Mahojiano na aliyenusurika katika shambulio lililoua askari wanne

Kuna kitu hakijakaa sawa kichwani mwa Watanzania na sijui nani atakiweka sawa. Kushangilia au kufurahia kifo cha binadamu mwenzako!!!! hata kama amekutendea ubaya kwa namna gani lakini katika kuondoka duniani inatakiwa tusikitike yawezekana angeweza kukomba mshamaha na mkamalizana. Lakini pia bila kujali ni askari, mwandishi wa habari, mwanachama wa chama cha upinzani au tawala wote ni binadam mauaji kwa namna yoyote ile yakemewe na kulaaniwa na mpenda haki yeyote. Eee MUNGU tuepushie uchuro huu.
Wanasahau Kesho inaweza ikatokea kwao.
 
r.i.p polic we2 inackitsha sana. na nyie police heb intelgensia iamishien kwenye kupambana na uhalifu. mpo makn mno kuwakibil raia wasio kuwa na silaha na kupiga wa2 kweny mkutano ya kisiasa
 
Eti hizo silaha zinaweza kutumika miilini mwetu,eboooh,hata wasingepora hao mlishaaapa zitatumika miilini mwetu sept mosi,na mlituambia kibiriti cha gesi kitatulipukia,serikali initathimini na kuelewa madhumuni ya kuwa na jeshi la polisi ni nini
 
ANGALIZO:
Kuna baadhi ya watu wanaleta kejeli kuhusiana na tukio hili ambalo linasikitisha sana kwa watu wanaofahamu misingi ya kibinadamu.

Ni kweli binadamu tunatofautiana katika mitazamo lakini mizania ya kibinadamu huwa inapimwa wakati wa majonzi.

Hizo silaha walizopora inawezekana kesho zikatumika katika mwili wako au ndugu yako. Kama hujabahatika kutembelewa na majambazi huwezi kuelewa maana na uzito wa maneno yangu.

Tuombe uzima na Mungu awape faraja ndugu wa askari waliopoteza maisha wakiwa katika kazi ya kulinda maisha na mali za watanzania.

R>I>P askari wetu. Niasiye fikiri sawa sawa anaweza kuleta kejeli kwenye hili. Ni kweli kuna mikwaruzao muda mwingine kati ya Raia na wanausalama ,lakini la Majambazi wao ni maadui zetu kwa hiyo ushirikiano wa sisi Polisi na Wananchi ni wakipaumbele kuliko jambo lingine.
 
Hebu nisaidien hawa ni majambazi ama ni walipiza kisasi?? Kwa hio walikuja kuua polisi na kuondoka tu hata hawakujaribu kuvunja bank ikashindikana?
 
R>I>P askari wetu. Niasiye fikiri sawa sawa anaweza kuleta kejeli kwenye hili. Ni kweli kuna mikwaruzao muda mwingine kati ya Raia na wanausalama ,lakini la Majambazi wao ni maadui zetu kwa hiyo ushirikiano wa sisi Polisi na Wananchi ni wakipaumbele kuliko jambo lingine.
Matatizo tunayetengeneza wenyewe hayo.Nikipeleka taarifa za kuwa nawahisi watu fulani kama wana jambo fulani wanataka kulifanya.Siri hufuja haraka sana.Haya uvamizi huu kwa polisi si kwa mara ya kwanza,au tumesahau kuhusu kule Tanga,Ushirombo na kwengineko?Je kwa haya matukio yote ya nyuma polisi walitoa ripoti zipi?Hatujaona badala yake hayo mauji yote yalipelekwa kwenye majukwaa na kuacha kufutilia nini hasa chanzo.Pia tukumbuke tuliwatangazia hawa jamaa kuwa ukikutana nao polisi wapige tu na kuua,je unafikiri wao wataacha kuua bila huruma?Hawawezi hata kidogo kuwaacha askari,hii ni vita ya chini kwa chini.Wanaongea ongea sana na kuropoka na kukurupuka ndio wanasababisha haya yote yatokee.Nimejisikia vibaya sana kwa hayo mauaji ya namna hiyo.Hii nguvu iliyoelekezwa kuzuia maandamano kama ingeliwetumika toka muda wa tukio kutokea mpaka sasa naamini wangekuwa wote wamekamtwa.Tukiacha ubabaishaji na kuruka ruka hovyo na maneno yasio na tija kwa nchi kama hii,jeshi la polisi litakuwa sehemu salama,na raia watatoa ushirikiano kwa kadri wawezavyo.Ila kwa sasa raia hawana uaminifu tena na nyie baada ya kuanza kutumika hovyo hovyo na jamaa zenu wa huko juu.Tunaishi nanyi mtaani na mnajua fika maisha yalivyo na uhalisia ulipo,mnayoyafanya kwa uovu yatawarudia.Tendeni haki mitaani na jalini maisha ya watu wanaotaabika kipindi hiki.Acheni hayo maigizo,kuna binadamu hawaigizi tena siku hizi.Kwao kutoa roho kama hivi ni kitu chepesi sana.Hatuko karne ya 10 sasa hivi.AMKENI NA TAMBUENI NINI KINAWAKABILI NA PIA MJUE HUKU MTAANI WATU WANAJUA MAMBO MENGI SANA MAZITO ZAIDI YA NINYI MNAVYOFAHAMU.R.I.P&POLE KWA FAMILIA PIA.
 
rip..Polisi waache tabia ya kuchat na simu while wapo lindo..Ushauri polisi watumie nguvu nyingi katika mazoezi ya kupambana na wahalifu kuliko mazoezi ya kupambana na raia wema kwenye maandamano
 
Polisi kufanya mazoezi ni amri, na taratibu za jeshi hakuna kukataa amri, kwa hiyo kuwatuhumu polisi siini kama kuna mantiki yoyote, wao wanatekeleza majukumu chini ya amri za viongozi wao,lakini pia kunapotokea mauaji kama hivyo halafu ukatoa lugha yoyote inayoonesha polisi kushindwa inaonekana unawajua waliokuwa wanashindana nao, hii siyo sawa hata kidogo,wafiwa na wanandugu wa hao waliopoteza maisha wengine wamo humu jf
Kufanya hivyo ni kufanya uchochezi kwa njia ya mtandao

Tatizo kuna watu wanajisahau, kujifungia chumbani kwako ukichati na smartphone yako kunakuondolea faragha na kukuweka hadharani kwa njia ya mtandao, wewe unabaki na hisia za kuwa peke yako!!
Mtakuja lipa madeni ya watu wengine kwa kujitoa akiri!!
Lazima mtenganishe,
Mazoezi ya polisi,
Ukuta,
Na ujambazi, hapo kila kitu kinajitegemea
 
Siku zote tunajifunza kutokana na makosa.
Ni wakati wa jeshi la polisi kufanya kazi yake kwa weledi bila kuonekana kutumika na upande fulani dhidi ya upande mwingine.
Mazoezi ya hadharani ya siku mbili zilizopita yameonesha dhahiri jeshi la polisi lipo kwa ajili ya kupambana na upinzani. Hali hii inaleta uhasama kati ya polisi na upinzani ambao sio wachache kwa mujibu wa uchaguzi uliopita.

Kwa sasa ni vigumu mno kwa raia mwema kuweza kusaidia jeshi la polisi kwa sababu ni kama wameshatengeneza uhasama wa kudumu kutokana na kauli tata za viongozi zinazowasisitiza wananchi kuwaogopa polisi.
RIP polisi wetu..
Kama nimekuelewa vizuri ni kweli kabisa mkuu kwa hali tuliofikia sasa ni ngumu kwa raia kutoa taarifa za kuisaidia polisi hii inatokana na vitendo vya polisi kuegemea upande mmoja wa serikali na kuukandamiza ipinzani sasa yatawatokea puani
 
Hebu nisaidien hawa ni majambazi ama ni walipiza kisasi?? Kwa hio walikuja kuua polisi na kuondoka tu hata hawakujaribu kuvunja bank ikashindikana?
Mie mwenyewe najiuliza hivyo hivyo... Hivi hao majambazi walikuja kupora bank, au walikuja kuua askari ili wapore bunduki zao?

Na kama walienda kupora bunduki,nia yao wakazifanyie kazi gani hizo bunduki??
 
Police nao waache kutumika vibaya na wanasiasa...Haiwezekani inteligensia za Police ziwe zinaona mikutano na maandamano ya vyama vya upinzani tu lakini ujambazi haiuoni ...Iwe fundisho kwao wafanye kazi za kupambana na ujambazi sio kupambana na raia wasiokuwa hata na fimbo
MKUU BAADAE HAYA MAANDISHI UTAKUJA KUYAKANA WAKIAMUA KUYATUMIA KUANZA NAYO.
 
Dah sijui hata kwanini umejua kusoma na kuandika. Mungu akusamehe acha itikadi kwenye mambo ya msingi yaliyopoteza uhai wa watu, ndugu na jamaa. Kama mmoja wao angekuwa nduguyo usingeleta upuuzi huo Mkuu. So sad

Ana sababu ya kusema hivi... sio lazima kila mtu awe na mtazamo wako.. tumepitia maisha tofauti. Ni kuvumiliana tu...
 
nadhani hao majambazi walikuwa wanapima kama mazoezi waliokuwa wanafanya askari yamewasaidia au laa.askari wamepewa practical bila kujua Mungu awarehemu
 
Police nao waache kutumika vibaya na wanasiasa...Haiwezekani inteligensia za Police ziwe zinaona mikutano na maandamano ya vyama vya upinzani tu lakini ujambazi haiuoni ...Iwe fundisho kwao wafanye kazi za kupambana na ujambazi sio kupambana na raia wasiokuwa hata na fimbo

Mkuu bado hujaelimika tu mpaka leo?.....hachia huo UKUTA
 
Wapumzike kwa amani vijana wetu. Wameacha ndugu jamaa na familia zinazowapenda na kuwategemea sana
Kuna ongezeko kubwa la uhalifu siku za karibuni, lakini askari wetu wako kwenye mazoezi mazito tena yanayoonekana live mitaani (kitu ambacho nadhani sio sahihi)kuonyesha utayari na umahiri wao (wa kupambana na upinzani? Nisihukumu)
Jeshi la polisi linapaswa kujitambua na kujitafakari, askari wengi vijana ndio wameanza kazi jeshi la polisi, bado hawajawa na uzoefu kazini...mbaya zaidi wamekutana na adha ya mazoezi yenye kutesa na kuchosha mno...kwa ajili ya show off za ubabe usio na maana yoyote
Wanachoka mno ila hawana pa kusemea... wana changamoto za maisha ni binadamu wanahitaji kupumzika lakini wakubwa hawajui hilo
Wengi siku hizi utawakuta kwenye vituo vya polisi kwenye mageti ukiwaangalia unasoma kabisa sura za uchovu na kukata tamaa
Wana kazi zenye kukera kuhoji wanaoingia kituoni, kuwapigia salute wakubwa wote kila dakika wanapopita hapo, kutumwatumwa kila wakati kama wasichana wa kazi
Wahurumieni hawa vijana sisi tunaoongea nao tunajua wanachoka mno . wanafanya kazi kwa shift muda wa kuwa off Wapumzike wanatakiwa kwenye gwaride
Kwa jinsi hii hata wakivamiwa ni ngumu kujibu mashambulizi
Wasomapo ujumbe wako nao pia wawe na huruma kwa raia. Kwa mfano yule askari aliyemtupukula mwandishi wa habari kule iringa unadhani kitendo kile kinajenga mahusiano mema kati ya polisi na raia wema?

Hawatawanyi waandamanaji ispokuwa wamepiga mabom ya machozi ya kutosha!!! Hawaoni wanajipaka nuksi mbele ya wenyenchi?

Sipendi wauliwe lakini nimefurahiswa na jinsi walivyoumbuliwa hasa wale waliojitoa kimasomaso luningani wakisema "Tuko imara kabisa"
 
Inasikitisha sana Mungu awape nguvu familia za hao askari wetu. Pia walale pema Mbinguni Amen
 
Back
Top Bottom