Niambieni
JF-Expert Member
- Jul 20, 2011
- 625
- 170
Hapo ndipo usipoujuwa Uislam, kwanza kabisa, mwanamke akishakuwa na watoto tu, basi hata kama nyumba ni yako, unaondoka wewe, mpaka watoto wakuwe (balehe) au aolewe na mume mwingine. Kumbuka hilo.
Ya kuchuma pamoja Uislam umehimiza maandikiano ya mikataba yenu (hii ipo kwenye Qur'an) si kukubaliana tu kisha kudhulumiana, kila mmoja aandike mali zake na mkiwa partners kila mmoja apate haki yake akiwa hai na si mpaka mmoja afe - kumbuka hilo pia.
Urithi kwa Waislam ni kitu kingine na mali za kuchuma pamoja ni kitu kingine. Hapo ndipo mnapowadanganya wake zenu, kuwa tunachuma pamoja, katika Uislam kama mnachuma pamoja mgawane kama biashara nyingine yoyote ile mkiwa hai, kila mtu anachukuwa haki yake na kuifanyia apendacho akiwa hai. Si kungoja mmoja kafa mwengine akombe zote.
Unaona raha ya sharia hiyo?
Ni kweli ni nzuri. Kama ipo na inatambulika sasa mnataka nini? au mnataka bunge lijadili nini?