Indian
JF-Expert Member
- Oct 27, 2012
- 821
- 708
Siku zote tunajifunza kutokana na makosa.
Ni wakati wa jeshi la polisi kufanya kazi yake kwa weledi bila kuonekana kutumika na upande fulani dhidi ya upande mwingine.
Mazoezi ya hadharani ya siku mbili zilizopita yameonesha dhahiri jeshi la polisi lipo kwa ajili ya kupambana na upinzani. Hali hii inaleta uhasama kati ya polisi na upinzani ambao sio wachache kwa mujibu wa uchaguzi uliopita.
Kwa sasa ni vigumu mno kwa raia mwema kuweza kusaidia jeshi la polisi kwa sababu ni kama wameshatengeneza uhasama wa kudumu kutokana na kauli tata za viongozi zinazowasisitiza wananchi kuwaogopa polisi.
RIP polisi wetu. Mmetutangulia hata kabla ya 1 sept.
Mwigulu anasema hiki sio kibiriti cha njiti ni gesi, hizi kauli hazifai kabisa sote ni dhaifu, viongozi wanatengeneza mazingira ya chuki kama vile wako usingizini. wanafikiri hao askari ni robot?