Mahusiano yanataka kuniua kwa stress. Nimezaa watoto wawili nje ya ndoa, mke wangu amenisamehe ila natamani kuachana naye

selemangrace346

JF-Expert Member
Sep 26, 2018
450
613
Wasalaamu wakuu!

Imenilazimu kuja na uzi huu baada ya kuona Hali inazidi kuwa Tete

Mwaka 2017 nilibahatika kukutana na Mrembo fulani shombeshombe Mkoani Pwani(home), Ambaye nlimpambania kwa nguvu zote ili mwisho wa siku aje kuwa mke wangu. Inshallah Nlifanikiwa kumnasa Binti huyo na Tukaanza uhusiano. Baada ya muda nlimtambulisha kwa familia yangu na kiukweli walimkubali sana na mama alinisisitiza nimuoe na nlifanya hivo kiukweli maana sikuona cha kusubiri

Mwaka 2018 nilifanikiwa kupata Ajira rasmi Serikalini kama Engineer Mkoani Tanga, nilikwenda kuripoti kazini na kuweka mambo sawa ya kimakazi, Nlipokuwa kule nlikutana na Dada mmoja ambaye ni Engineer pia alitokea kuwa mwenyeji wangu na kuonekana kunijali sana yaani muda mwingi alitaka tuwe pamoja, unfortunatelly nikajikuta navunja amri ya saba na haikuchukua muda yule dada akapata ujauzito

Mimba ikafikia miezi 8 hivyo ikabidi arudi nyumbani kwao kwenda kujifungua huko Arusha , kipindi yupo kule nimekaa kama mwezi mmoja hivi ndipo tena nikawa nimekutana na Binti mwingine ambaye ni kabila langu naye alikuwa ni mfanyakazi( Askari), akatokea kunipenda sana na kunijali nikajikuta nimeanzisha uhusiano na yeye tena yaani ilikuwa sijui shetani gani yule alinipitia kipindi hicho.

As time goes yule dada nae akapata ujauzito na movie ikaanzia hapo maana kiukweli hawa wote sikuwa nimewakubali na wao ndiyo kama walinitongoza, akili yangu yote ilikuwa kwa mke wangu, But wote sikuwa nimewaweka wazi kuwa nina mke nyumbani

Haikuchukua muda mke wangu naye akataka aje tuishi pamoja huku nilipo, nikamkatalia kwanza maana nilijua huku ni pa moto sana asubiri niweke mambo kwanza kama itawezekana na nilikuwa mkali sana kwake. Kiukwel akili yake sijui ilimtuma vipi , Baada ya siku kadhaa ananiambia yupo stand niende nikampokee ilibidi nifanye hivyo, kiukwel nilitamani ardhi ipasuke.

Wakuu ilikuwa bonge ya movie, maana yule Askari aliposikia kuwa nimepata mgeni( mke ) alikuja usiku huo huo na kufanya fujo pale nyumbani, Mke wangu alipata kujua kuhusu hiyo situation kwa majirani na ikabidi nimweke wazi kuwa nimeteleza kuna watu wawili wana ujauzito wangu.

Mazungumzo yalikuwa si mazuri maana alilia sana aliposikia hizo taarifa kiukwel,but finally mke wangu alinisamehe na akakubali kuendelea kuishi hii ulikuwa ni zaidi ya upendo maana nilitegemea asingekubali kuendelea kuishi na mimi,

As time goes wakuu maisha kidogo yamekuwa magumu sana kelele haziishi kwa hawa wanawake hadi inafikia stage natamani kuachana na mke wangu japo ninampenda sana ili tu nchukue Mwanamke mmoja wapo kati ya hao wenye watoto na ni wafanyakazi kidogo nahisi nitapata ahueni ya maisha maana hata jamii inanchukulia kuwa ni mtu mbaya sana yaani sina amani japo kiukweli nampenda sana mke wangu.

Naomba ushauri wakuu je niendelee tu na mke wangu ambaye amekubali kuishi na mm licha ya mazingira hayo magumu au niachane nae nichukue mmoja kati ya hao wenye watoto?
 
Mkuu omba uhamisho hama mkoa mi nilifanya hivyo kuna mwanajeshi ofisa kabisa alinipenda sana sema mlevi kila nikijalibu kumuacha haelewi nikaamua kuhama mkoa saizi niko shwali kabisa ukiendelea kubaki hapo Tanga watakuvuruga hao ha ha ha ha ha ila nimecheka mkuu utakua unapenda sana utelezi
NB : Maendeleo hayana chama jikinge na korona nawa mikono na maji tiririka
 
Mudau hapo juu amekushauri vizuri sana, nami najazia tu usimuache mkeo unaempenda jiepushe kuwaza hao wanawake wenye kazi ili upate pa kutelezea, so omba uhamisho fasta ondoka, unaweza hata ongea na Mkuu wako wa kazi ukamueleza situation ukapata kituo kingine cha kazi, vinginevyo naiona hatari iliyoko mbele yako kama utamuacha mkeo!

Sent using kidole gumba
 
Namuonea mkeo huruma.
Mkeo unamaanisha hazai? Ila huyo ndiyo mkeo, unataka umpige chini kwasababu ya hao wakupita, ona wasivyo na hekima. Mwenye Mali Kaja wao wanakuja kuleta vurugu. Mkeo alivyo na hekima hakuleta makuu, anafahamu wewe ndiyo mume wake, akasamehe.

Alafu unawaza kumuacha kwaajili ya hao vioja. Umepigwa upofu Kama Mkristo sali Sana, na jutia dhambi zako za uzinzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwehu wewe,kwa taarifa yako huyo mwanamke hajakisamehe Wala Nini NI vile anaona aibu kuachika anakuchota happy ukijaa kwake atakufanyia kitu ambacho atahisi kinampunguzia maumivu ya kusalitiwa double na wewe..... wanaume mnarahisisha maisha eeti kanosamehe......ungekuwa wewe ungemsamehe?
 
Asikwambie mtu.ndoa za mbali huwa hazidumu.ukikuta mko na ndoa za mbali bado ziko vizuri ni mambo mawili tuu makubwa .mmoja wenu anachepuka hasa mwanaume.au wote jua limeasha zama aka wazee.tuje kwenye maada

Mkuu usijaribu kumuacha huyo mwanamke uliyemuoa .huyo ni mwanamke mvumilivu sana kuwahi kutokea.hao wote wawili ni pasua kichwa hasa huyo afande sele.sema huyo mhandisi hana shida yeye alikuwa anataka mtoto japo pia allidhani uko single.

unaweza kufanya yafuatayo kabla ya kufikiria kuhama
1.Kaa na mmoja mmoja waeleze ukweli kwamba hutawaoa kwa sababu tayari una ndoa kifahamiana nao, ila mkubaliane namna mtakavyolea mtoto.ijapo huyo afande atakupa masharti magumu sana ya kukukomoa.wewe kubaliana naye tuu.utekelezaji wake litakuwa jambo lingine
2.Muweke wazi mke wako kwamba unataka kutafuta uhamisho ili kuilinda ndoa yenu
3.Anza kwenda ibadani.ili kuimarika kisaokolojia na kiroho.sababu unakokwenda hao wanaweza kwenda kwa wataalamu wakufix ukome.
4.Uwe na kitu umejifunza hapo.pia acha kupenda miteremko siku nyingine.
5.process uhamisho taratibu.kwa sababu ukifanya haraka unaweza pelekwa mkoa mbaya
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom