamba!!

Umeongea point sana, ila ndo hizi tulikua tunaziita PUMBA POINT toka tukiwa sekondary. umewahi kusikia Baba yake Dr. Slaa amelala na njaa, au nyumba yake inavuja, au hana kitanda? we vipi. Ndo nyie nyie mna akili za kifisadi, unafikiria ukiingia kwenye siasa ujenge nyumba yako nzuri, nyumba ya baba na mama yako, wadogo, wajomba, akina shangazi, wakwe zako, shemeji zako, vimada wako kama KIKWETE ALIVYOFANYA!!

Kwa mimi, najua hela za slaa anatumia kusaidia maendeleo kwenye jimbo lake, na ndio maana, Karatu ni Jimbo lilioendelea kuliko majimbo yote Tanzania (Hilo unalionaje?) hizo zote ni hela za Dr. Slaa, na usisahau kuwa muda wote Slaa amekua mbunge chini ya serikali ya Kifisadi ya CCM ambayo haipeleki maendeleo kwenye majimbo ya wapinzani ili waonekane hawafanyi kazi.

Cha mwisho Dr. Slaa amepitia mafunzo ya upadre, ambayo wanafundishwa kutokua wabinafsi, bali kumjali kila mtu, sio baba yako tu, (na ndio maana, asingeweza kumjengea baba yake hekaru likazungukwa na vijumba vibanda vya majirani.

DR. SLAA IS THE CHANGE WE NEED!!
 
umesahau nyumbani kwao wazili mkuu Pinda palivokuwa? hata cardinali pengo hajafanya lolote kwao huko sumbawanga kwa sababu uongozi siyo opportunity ya kujitajirisha na kuneemesha ukoo wako. hivi hebu nikuulize kwanza huyo babake slaa amelalamika kuwa mwanae hajamjengea nyumba au we umeropoka tu kujifanya kumtetea bila kuwa na locus stand we bush mwanasheria.
 
Halafu wakilamliza kwa baba yake Slaa waende na kule kijiji cha Soga wakahoji wana familia wa JK, wasisahau kule Lindi kwa Salma!
 
TBC walitaka kuonyesha kwamba Slaa ameshindwa hata kumjengea nyumba baba yake jee ataweza kuwahudumia watanzania? Plan yao ime-BACKFIRE na badala yake watanzania tunamuona ni mtanzania mwenzetu kwa maana halisi maana shida zake ni zetu. Nyumba ya udongo ya wazazi wake ndio nyumba za udongo za wazazi wetu!!!! TBC punguzeni kutumiwa.

Najua wengi wa watangazaji hawaikubali hiyo CCM ila, kwavile wanapewa amri na TIDO hawana jinsi.

Najua mnalipwa mishahara kiduchu na inayokatwa kodi kubwa hata hivyo jibu lenu ni Dr. Slaa.

Najua TIDO atataka mtoe habari nyingi ili kumchafua DR, tafadhali jitahidini kuionyesha jamii kuwa MMELAZIMISHWA kufanya hvyo.

Najua mnajua na TIDO anajua kuwa Oktoba 31 Dr. atatinga Ikulu.

Najua MS, Vaticano, Selous na Wengineo bado watajifanya kutokujua kuwa hawajui CCM haitoingia Ikulu.
 
Anahojiwa Baba yake. Anaishi kwenye nyumba ya tope licha ya mwanawe kuwa bunge for 25 years,

Anaepnda sana kujisomea.

Anaongea kiswahili cha shida but ina mashaka na slaa kugombea hasa kutukanana

Nyumba ya baba wa JK (rip) ni ya matope kabisaaa ila imewekwa plasta ya smenti. Fika bagamoyo uwe kama unaelekea Halmashauri ukifika shell ya BP kunja kushoto hesabu nyumba ya nne. Wakati JK akiwa waziri wa Nishati na Madini ile nyumba ilikuwa ya MAKUTI, alipokuwa waziri wa mambo ya nje ndo angalau ikapigwa bati. Sasa Tbc wangekuwa fair wangeonyesha na nyumba ya baba wa JK
 
Wazee ambaom wanaishi na Mh. Jakaya Kikwete huko Bagamoyo wakitupa historia ya maisha yao kwa ujumla.
 
Last edited by a moderator:
Watu wengine wanajaribu kujenga hoja za ajabu ajabu.

Nani amesema kuwa unaweza kwenda kwenye ardhi ya Baba yako, ukamlazimisha ujenge nyumba unayotaka wewe? Ukifanikiwa kwa mzazi wako, ni ajabu. Wazee wengi hawapendi kuona watoto wao kutoka mijini wakija kwenye BOMA lao na kuanza kufanya mabadiliko yoyote wanayotaka.

Kijana akikua, hupewa eneo lake (MJI) ili akaliendeleze anavyotaka yeye na kuondoka kwenye BOMA la Baba yake. Kuanzia muda utakaopewa eneo lako, inakuwa mwiko kukata hata tawi la mti kwenye Boma la Baba yako. Kama kuna watu hapa hawajui hilo, ni vyema wakaenda vijijini na kujifunza maisha ya watu wa huko.

Msifikiri ni rahisi kujenga tu kama mnavyodai hapa. Wazee hawa nao hujisikia fahari kwa majengo (hata kama ni duni) waliyoweza kujenga walipokuwa na nguvu. Kuyabomoa na kujenga yenu, huchukulia kama kudhalilishwa. Mnatafuta laana?
 
Mkuu Recta,
hapo umemaliza yote. Yaani tuna watu wengi wame-lose touch on basics- baada ya kuwa wala rushwa na mafisadi.
Nashukuru kwa kukumbusha hili la msingi.

Watu wengine wanajaribu kujenga hoja za ajabu ajabu.

Nani amesema kuwa unaweza kwenda kwenye ardhi ya Baba yako, ukamlazimisha ujenge nyumba unayotaka wewe? Ukifanikiwa kwa mzazi wako, ni ajabu. Wazee wengi hawapendi kuona watoto wao kutoka mijini wakija kwenye BOMA lao na kuanza kufanya mabadiliko yoyote wanayotaka.

Kijana akikua, hupewa eneo lake (MJI) ili akaliendeleze anavyotaka yeye na kuondoka kwenye BOMA la Baba yake. Kuanzia muda utakaopewa eneo lako, inakuwa mwiko kukata hata tawi la mti kwenye Boma la Baba yako. Kama kuna watu hapa hawajui hilo, ni vyema wakaenda vijijini na kujifunza maisha ya watu wa huko.

Msifikiri ni rahisi kujenga tu kama mnavyodai hapa. Wazee hawa nao hujisikia fahari kwa majengo (hata kama ni duni) waliyoweza kujenga walipokuwa na nguvu. Kuyabomoa na kujenga yenu, huchukulia kama kudhalilishwa. Mnatafuta laana?
 
Kuwa MBUNGE kwa majimbo masikini kama haya Tanzania ni MZIGO. Kama wewe ni mwadilifu kweli na unajali shida za watu waliokuchagua huwezi kubaki na hela ya kujenga.

Isipokuwa hela za kwenda "kuchumbia" wake za watu ndiyo unazo?
 
Back
Top Bottom