Mahojiano na aliyenusurika katika shambulio lililoua askari wanne

Police nao waache kutumika vibaya na wanasiasa...Haiwezekani inteligensia za Police ziwe zinaona mikutano na maandamano ya vyama vya upinzani tu lakini ujambazi haiuoni ...Iwe fundisho kwao wafanye kazi za kupambana na ujambazi sio kupambana na raia wasiokuwa hata na fimbo
Acha upuuuzi wewe, intelligensia ya maandamano kivipi? Wee hukumsikia kamanda wenu akiwa laivu kutangaza mwenyewe maandamano mnayopangaga kufanya?
 
Kwanza niwape pole sana Polisi na familia za askari waliouawa. Pili polisi lazima wafahamu kuwa kuna tatizo sana la askari kulinda usalama wa raia, walijisahau sana ikafika mahali mpaka majambazi yakaona uwezekano wa kupambana na polisi. Naweza kusema wamewalea sana wezi na majambazi. Sikuwa nafahamu kama jeshi la polisi lina vyombo imara na madhubuti vya kulinda usalama wa raia, hizi siku mbili wametuonesha wanazo nguvu, sasa nachoshindwa kuelewa inakuwaje majambazi yatende haya yote na hata kujiaminisha kwenda kwenye makao ya polisi (ref staki shari incident) na kufanya ualifu? Mh Mwiguli naamini Uwezo unao wa kubadili hii dhana ya majambazi kwenye ardhi ya Tanzania. Kuweni makini na achene masihara na wezi na majambazi, ifike mahali kila mtu anayeona alternative ya maisha ni kuiba aogope. Nchi zingine mbona zimeweza? wakikukamata tu ndio mwisho wako. Lkn sisi tumezoea kuona majambazi yanapelekwa polisi na kurudi, kufanya masihala na waalifu sio jambo jema.
Halafu polisi wamejiingiza kwenye biashara halali na zisizo halali kwahiyo wanatoa siri za jeshi hilo kupitia mahusiano ya kibiashara
 
Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba anasema tukio limeondoa maisha ya askari wanne.

Majeruhi anaitwa Ally Chionda ambaye ni mfanyabiashara wa duka la vifaa vya ujenzi karibu na benki ya CRDB ambayo pilisi wamepoteza maisha.

Anadai walikuja majambazi kwenye muda kama wa saa 1:15 usiku wakiwa na pikipiki kama tano na kila pikipiki ilikuwa na watu wawili.

Kulikuwa na watu sita au saba ambao walikuwa wamebeba bunduki.

Walipofika walianza kupiga risasi upande wa eneo la benki na upande wa duka lake.

Bahati mbaya risasi moja ilimpata kwenye mguu wa kushoto ikatokeza na kwenda tena kwenye mguu wa kulia.

Majeruhi anaendelea vizuri na anategemea kufanyiwa x-ray kwa uchunguzi zaidi.

VIDEO.

ANGALIZO:
Kuna baadhi ya watu wanaleta kejeli kuhusiana na tukio hili ambalo linasikitisha sana kwa watu wanaofahamu misingi ya kibinadamu.

Ni kweli binadamu tunatofautiana katika mitazamo lakini mizania ya kibinadamu huwa inapimwa wakati wa majonzi.

Hizo silaha walizopora inawezekana kesho zikatumika katika mwili wako au ndugu yako.

Tuombe uzima na Mungu awape faraja ndugu wa askari waliopoteza maisha wakiwa katika kazi ya kulinda maisha na mali za watanzania.

Mkuu kumbe na wewe unajua kuna kitu kinaitwa "misingi ya kibinadamu" mbona kutwa unasheherekea kuwa kuna binadamu watavunjwa miguu na wengine kuuliwa tarehe 1 September?
 
Police nao waache kutumika vibaya na wanasiasa...Haiwezekani inteligensia za Police ziwe zinaona mikutano na maandamano ya vyama vya upinzani tu lakini ujambazi haiuoni ...Iwe fundisho kwao wafanye kazi za kupambana na ujambazi sio kupambana na raia wasiokuwa hata na fimbo
Kwa nini unajikita kwa polisi pekee wakati kuna wananchi wawili wamejeruhiwa katika shambulio hilo na wako hospitali.

Jaribu kuangalia picha kwa ukubwa wake!
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Well said mkuu. Linapokuja suala la maisha/uhai ni kitu kisichohitaji masihara wala kejeli! Na ni kweli pia hiyo silaha kesho yaweza kukudhuru wewe au kama sio wewe ni ndugu jamaa au mtanzania mwingine yeyote ambae ni nguvu kazi!

Mkuu kumbuka risasi/silaha aliyopigwanayo SHEKH PONDA MOROGORO na Mwandishi wa Habari MWANGOSI ziliibwa wapi? hao sio Watu

Tatizo haliwezi kuisha tu huku POLISI wakiwakandamiza RAIA
 
Hii kitu ni serious halafu watu wanafanya mzaha.
Siku si nyingi polisi walendesha zoezi la usajili wa silaha na hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa uwepo wa silaha zisizo rasmi kwenye mikono ya watu waovu.
Kitendi hiko cha mbagala kinaonyesha kuwa watu waovu wana njaa ya silaha kwa ajili ya mambo yao. Ndio maana baada ya kupora silaha wametokomea.
Maana yake ni kwamba silaha zilizo kwenye mikono isiyo rasmi zinaongezeka.
Na tutake au tusitake zitatumika katika matukio ya kihalifu humu humu nchini.
Hili suala haliwahusu polisi peke yao.
YATUPASA KUWA MAKINI SANA.
Hivi kwanini Jambazi akikamatwa anapelekwa mahakamani?. Ndiyo maana kila siku matukio kama haya hayataisha.
 
Well said mkuu. Linapokuja suala la maisha/uhai ni kitu kisichohitaji masihara wala kejeli! Na ni kweli pia hiyo silaha kesho yaweza kukudhuru wewe au kama sio wewe ni ndugu jamaa au mtanzania mwingine yeyote ambae ni nguvu kazi!
Tatizo hao hao polisi wanatoa uhai wa raia asiye hata na fimbo. Kwa hiyo unaposema tusicheze na uhai wa binadamu, ujumbe wako unatakiwa uwafikie polisi. Angalia mwandishi Daudi Mwangosi (RIP), alikuwa na kamera tu, lakini akauawa na askari wetu tuliowaamini kutulinda, tukalipa kodi iliyokuja kununua mabomu yaliyomuua raia asiyeweza kujitetea!
 
Narudia tena, wahalifu fanyeni uhalifu wenu wote lakini msiue polisi, ila na ninyi polisi muanze sasa kuboresha mahusiano yenu na raia maana tangu utawala huu uingie madarakani mahusiano yenu na raia yemaharibika sana, na intelejensia yenu ianze kujikita kwenye uhalifu sio kwenye upinzani, itafika wakati wananchi wataanza kushangilia ikitokea mauaji ya polisi
 
Kamanda Siro hana mipango madhubuti ya kuwadhibiti wahalifu na majambazi tatizo nae kashajiingiza kwenye siasa na kusahau kazi yake..kipindi chake hiki Panya road wameongezeka,majambazi pia,hata wakabaji ndo usiseme afu anadiriki kukwambia hatuhitaji msaada kwa raia maana tumejipanga kikamilifu kupambana na wahalifu,ushawahi ona wapi mnafanya oparesheni ya kuwakamata wahalifu bila kuwashirikisha raia wema
Mwisho; wasijikite kupambana na UKUTA huku upande mwingine wanajisahau ndipo majambazi yanachukua point 3 muhimu
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Hii kitu ni serious halafu watu wanafanya mzaha.
Siku si nyingi polisi walendesha zoezi la usajili wa silaha na hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa uwepo wa silaha zisizo rasmi kwenye mikono ya watu waovu.
Kitendi hiko cha mbagala kinaonyesha kuwa watu waovu wana njaa ya silaha kwa ajili ya mambo yao. Ndio maana baada ya kupora silaha wametokomea.
Maana yake ni kwamba silaha zilizo kwenye mikono isiyo rasmi zinaongezeka.
Na tutake au tusitake zitatumika katika matukio ya kihalifu humu humu nchini.
Hili suala haliwahusu polisi peke yao.
YATUPASA KUWA MAKINI SANA.
Nisiongelee tukio lenyewe, bali zoezi la usajili wa silaha.
Hivi unaamini kwamba wahalifu au wale wanaomiliki silaha kinyume na taratibu walisalimisha silaha zao kweli? Yaani jambazi asalimishe silaha yake asiyomiliki kihalali halafu kesho yake akavamie lindo au kituo cha polisi ili apore silaha nyingine? Waliosajili ni wale wenye nia njema tu.

Kifupi bado polisi, kama yalivyo maeneo mengine ya utendaji nchini wanahitaji kujipanga upya.

Kuhusu kejeli zinazotokeza, nadhani polisi, serikali na wapenzi wa CCM wamezitaka wenyewe. Hii ni kwa sababu jeshi la polisi limejipambanua kama lipo maalum kukandamiza wapinzani badala ya kuwa neutral. Haiwezekani raia wanapanga kuandamana bila hata fimbo wala jiwe lakini karibia mwezi sasa tunaona polisi wanafanya mazoezi ya vitisho mitaani na kutishia kuvunja miguu na hata kuua watu. Huu uhasama wameutaka wenyewe. Na linatakiwa liwe fundisho kwa kila mtu. Usitegemee huruma pale yanapokukuta wakati wewe huna huruma unapokuwa na maamuzi na nguvu. Yaani ubinadamu kwao ni vitisho vya bunduki nzito na mabomu mitaani? Polisi wanakabilije waandamanaji kwa nguvu namna hiyo badala ya kuwalinda ili wafike salama huko waendako ikiwa ni pamoja na kuzuia wale kenge kwenye msafara wa mamba, ambao watataka kutumia mwanya huo kusumbua raia na mali zao?

Polisi wajichunguze
CCM wajichunguze
Serikali ijichunguze
Watanzania wajichunguze
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Lameck kupose kwenye vyombo vya habari huku umevaa uso wa simanzi ya kutengeneza na kuongea kwa tuo huku ukiwa kwenye mavazi rasmi ya jeshi la polisi haitoshi kabisa
Achana na ambitions, hebu mtafute Mrema akuambie yeye alifanyaje utu uzima dawa you can learn something crucial from them . ukiwa mwerevu unaweza kuleta mapinduzi makubwa sana kwenye jeshi la polisi
Ila ukibaki na hiyo hulka yako utavaa nyuso nyingi za simanzi kabla hujatoka hapo
nilisikia iyo nafas yake ilitakiwa apewe mrema ngosha alidhamiria ila mizengwe tu ndio ngosha ikabidi abadili
 
Kamanda Siro hana mipango madhubuti ya kuwadhibiti wahalifu na majambazi tatizo nae kashajiingiza kwenye siasa na kusahau kazi yake..kipindi chake hiki Panya road wameongezeka,majambazi pia,hata wakabaji ndo usiseme afu anadiriki kukwambia hatuhitaji msaada kwa raia maana tumejipanga kikamilifu kupambana na wahalifu,ushawahi ona wapi mnafanya oparesheni ya kuwakamata wahalifu bila kuwashirikisha raia wema
Mwisho; wasijikite kupambana na UKUTA huku upande mwingine wanajisahau ndipo majambazi yanachukua point 3 muhimu
kamwe chini ya hiki chama usitegeme ulinzi au msaada wa polisi jilinde mwenyewe be vigilant. Kama una uwezo weka bajet kubwa ya kujilinda kama bullet proof car, live in a gated community with electric fence and night vision surveillance cameras etc
 
Shukran kwa taarifa hii na kauli nzuri za maelekezo. Inasikitisha kuona mwanadamu anamkasifu mlinda usalama badala ya kulaani majambazi. Wao ni walinda usalama popote pale hata ktk mikutano hiyo kwakuwa haijaruhusiwa kutokana na sababu za kiusalama kwakuwa kauli nyingi zinaashiria uvunjifu wa amani na kuingilia kati utendaji Serikalini. Hiyo mikutano si ifanyike kule ilikoruhusiwa?
Pamoja na kuwahurumia polisi waliopoteza maisha pamoja na kuhurumia familia zao, naomba kutofautiana na wewe kuhusiana na mikutano na maandamano. Hayo maandamano na mikutano yamekatazwa kwa sababu zipi za kiusalama? Hiyo hali ya hatari iliyopo hapa nchini iko wapi, na kuna vitisho gani Tanzania hii hadi kuzuia mikusanyiko? Nasikia kuna mahali watu wameambiwa mwisho wa kuonekekana barabarani/mitaani ni saa nne usiku. Si mnaokoteza vijisababu vya kipuuzi mradi tu muwazuie chadema kufanya mikutano? Kuna kipindi mkasingizia ugonjwa usiojulikana Dodoma, kesho yake mkazuia Mahafali Moshi mkakosa sababu maana huo 'ugonjwa' haukuwepo Moshi.
Sasa hivi hakuna tena sababu za kiusalama, ila mwenye nchi anasema wakifanya mikutano watu watakosa muda wa kufanya kazi! Sio tena habari ya usalama hapa! nashangaa wewe sababu hiyo umeitoa wapi leo hii.
 
Sifa ya wateule Wa mkuu ni wale wanaoonekana kuwa na uwezo Wa kudhibiti wapinzani (vyama vya upinzani).
Hiyo ndiyo sifa kuu. Tunadhani tatizo kubwa la taifa letu ni vyama vya upinzani. Hatuwazii uchumi, wala uharifu.
Mentality hii isipodirika tutakua kwenye matatizo makubwa sana.
 
Lameck kupose kwenye vyombo vya habari huku umevaa uso wa simanzi ya kutengeneza na kuongea kwa tuo huku ukiwa kwenye mavazi rasmi ya jeshi la polisi haitoshi kabisa
Binafsi nimeona ni uigizaji uliotukuka......Anyway ''Mkulu'' anafarijika na kuhadaika sana ukifanya haya..
 
Mkuu kumbuka risasi/silaha aliyopigwanayo SHEKH PONDA MOROGORO na Mwandishi wa Habari MWANGOSI ziliibwa wapi? hao sio Watu

Tatizo haliwezi kuisha tu huku POLISI wakiwakandamiza RAIA
Na sio hao tu uliowataja. Wapo wengi sana, na nina hakika mazoezi yanayoendelea mitaani ni kwa ajili ya kutoa roho za watu na kujeruhi raia, kwa kutumia silaha zilizochukuliwa moja kwa moja kwenye ghala la silaha la polisi...si kuibwa na majambazi.

Tuache double standards. hakuna anayefurahia ujambazi maana uhalifu hauchagui. Ila hii chuki ya serikali na polisi dhidi ya wananchi wake haitatufikisha popote. Serikali kwa kuwa ina vyombo vya dola vyenye nguvu haitaki kumsikiliza mnyonge. Kila wakati ni vitisho tu! Msinijaribu, mimi sijaribiwi. mara, wasiingie barabarani tutawavunja miguu, n.k. Sasawatu wenye nguvu namna hiyo unategemea watahurumiwa na nani? Hiyo ni natural hate ambayo jeshi la polisi na serikali wanaitengeneza wenyewe, na ni "insanity" kutegemea matokeo ya tofauti.
 
Back
Top Bottom