Mahari bei gani

Varbo

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
1,117
856
Wana Jamii Forum naomba kuwasilisha hapa mbele ya jukwaa hili
Nina mpenzi wangu kamaliza chuo now nataka nioe kabisa!! Tukiwa katika maongezi ya kawaida tu nikamdokezea
Hivi mahari yako ni kiasi gani mchumba wangu kaniambia millioni nne!!Kiukweli na mpenda sana lkn naona hio pesa nyingi japo uwezo wa kuitoa nianao Je Ndio mahari za siku hizi zilivo? Naomba ushauri wenu wana JF
 
Yeye alinigusia wazazi wake ndio wanapanga hivo
 
Sasa uwezo unao, tatizo ni nini?

Punguzeni ubahili. Princess wa Spain aliutoa mji mzima wa Bombay kwa Mfalme wa Uingereza kama mahari, itakuwa milioni nne hata gari hununui!
 
4m mmmmmmh! Hapo napata Tuk Tuk mbili afu nakula buku 20 daily.. Kwa wiki 140000.. Kwa mwezi 560000.. Stress za nn!!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
ni pm nikupe msaada wa mahari lakini uje na huyo mchumba wako
 
unaonekana umepata mawazo? Pole

kama huna hizo pesa mwambie kabisa wapunguze ili wewe uweze kum-afford lol

ni nyingi ila sio mbaya sana, ni kama ng'ombe 30 tu.
 
Hivi watu wanatoaga mahari hadi leo eeh? Kumbe kuzaa mabinti ni kabiashara kazuri. Jilipue baba, nakushauri utafute mtu mzima wa kabila lake akupe picha ya pa kuanzia.
 
Mpige chini avimbe juu, hatakudai tena milioni nne.....staili mpya hii nakupa......(ni-pm nikupe ushauri wa ksheria)
 
Hivi watu wanatoaga mahari hadi leo eeh? Kumbe kuzaa mabinti ni kabiashara kazuri. Jilipue baba, nakushauri utafute mtu mzima wa kabila lake akupe picha ya pa kuanzia.

Mahari mpaka kiama kitasimama yatakuwepo tu.

Kwa wengine mahari ni zawadi ya biharusi, kwa hiyo wazazi hawana chao.
 
inaweza kuwa hivyo.

Bei ya ng'ombe wa mahari huwa sio kama anavyouzwa sokoni, anakuwa na bei ya chini zaidi.

Hii huwa naona tunavyobargain wakati wa mahari.

Sasa hapa kama ng'ombe sokoni ni laki mbili kwa msimu huu wa kiangazi, basi ng'ombe wa mahari anaweza thamanishwa kati ya 125,000 hadi 150,000.

kumbe ng'ombe 30 ni milioni 4 tu! :(
 
inaweza kuwa hivyo.

Bei ya ng'ombe wa mahari huwa sio kama anavyouzwa sokoni, anakuwa na bei ya chini zaidi.

Hii huwa naona tunavyobargain wakati wa mahari.

Sasa hapa kama ng'ombe sokoni ni laki mbili kwa msimu huu wa kiangazi, basi ng'ombe wa mahari anaweza thamanishwa kati ya 125,000 hadi 150,000.

Mmmmh ni hivyo eee? Maana niliona humu JF ng'ombe wa kisasa wa maziwa kila mmoja anauzwa 950,000 na kuendelea hadi 1,350,000. Sasa hii ya milioni nne kupata ng'ombe 30 imenishtua na kunishangaza sana.

Hebu nieleweshe mnavyo bargain wakati wa mahari inakuwaje? Mnakuwa mna bargain ng'ombe au thamani yake?
 
Mahari inapaswa kubakia kama symbol ya heshima ya kumchukua binti wa wenyewe. Na sio biashara! Umuhimu ni kwenye kujuana pande mbili na kujenga upendo.

Ukishalipiwa mahari 4M, unasubiria mume aendelee kukuletea perfumes na gari kama zawadi nyingine? Ndo maana hamuishi kunyanyaswa! Babangu akitaka 4M ya mahari nitamlipa mie mwanae, afu ataniskia bombani!
Mahari mpaka kiama kitasimama yatakuwepo tu.

Kwa wengine mahari ni zawadi ya biharusi, kwa hiyo wazazi hawana chao.
 
Hahaha!
Binti anauzwa kwa bei ya sokoni?
Inabidi muangalie stock market that morning?
Aisee! Kwetu unaweza ambiwa ng'ombe 10 lakini kila mmoja kwa bei ya tshs 1000 tu!

Back
Top Bottom