Kumbukizi: Naoa next month, naomba usikose kufika harusini

Just Nana

JF-Expert Member
Jul 27, 2023
500
1,001
Ni miaka mingi imepita, nipo na kumbukizi nyingi, lakini hii naona inafaa kuingia top ten....nisiwachoshe sana twende kazi.

Nakumbuka ilikua jumamosi, mi sio mtu wa kutoka kabisa, week end ni movie ,kula na kulala . maisha ya chuo kwa week end hua panakua na utulivu kiasi , watu wanakua wametawanyika wanapopajua, wale wazee wa kulala, ndio mida yetu sasa ya kujidai...kuitumia vizuri accommodation fee .

Nipo bize na kausingizi kangu , kuna raia alikua anagonga mlango, anagonga kwa fujo kama ugomvi yaani, daaah sio poa...ikabidi niamke tu maana hakua na dalili ya kusepa , na mimi nisingeweza kuendelea kufaidi rasmali za chuo fresh na zile kelele , nikaamka nikafungua mlango.

Nikamkuta mkaka mrefu, mweusi, ana mwili kiasi, alikua katupia jezi ya Liverpool. Akanisalimia, nilikua nimenuna balaa, si unajua wenge la usingizi bhana. Akaniuliza jina la mdada silikumbuki, miaka imepita kidogo, nikamwambia hapa hamna huyo mtu, akawa kama haamini yaani Kama kapigwa tukio hivi, nikamuuliza vipi kaka, mi nataka kulala, akanambia ohh...sorry nitakua nimekosea block, nikamwambia poa ,nikarudi kuuchapa.

Baada ya kama wiki na zaidi nilikua cafe napata msosi, the same cafe walikua wanaonesha mechi za nje, sina hakika kwa sasa, one of my friends ni shabiki wa Man U, akafanyaga niipende Man U hadi leo, achana na yanayotusibu kwa sasa, enzi hizo ilikua noma balaa...tupo tunapata viepe vyetu , si nikamuona yule mjamaa alinivurugia usingizi wangu bhana anachek game..pale watoto wa kike walikua wakuhesabu sana, sina hakika kama tulifika hata watano, kwaio ilikua rahisi kutuspot.

Mara zikaja juice pale, tukamwambia muhudumu hatujaagiza kitu, akasema nimeambiwa na yule kaka pale nilete, kuangalia huo upande anatuonesha ndio aliokaa yule kaka msumbufu, Anitha ( sio jina halisi) akaniuliza unamfahamua, mi simfahamu ata, nikamwambia yaaap, jamaa fulani ivi msumbufu sana, akacheeeeka ....nikamsimulia jinsi memfahamu , akasema kama alitukatisha usingizi anafaa alipie, kunywa juice mwali wangu.

Anitha anajua jinsi nahusudu kalala hatari....tukatupia vitu pale nini huku tunachek game, off course tulishinda bhana, baada ya mda akaja kutupa hi...akanambia anaomba radhi kwa usumbufu maana nilikua mekasirika sana Ile siku, nikamwambia poa haina shida.

Story ziliendelea pale, nikaona wananichosha tu, kumbuka mi sio mtu wa ma outing, yaani nipo pale kwa ajili ya rafiki angu Anitha na mipira yake...na pia sio muongeaji kiivo...Story zikanoga kati ya Anitha na yule kaka Thoby ( sio jina halisi).
Thoby akatoa wazo tutoke twende kwa bar fulani ivi ipo kati kama unatoka chuo unaelekea town, alitaka atupongeze eti Man U imeshinda, vijana kwa kutumia fursa bhana...

Mi nikamwambia kua sitomudu naenda kulala, Thoby akamuuliza Anitha inamaana huyu mwenzio hana starehe nyingine zaidi ya kulala au,maana Ile siku alikua amelala, hapa mnachek game analalamika anasikia usingizi, nawaambia tutoke anasema anasinzia, mwambie asinifanyie ivyo jamani

Anitha mtu wa bata, atakua alishapiga hesabu zake akaona hapa sio pa kulaza dam ikabidi anivute nje kwanza, akamwambia Thoby ...shem usijali hili limeisha , ngoja niongee nae, nikatoa macho balaa, shem tena ...mbona kama sielewi, mambo yanaenda kasi balaa, Anitha Anitha doooh.

Anitha akapiga vocal pale nje, nikajikuta nishafika hapo kwa iyo bar, yaani mambo zilienda chaaap , wakanywa mi nikiwa napambana na usingizi wangu tuuu, sikumbuki ata tulirudi saa ngapi, ila kwa ushawishi wa Anitha lilizaliwa pendo moja mujarabu sana, Thoby was a nice guy, so loving so caring ...ila tu nilikua namkwaza ikifika mida ya kutoka, mi nataka nilale au nichek movie, ye anataka tutoke, ili asinikwaze wala nisimkwaze Anitha akashauri tukutane kati, kama wiki hii tunatoka, the next week tunabaki room tunalala.

Thoby alikua third year, kwaio akamaliza akatuacha chuo, mi na Anitha tulikua second year. Maisha baada ya Thoby kumaliza chuo daaah, hayakua rahisi sana, kuna vitu vilimiss kiasi, tukapambana nasi tukamaliza chuo, tukaingia uraiani, by then Thoby alikua anajitolea mahala na pia alikua anafanya biashara zake binafsi ambazo alianza tangu tupo chuo, wachaga na biashara daaah.

Alikua anaishi Mwanza, mi nipo dar...ila alipambana kila baada ya mda fulani lazma anione, kale kadistance hakakakuwahi kutupa shida kabisa, jamaa alipambania kombe balaa, Ni Ile relation ambayo unammiss mtu hadi unaisafirisha mwenyewe iende ikaliwe daaah...

Ukafika mda Thoby akapata stability kiuchumi, akanambia nahitaji nikuoe ma, naomba uongee na nyumbani, nataka kufahamu taratibu nije kwenu ,mechoka kuisafirisha ....hadi hapo sikua na mashaka kua Anitha angekua my maid of honor, yaani tulikua tunakaa tunakumbuka tunacheka sana, eti we fala bila mimi usingempata Thoby...ila kweli doooh.

Nikamwambia mama, nimepata mchumba anaitwa fulani, anataka kuja kujitambulisha na kufata utaratibu utakaozaa ndoa, amenambia niwaambie, bi mkubwa akaniuliza kabila gani? Nikamwambia mchaga....aiseee yule mwanamke alinyanyuka akaondoka sebuleni, Niko heeee kwani nimeongea tofauti au?

Familia iligawanyika sana, mzee ananipenda mnooo, alikua upande wangu, bi mkubwa na baadhi ya ndugu wa mama walikua na msimamo wao, hawataki niolewe na mchaga, hakuna sababu ya maana inayotolewa ila tu hawakutaka ndoa ifungwe. Mama alipata hadi presha akalazwa baada ya kuona kua mzee alikua anasimama na mimi, sikuona Kama ni sawa familia yangu inayoishi kwa upendo ivurugike kwa ajili ya ndoa, nilikubali yaishe...nikamuomba Thoby aje nimshirikishe maamuzi ya familia, haikua rahisi hata,sikumudu hata kumuangalia usoni.

Sikuwahi muona Thoby analia, Ile siku alilia mbele yangu, akanambia toto, hua anapenda kuniita toto maana ananambia niko na mambo za kitoto sana, nafikaje chuo hata reds sijawahi kunywa...Thoby akanambia toto nimeumia sana, naomba nikutanishe na mzee wako, maana nilimwambia mzee hana shida, bi mkubwa ndio changamoto.

Thoby ilibidi ampigie mjomba ake wanaelewana sana yupo Morogoro aje kuongea na mshua, nikaongea na mshua wangu nikamuomba anisaidie aonane na mjomba wa Thoby, sikujua Kama yule kaka alikua ana nia namna Ile, hakuacha tu mjomba amzungumzie, Thoby alifika pia akiwa na mjomba ake, kikao cha wanaume watatu kilikaa, Thoby alipambana kumshawishi mzee wangu ili aone ni jinsi gani ana nia na mimi....mzee anakiri kua , mwanangu ulipata mwanaume, ikapangwa siku ya kutoa posa na mahari pia, Thoby hakutaka kuchelewesha mambo.

Siku Ile ilifika, sitomudu kuisahau maana iliondoka na uhai wa mama angu mpendwa, alishindwa kuhimili kuona bintiye mpenzi tena wa kwanza akiolewa na mchaga, usiku baada ya mahari kutolewa, mama alipata sroke mbaya sana, tukamkimbiza hospitali, baada ya masaa matatu mama aliaga dunia...nakumbuka maneno machache aliyoongea mama kabla hajakata roho ambayo niliyasikia kwa taabu sana , alinambia umenidharau, utanikumbuka ....wachaga sio watu....

Tulimpumzisha mama makaburi ya kinondoni, maisha baada ya hapo hayakua rahisi, mzee hakua muongeaji sana, mara nyingi amekua mtu wa kujifungia ndani....Thoby alifika msibani na alitoa kampani kubwa sana, Anitha pia...nawashukuru kwa upendo wao kwangu, haikua rahisi...mzee akanambia maisha yako ni jukumu lako, ila usidharau maneno ya mama ako, najuta sikua na cha kufanya...wote ni watu muhimu sana, nilidhani nilikua sahihi kusikiliza furaha yako ...

Ilibidi niweke kikao na Thoby wangu tukubaliane kutokukubaliana, nikamwambia Thoby hata dunia iumbwe tena unabaki kua mwanaume muhimu sana,ahsante kwa upendo wako...sina budi nikuache uende....hata naye aliumia lakini hakua na amani kuoa mahala ambapo umekataliwa kiasi cha kusababisha mauti....niliachana na Thoby rasmi Ile siku na ilipigwa mechi moja ya farewell matata sana...kijana alijituma sana Ile siku kuliko siku zote, nadhani alitaka kuweka alama kua ukipata mwingine mama ,usije ukanisahau ....yaaas...sijamudu kumsahau hadi leo, yule kijana wa kichaga mwenye upendo uliotukuka...my Thobias.

Leo ni harusi yake ...ameamua kuoa binti wa kichaga, amenambia hakutaka tena kubaguliwa sababu ya kabila, leo hii mwanaume niliempenda sana anafunga ndoa, na amenisisitiza niwepo maana mimi ni mmoja wa watu wake muhimu...nipo saloon mda huu na my partner in crime Anitha, wakati wapambaji wakifanya yao nami napambana na kumbukizi yangu chungu....off course nitafika harusini na namtakia kila lenye kheri....

Wasalaam

Just Nana...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom