Mahita ajitosa ubunge Moro

Tatizo letu tunafikiri kwenda bungeni ni kupato manufaa ya bure. Mahita hafai hata kidogo kuwa mbunge kama mwakilishi mkereketwa wa wana morogoro. Ushauri wangu kwa wana Morogoro msikubali kudanganyika!!!!
 
Duh kweli kazi ipo sasa hivi, Mara Tibaigana naye huko Kagera anataka kugombea sisi Watanzania tunawaza politics tu
 
Mahita amekuwa rafiki sana wa majambazi wa kutumia silaha wakati akiwa IGP sijui hana hata aibu? Hivi CCM

KWANI HUJUI CCM CHAMA CHA MAJAMBAZI
 
Hivi hawa maofisa wastafu wa majeshi na polisi wana kadi za CCM?? hivi wakiwa madarakani ni Wanachama wa chama kipi??
 
Kwa hiyo una m support? Na unaandika kabisa "anajaribu bahati yake" unamaana unaamini uwakilishi wa watu uende kwa kufuatana na bahati?

Attitudes kama hizi ndizo zinatupa viongozi tulionao, halafu wakiboronga tutalalamika?

Kwani wewe hujui kama kuukwaa Ubunge ni kubahatika life kwa hapa kwetu? Hata Zombe unaweza kusikia kagombea ubunge jimbo fulani akifikiri watu hawajui aliyoyatenda. TZ inawezekana tu. Si kila mtu tu anafanya atakavyo lakini bdae tunaona eti nae ni mmoja wa watunga sheria wetu? Mtu ashakua IGP sasa ubunge tena anataka yeye...kwa ticket ya chama tawala! Inamaana huyu kwenye chama kaingia lini? Kuna haja ya kuwafanyia screening hawa wanaojiita watumishi wa serikali kuu ambao eti hawapaswi kua na ushabiki wa vyama. How can we believe such a person? I'm curious! may be this person was a ccm affiliate and has done them favours kipindi yupo kazini ndio maana wanataka kumlipa fadhila kwa yale aliyofanya. Hapo the map is: kuukwaa ubunge then waziri wa mambo ya Ndani. Huoni kama ni bahati hiyo? Do you think it is that easy ???
 
Mahita huyu askari polisi mkakamavu kuwasikiliza na kuwawakilisha wananchi itakuwa burudani. Well, wananchi wa Morogoro wanamjua zaidi na wataamua. Ila style za kubadili ngangari kuwa ngunguri itabidi aziangalie mara mbili mbili
 
anataka kugombania ubunge ameshindwa mtoto aliekamua kiunoni mwake huku jasho likimtoka???

Hahahaa duh watu wabaya kweli...nimecheka mno! Kweli huyu hatufai kama anaweza kukana jasho na damu yake mwenyewe atawezaje kutetea jasho na damu za wengine?
 
mahita akata rufaa...akidai mtoto sio wake....huyu anakataa mtoto aliyerandana nae je atawakubali watz asiowajua kweli.....hizi siasa jamani hawa ndio wazee ambao jk anasema tuwaache wapumzike wanatafuta nini.....halafu uadilifu wake mdogo sana
 
Mahita kwani anataka nini jamani kama umaarufu anao...kama kiburi anacho kama dharau anayo kama kiinua mgongo akancho anataka nini??alisahau ??
 
Ndio maana hawa watuwakiwa madarakani wanashindwa kutumikia nyadhifa zao itakiwavyo kwanisheria haiwaruhusu kuwa wanachamawa chama chochote. Je aliingia lini CCM au hakurudisha kadi ? Pili, nilishakaa Morogoro wakati uchaguzi ulipofanyika na Mahita alileta shida mojakwa kusema Morogoro inatawaliwa na watu ambao sio wazawa na alisababisha kasheshe kwa CCM kwani alikuwa na watu wake kwenye Udiwani pia hata Ubunge lakini katika Ubunge walipigwa chini kura za maoni pia katika kinyanyanyiro cha Umeya pia huyo mgombea wa Mahita akashindwa ndio Profesa Ishengoma akashinda, kwa bahati mbaya huyo mgombea wa Mahita nimemsahau jina ila kwa Morogoro watu wengi wanajua na pia nitafanya followup nilipate hiloj ina
 
Mahita kwani anataka nini jamani kama umaarufu anao...kama kiburi anacho kama dharau anayo kama kiinua mgongo akancho anataka nini??alisahau ??

Wewe hujui uroho wa madaraka walionao wabongo? Subiri 2010 haiko mbali,utaona mengi!
 
Nasema mwacheni kaka yangu ngunguri agombee nyumbani kwao, prof. Aende kwao naye akagombee.

Gerhad schroder ana rekodi pevu kula ngozi kwenda mbele lakini aliukwaa u kansela pale kwa mzee adolph iwe bob ommy?!!!!

Wacheni majungu bwana, acha akapambane kwenye ulingo wa siasa, maana kama saluti keshawachapia sana politicians sasa na yeye naye ausake uheshimiwa.

Nasema 2010 wakuu.... Kazi kwelikweriiiiiiiiii
 
I beg to differ,

Kukataa mtoto ni irresponsibility ya hali ya juu ambayo mwanadamu anaweza kuifanya.Hata baadhi ya wanyama wanaosemwa kutokuwa na akili kama binadamu wanajua kutunza watoto. Waswahili wanasema damu nzito kuliko maji, sasa huyu aliyeshindwa kuitunza damu (mtoto wake mwenyewe) ataweza kuwaenzi watu baki (maji) ?

Fikra kama hizi za "kukataa mtoto na uongozi ni vitu tofauti" ndizo zinatupa viongozi kama kina Pinda na Kikwete.

Kama mtu hana discipline kiasi cha kufanya rape (mahakama iangalie kama anaweza kushtakiwa kwa statutory rape) tena kwa mfanyakazi wake wa ndani, unafikiri akipata nafasi ya kuwa rape wananchi wa Morogoro katika ufisadi atakuwa na discipline ya ku resist?

Sija question kama anaweza au hawezi kugombea, certainly this is a straight provision of his civil rights.What I am questioning is his ability to lead.These are two different things and should not be confused as one.
You are damn right! Huyu jamaa hafai hata kuwa balozi wa nyumba kumi, the best person ni yule ambaye familia yake iko salama sasa huyu mtu anaweza kutembea na house girl..(shame) above all anakataa kutunza mtoto uhuni kh! wapi tunaenda wandugu.
 
watru kama akina mahita jk ametushauri watz tuwaache wapumzike kwani wamekula vya kutosha.....sasa huyu mzee anataka nini zaidi? Wana moro kazi kwenu.....
 
Mahita kwani anataka nini jamani kama umaarufu anao...kama kiburi anacho kama dharau anayo kama kiinua mgongo akancho anataka nini??alisahau ??
Anataka kuwarudi wabunge ngangari maana yeye ni ngunguri.Halafu baada ya ubunge njia ni kuwa waziri.Imagine! Mahita the minister!Duuh.
 
kama ndo hivo mtu unaamka tu na kuamua ...lol na mie naombeni nafasi ya ubunge
la tutaendelea kulalamika kila siku tunapata makapi

Imagine unampa mahita ubunge what iz next???
 
Jamani hii inawezekana ikawa ni kichekesho kama kweli nimesikia jamaa anataka kugombania ubunge ameshindwa mtoto aliekamua kiunoni mwake huku jasho likimtoka ataweza wana morogoro zaiidi laki kadhaa???

watu wa morogoro hamnazo samahani kwa kutumia lugha hiyo hata akija mzungu wanaweza mpa ubunge.Fikiria wamempa mhindi mmoja lotto ambaye alimpiga kofi mfanyakazi wa maji safi na maji taka,wamempa mwarabu mwingine aitwae sadiki,wamempa mtu mwarabu mwingine anayeitwa shabibi yaani hakuna hata uzalendo ni uhuni mtupu kwa hiyo na yeye anaweza pata hakuna cha maana huku chukua chako nenda mbele
 
Si anajua akidanganya kwa khanga, t-shirt, kitenge, chumvi na pombe watu watahadahika na kumpa ubunge, si unajua sisis wadanganyika tulivyo?
 
Kukataa mtoto na ubunge ni vitu viwiwli visivyo na uhuhusiano kabisa.kama mtanzania na katiba inamruhusu atumie nafasi hiyo.
kweli wenye visa watu.

Yani hapa you are very wrong.Kama ameshindwa kuonyesha upendo kwa mtoto wake 1 ,atawezaje kuwapenda hao wananchi wa jimbo lake? ukiwa mwaminifu katika madogo utakuwa mwaminifu katika makubwa pia.Kama ufisadi kaanza kwa familia yake basi hafai kuwa kiongozi.
 
Back
Top Bottom