Mahari bei gani

Hapana,

Moja ya mila ni kwamba ukitaka kuoa mambo yote yanapitia kwa washenga.

Kikwelikweli kwa utamaduni wetu hata hutakiwi kumjua kwa sana personally mke mtarajiwa, kuna watu maalum kazi yao kumchunguza na ku negotiate mahari.

Sio siku hizi watu mshakaa, mshatiana mimba, mshazichoropoa (ashakum, ndo ukweli wenyewe), leo mnaenda kuulizana mahari?

Au binti hata litmus test ya Tantawi hawezi kupita hana hata haya anadai mahari na yeye!

La!

Hahaha hivi hao wanawake nyie wote mnawaona sawa? Kuna wanaofika kuolewa wala jimai haijapita na huyo mwanamme, full haya na utasema vigezo Tantawi kamuangalia yeye ndo akaweka.....asidai mahari kwa sababu gani?

Acheni kuwaweka wanawake wote kwenye chungu kimoja. Mshenga kabla ya kudaiwa mahari kaka wa binti atamuuliza binti iweje, binti atataja, kaka atawasilisha kwa mshenga. Simple as that.
 
Mahari si lazima uimalize, ulizia kabila lao mila zikoje.

Unaweza kutoa "kishikia mke" ukachukua mke wako, mahari iliyobakia ukaweka kwenye "college fund" ya wanenu.Nyingine utawafadhili wazee vitu vidogovidogo over the years ambayo itakuja kuwa zaidi ya mahari.

Pengine unatajiwa kupimwa uanaume wako na nia tu.

Kutishika kwa kitu kama bei wakati hujaanza ku bargain si biashara.

Yeah, biashara, maana ishakuwa biashara siku hizi.

Kweli aisee ila tatizo na hizi mila zetu siku ambayo umekuwa babu mke wako akifariki unaambiwa umalizie mahari kwanza ndi ukazike na wanakomaa kweli
 
Usawa huu hamna kuoa babake.

Oa usiogope Kiranga, hapo wanaweza kuanza 4 million mwisho wa siku wakafikia muafaka laki 8 na bado jamaa akatoa laki 4 na ndoa ikafanyika. Kwa familia zinazoelewa mahari ni utaratibu ambao umewekwa na mababu zetu wanakuwa wanaundeleza kama sehemu ya kukamilisha mila na desturi hata kama wahusika na wazazi wamekulia mjini
 
Last edited by a moderator:
Kweli aisee ila tatizo na hizi mila zetu siku ambayo umekuwa babu mke wako akifariki unaambiwa umalizie mahari kwanza ndi ukazike na wanakomaa kweli

Duuh,

Hii noma mazee, inabidi uwe mdogo tu hapo.

Hizi mila unaweza kukamilisha mahari, unataka kuchukua mke kuna kibabu kinatokea kinadai hakijapata usinga wake.

Inabidi kukohoa tu kama ndo ushakubali mila hizi.
 
Unaambiwa koti la babu na blankent la bibi na mila zingine ukijipendekeza na muoaji kuwepo eneo la tukio utapigwa fine unaambiwa mila zao anaetaka kuoa haruhusiwi kutia timu eneo la tukio, ndio hivyo lazima taratibu zifuatwe kama wazazi wanakomaa
 
Oa usiogope Kiranga, hapo wanaweza kuanza 4 million mwisho wa siku wakafikia muafaka laki 8 na bado jamaa akatoa laki 4 na ndoa ikafanyika. Kwa familia zinazoelewa mahari ni utaratibu ambao umewekwa na mababu zetu wanakuwa wanaundeleza kama sehemu ya kukamilisha mila na desturi hata kama wahusika na wazazi wamekulia mjini

Mie sababu yangu ya kutooa si hiyo milioni nne, mbona hiyo ni ada ya cuz mmoja kwenda chuo kwa mwaka tu?
 
inaweza kuwa hivyo.

Bei ya ng'ombe wa mahari huwa sio kama anavyouzwa sokoni, anakuwa na bei ya chini zaidi.

Hii huwa naona tunavyobargain wakati wa mahari.

Sasa hapa kama ng'ombe sokoni ni laki mbili kwa msimu huu wa kiangazi, basi ng'ombe wa mahari anaweza thamanishwa kati ya 125,000 hadi 150,000.
juzi juzi mdogo wangu kaolewa, tunaenda kupanga mahari, wazee wanasema ng'ombe 5 kila ng'ombe 100,000; mbuzi 10, kila mbuzi 20,000; mi nikabaki nashangaa tu....... tukawa tunakonyezana na mdogo wangu hapa tutaiskia kuku kwa 1,000.
 
Huwa kuna ng'ombe fedha na ng'ombe mnyama, ukiambiwa mnyama hapo maana yake unaangalia bei ya sokoni ya ng'ombe tena wanatakiwa wachague wenyewe lakini kama ng'ombe wa fedha unaweza kuambiwa ng'ombe mmoja alfu 80
 
Back
Top Bottom