Mahojiano na aliyenusurika katika shambulio lililoua askari wanne

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,974
Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba anasema tukio limeondoa maisha ya askari wanne na kujeruhi raia wawili.

Majeruhi mmoja anaitwa Ally Chionda ambaye ni mfanyabiashara wa duka la vifaa vya ujenzi karibu na benki ya CRDB ambayo pilisi wamepoteza maisha.

Anadai walikuja majambazi kwenye muda kama wa saa 1:15 usiku wakiwa na pikipiki kama tano na kila pikipiki ilikuwa na watu wawili.

Kulikuwa na watu sita au saba ambao walikuwa wamebeba bunduki.

Walipofika walianza kupiga risasi upande wa eneo la benki na upande wa duka lake.

Bahati mbaya risasi moja ilimpata kwenye mguu wa kushoto ikatokeza na kwenda tena kwenye mguu wa kulia.

Majeruhi anaendelea vizuri na anategemea kufanyiwa x-ray kwa uchunguzi zaidi.

VIDEO.

ANGALIZO:
Kuna baadhi ya watu wanaleta kejeli kuhusiana na tukio hili ambalo linasikitisha sana kwa watu wanaofahamu misingi ya kibinadamu.

Ni kweli binadamu tunatofautiana katika mitazamo lakini mizania ya kibinadamu huwa inapimwa wakati wa majonzi.

Hizo silaha walizopora inawezekana kesho zikatumika katika mwili wako au ndugu yako. Kama hujabahatika kutembelewa na majambazi huwezi kuelewa maana na uzito wa maneno yangu.

Tuombe uzima na Mungu awape faraja ndugu wa askari waliopoteza maisha wakiwa katika kazi ya kulinda maisha na mali za watanzania.
 
Siku zote tunajifunza kutokana na makosa.
Ni wakati wa jeshi la polisi kufanya kazi yake kwa weledi bila kuonekana kutumika na upande fulani dhidi ya upande mwingine.
Mazoezi ya hadharani ya siku mbili zilizopita yameonesha dhahiri jeshi la polisi lipo kwa ajili ya kupambana na upinzani. Hali hii inaleta uhasama kati ya polisi na upinzani ambao sio wachache kwa mujibu wa uchaguzi uliopita.

Kwa sasa ni vigumu mno kwa raia mwema kuweza kusaidia jeshi la polisi kwa sababu ni kama wameshatengeneza uhasama wa kudumu kutokana na kauli tata za viongozi zinazowasisitiza wananchi kuwaogopa polisi.
RIP polisi wetu. Mmetutangulia hata kabla ya 1 sept.
 
Tukio linasikitisha kweli, Mungu azilaze roho za waliofariki mahali pema!
Lakini nao polisi wafanye kazi zao kwa weledi, wakati wa maandamano imekuwa ni desturi polisi kuwapiga raia wasio kuwa na hatia na wasio na silaha, hii hali imechangia kwa kiasi kikubwa wananchi kujenga chuki dhidi yao!
Polisi waache kutumika kisiasa, tabia ya kuwakamata, kuwapiga na hata kuuwa watu wanaofanya yao kwa mujibu wa katiba ni fedheha na kukosekana kwa weledi!
 
Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba anasema tukio limeondoa maisha ya askari wanne.

Majeruhi anaitwa Ally Chionda ambaye ni mfanyabiashara wa duka la vifaa vya ujenzi karibu na benki ya CRDB ambayo pilisi wamepoteza maisha.

Anadai walikuja majambazi kwenye muda kama wa saa 1:15 usiku wakiwa na pikipiki kama tano na kila pikipiki ilikuwa na watu wawili.

Kulikuwa na watu sita au saba ambao walikuwa wamebeba bunduki.

Walipofika walianza kupiga risasi upande wa eneo la benki na upande wa duka lake.

Bahati mbaya risasi moja ilimpata kwenye mguu wa kushoto ikatokeza na kwenda tena kwenye mguu wa kulia.

Majeruhi anaendelea vizuri na anategemea kufanyiwa x-ray kwa uchunguzi zaidi.

VIDEO.

ANGALIZO:
Kuna baadhi ya watu wanaleta kejeli kuhusiana na tukio hili ambalo linasikitisha sana kwa watu wanaofahamu misingi ya kibinadamu.

Ni kweli binadamu tunatofautiana katika mitazamo lakini mizania ya kibinadamu huwa inapimwa wakati wa majonzi.

Hizo silaha walizopora inawezekana kesho zikatumika katika mwili wako au ndugu yako.

Tuombe uzima na Mungu awape faraja ndugu wa askari waliopoteza maisha wakiwa katika kazi ya kulinda maisha na mali za watanzania.

Well said mkuu. Linapokuja suala la maisha/uhai ni kitu kisichohitaji masihara wala kejeli! Na ni kweli pia hiyo silaha kesho yaweza kukudhuru wewe au kama sio wewe ni ndugu jamaa au mtanzania mwingine yeyote ambae ni nguvu kazi!
 
Polisi wajikite zaidi katika kuzuia uhalifu kabla haujatokea,wajishughulishe na mambo makubwa ,wazingatie zaidi kanuni na taratibu za kazi zao .
Tatizo wanajishughulisha na vitu vidogo vidogo kama kuzuia mikutano na maandamano hadi wanasahau majukumu yao ya msingi .
 
Hii kitu ni serious halafu watu wanafanya mzaha.
Siku si nyingi polisi walendesha zoezi la usajili wa silaha na hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa uwepo wa silaha zisizo rasmi kwenye mikono ya watu waovu.
Kitendi hiko cha mbagala kinaonyesha kuwa watu waovu wana njaa ya silaha kwa ajili ya mambo yao. Ndio maana baada ya kupora silaha wametokomea.
Maana yake ni kwamba silaha zilizo kwenye mikono isiyo rasmi zinaongezeka.
Na tutake au tusitake zitatumika katika matukio ya kihalifu humu humu nchini.
Hili suala haliwahusu polisi peke yao.
YATUPASA KUWA MAKINI SANA.
 
Nafikiri ni wakati sasa wa polisi kaweka vituo Vingi upande wa mbagala yaani ukanda huo wote hadi hadi maeneo ya kupita kisemvule kote jaza vituo, pia wafanye mpango wote wote ili kuondoa msongamano wa magari hapo stendi kuu ya mbagala, vibaka na mateja wamejaa sana hapo, InAuma polisi wetu kuendelea kuuuwawa, pole kwa jeshi LA polisi pole kwa familia za marehemu
 
Wapumzike kwa amani vijana wetu. Wameacha ndugu jamaa na familia zinazowapenda na kuwategemea sana
Kuna ongezeko kubwa la uhalifu siku za karibuni, lakini askari wetu wako kwenye mazoezi mazito tena yanayoonekana live mitaani (kitu ambacho nadhani sio sahihi)kuonyesha utayari na umahiri wao (wa kupambana na upinzani? Nisihukumu)
Jeshi la polisi linapaswa kujitambua na kujitafakari, askari wengi vijana ndio wameanza kazi jeshi la polisi, bado hawajawa na uzoefu kazini...mbaya zaidi wamekutana na adha ya mazoezi yenye kutesa na kuchosha mno...kwa ajili ya show off za ubabe usio na maana yoyote
Wanachoka mno ila hawana pa kusemea... wana changamoto za maisha ni binadamu wanahitaji kupumzika lakini wakubwa hawajui hilo
Wengi siku hizi utawakuta kwenye vituo vya polisi kwenye mageti ukiwaangalia unasoma kabisa sura za uchovu na kukata tamaa
Wana kazi zenye kukera kuhoji wanaoingia kituoni, kuwapigia salute wakubwa wote kila dakika wanapopita hapo, kutumwatumwa kila wakati kama wasichana wa kazi
Wahurumieni hawa vijana sisi tunaoongea nao tunajua wanachoka mno . wanafanya kazi kwa shift muda wa kuwa off Wapumzike wanatakiwa kwenye gwaride
Kwa jinsi hii hata wakivamiwa ni ngumu kujibu mashambulizi
 
Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba anasema tukio limeondoa maisha ya askari wanne.

Majeruhi anaitwa Ally Chionda ambaye ni mfanyabiashara wa duka la vifaa vya ujenzi karibu na benki ya CRDB ambayo pilisi wamepoteza maisha.

Anadai walikuja majambazi kwenye muda kama wa saa 1:15 usiku wakiwa na pikipiki kama tano na kila pikipiki ilikuwa na watu wawili.

Kulikuwa na watu sita au saba ambao walikuwa wamebeba bunduki.

Walipofika walianza kupiga risasi upande wa eneo la benki na upande wa duka lake.

Bahati mbaya risasi moja ilimpata kwenye mguu wa kushoto ikatokeza na kwenda tena kwenye mguu wa kulia.

Majeruhi anaendelea vizuri na anategemea kufanyiwa x-ray kwa uchunguzi zaidi.

VIDEO.

ANGALIZO:
Kuna baadhi ya watu wanaleta kejeli kuhusiana na tukio hili ambalo linasikitisha sana kwa watu wanaofahamu misingi ya kibinadamu.

Ni kweli binadamu tunatofautiana katika mitazamo lakini mizania ya kibinadamu huwa inapimwa wakati wa majonzi.

Hizo silaha walizopora inawezekana kesho zikatumika katika mwili wako au ndugu yako.

Tuombe uzima na Mungu awape faraja ndugu wa askari waliopoteza maisha wakiwa katika kazi ya kulinda maisha na mali za watanzania.

Shukran kwa taarifa hii na kauli nzuri za maelekezo. Inasikitisha kuona mwanadamu anamkasifu mlinda usalama badala ya kulaani majambazi. Wao ni walinda usalama popote pale hata ktk mikutano hiyo kwakuwa haijaruhusiwa kutokana na sababu za kiusalama kwakuwa kauli nyingi zinaashiria uvunjifu wa amani na kuingilia kati utendaji Serikalini. Hiyo mikutano si ifanyike kule ilikoruhusiwa?
 
Pole kwa waliofiwa lkn police wajipange hasa katika vituo na malindo yaliyo nje.tufocus katika kuchangia hiko na tusiingize suala la namna gani wao wanavyojiandaa kuzuia mikutano ya tar moja kwa kuonya ,kupiga ,kuua au kukamata watu siku hiyo.hapa ni mbagala CRDB nn kifanyike kuondoa matukio haya ?
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba anasema tukio limeondoa maisha ya askari wanne.

Majeruhi anaitwa Ally Chionda ambaye ni mfanyabiashara wa duka la vifaa vya ujenzi karibu na benki ya CRDB ambayo pilisi wamepoteza maisha.

Anadai walikuja majambazi kwenye muda kama wa saa 1:15 usiku wakiwa na pikipiki kama tano na kila pikipiki ilikuwa na watu wawili.

Kulikuwa na watu sita au saba ambao walikuwa wamebeba bunduki.

Walipofika walianza kupiga risasi upande wa eneo la benki na upande wa duka lake.

Bahati mbaya risasi moja ilimpata kwenye mguu wa kushoto ikatokeza na kwenda tena kwenye mguu wa kulia.

Majeruhi anaendelea vizuri na anategemea kufanyiwa x-ray kwa uchunguzi zaidi.

VIDEO.

ANGALIZO:
Kuna baadhi ya watu wanaleta kejeli kuhusiana na tukio hili ambalo linasikitisha sana kwa watu wanaofahamu misingi ya kibinadamu.

Ni kweli binadamu tunatofautiana katika mitazamo lakini mizania ya kibinadamu huwa inapimwa wakati wa majonzi.

Hizo silaha walizopora inawezekana kesho zikatumika katika mwili wako au ndugu yako.

Tuombe uzima na Mungu awape faraja ndugu wa askari waliopoteza maisha wakiwa katika kazi ya kulinda maisha na mali za watanzania.

Kwanza niwape pole sana Polisi na familia za askari waliouawa. Pili polisi lazima wafahamu kuwa kuna tatizo sana la askari kulinda usalama wa raia, walijisahau sana ikafika mahali mpaka majambazi yakaona uwezekano wa kupambana na polisi. Naweza kusema wamewalea sana wezi na majambazi. Sikuwa nafahamu kama jeshi la polisi lina vyombo imara na madhubuti vya kulinda usalama wa raia, hizi siku mbili wametuonesha wanazo nguvu, sasa nachoshindwa kuelewa inakuwaje majambazi yatende haya yote na hata kujiaminisha kwenda kwenye makao ya polisi (ref staki shari incident) na kufanya ualifu? Mh Mwiguli naamini Uwezo unao wa kubadili hii dhana ya majambazi kwenye ardhi ya Tanzania. Kuweni makini na achene masihara na wezi na majambazi, ifike mahali kila mtu anayeona alternative ya maisha ni kuiba aogope. Nchi zingine mbona zimeweza? wakikukamata tu ndio mwisho wako. Lkn sisi tumezoea kuona majambazi yanapelekwa polisi na kurudi, kufanya masihala na waalifu sio jambo jema.
 
Pole kwa waliofiwa lkn police wajipange hasa katika vituo na malindo yaliyo nje.tufocus katika kuchangia hiko na tusiingize suala la namna gani wao wanavyojiandaa kuzuia mikutano ya tar moja kwa kuonya ,kupiga ,kuua au kukamata watu siku hiyo.hapa ni mbagala CRDB nn kifanyike kuondoa matukio haya ?
Ni kuachana na siasa za kuonea wapinzani na kujikita kwenye maswala ya kuisalama kama haya.
 
Lameck kupose kwenye vyombo vya habari huku umevaa uso wa simanzi ya kutengeneza na kuongea kwa tuo huku ukiwa kwenye mavazi rasmi ya jeshi la polisi haitoshi kabisa
Achana na ambitions, hebu mtafute Mrema akuambie yeye alifanyaje utu uzima dawa you can learn something crucial from them . ukiwa mwerevu unaweza kuleta mapinduzi makubwa sana kwenye jeshi la polisi
Ila ukibaki na hiyo hulka yako utavaa nyuso nyingi za simanzi kabla hujatoka hapo
 
25 Reactions
Reply
Back
Top Bottom