WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
Kukataa mtoto na ubunge ni vitu viwiwli visivyo na uhuhusiano kabisa.kama mtanzania na katiba inamruhusu atumie nafasi hiyo.
kweli wenye visa watu.
R U SURE MKUU?
Kwa uelewa wako unadhani kutafuta ubunge ni ile iweje? Ubunge ni uwakilishi wa watu wa jimbo lako - kwa maneno mengine mbunge ni mwakilishi na mtetezi wa watu kupata haki na stahili zao.Mahita alipokataa mtoto maana yake ni sawasawa na kushindwa kutekeleza kile anachotegemewa kukifanya kwa magnitude kubwa zaidi akiwa mbunge.Kama anashindwa kumtetea mtoto mmoja tena damu yake, ataweza wapi kuwatetea maelefu tena asiokuwa na nasaba nao?Labda utuambie kuwa unaamini ubunge ni kumpa mtu fursa kwenda kujitetea maslahi yake yeye binafsi.Kama ndivyo basi kagonga mwamba maana zama hizi watu wanajua haki zao.
Ushauri wa bure - kama ni ndugu yako basi mshauri aachane na hiki kipute ataaibishwa bure maana agenda yake ni irrelevant na point ya kummaliza ni ndogo sana.Na sasa ajue wanaharakati wa haki za binadamu wako macho - achilia mbali PCCB wanaoangalia rushwa kwenye uchaguzi.Kama ni vijisenti vinamsumbua basi amtunze mwanae aliyezaa namjakazi wake atapata sifa zaidi kuliko kujitosa kwenye kinayang'anyiro 2010.