Mahakama kuu Zanzibar kufuta kesi ya mauaji ya Padri Mushi

5525

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
5,412
6,273
- Mahakama Kuu yampa nafasi ya mwisho DPP na akishindwa kukamilisha ushahidi kesi itafutwa

- Ikumbukwe mtuhumiwa alikamatwa kwa kufuata mchoro wa katuni uliochorwa na FBI

Na Khamis Amani

MWAKA mmoja, miezi minne na siku 19 zimepita tangu kuuawa kwa Padri Evaristus Gabriel Mushi na upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Mahakama Kuu ya Zanzibar, imetoa muda wa mwisho wa kuendelea na kesi hiyo.

Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu anayesikiliza kesi hiyo, alisema Oktoba 3, mwaka huu ataiondoa kesi hiyo mahakamani ikiwa upande wa mashtaka utashindwa kukamilisha upelelezi wake.

Uamuzi huo wa mahakama umekuja baada ya kesi hiyo inayomkabili Omar Mussa Makame (35) kukaa kwa muda mrefu bila ya kusikilizwa, huku upande wa mashtaka ukiomba muda zaidi wa kukamilisha upelelezi huo, ombi ambalo lilipingwa na upande wa utetezi.

Upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili wa kujitegemea Abdallah Juma ambaye aliiyambia mahakama kwamba wamechoshwa na nyimbo za mara kwa mara za upande wa mashtaka juu ya upelelezi wa kesi hiyo.

Wakili huyo alisema kila kesi hiyo inapoitwa mahakamani upande huo unadai kutokukamilika kwa upelelezi.

Alisema madai ya upande wa mashtaka ya kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika hayana msingi wowote, ikizingatia kesi hiyo ni ya muda mrefu.

Wakili Abdallah, aliiomba mahakama kumwachia huru mshtakiwa bila masharti yoyote. Pia, alisema upande wa mashtaka ukijipanga unaweza kuirudisha tena mahakamani kesi hiyo kwa mujibu wa taratibu za kisheria:

“Mheshimiwa Jaji…jinai haiozi wanaweza wakaileta tena mahakamani wakati wowote baada ya kujipanga…kuachiwa huru kwa mteja wangu haina maana kuuzuia upande wa mashtaka kutokuifungua tena kesi hii,” alisema Wakili Abdallah.

Naye, Wakili wa serikali, Abdallah Mgongo licha ya kukiri kwamba kesi hiyo ni ya muda mrefu aliiomba mahakama kuangalia uzito wa kesi hiyo, ili kuona haki inatendeka.

Alisema kuahirishwa kwa ajili ya kuendelea na upelelezi ni sababu ya msingi. Hivyo, aliiomba mahakama kupanga tarehe nyengine ya kutajwa ili kuendelea na upelelezi.

Alisema upande wa mashtaka una jukumu la kusimamia mwenendo wa kesi mahakamani na suala la upelelezi lipo chini ya mikono ya polisi kwa mujibu wa kifungu cha 74 (1) cha sheria za mwenendo wa kesi za jinai (CPA) namba 7/2004 sheria za Zanzibar:

“Ni kweli hili shtaka ni la muda mrefu kwa hesabu za haraka haraka limeahirishwa mara 22…hatuwezi kusema ni lini upelelezi wake utakamilika,” alisema Abdallah Mgongo.

Hoja hizo zilipingwa na Wakili wa utetezi ambaye alidai shtaka hilo halistahiki kuwepo mahakamani kutokana na upande wa mashtaka kushindwa kukiri lini upelelezi utakamilika.

Wakili Juma alisema madai ya upande wa mashtaka ni uthibitisho tosha kuwa kesi hiyo itaendelea kufikishwa mahakamani na kumpotezea muda mshtakiwa.

Baada ya kusikiliza hoja za pande mbili hizo, Jaji Omar Othman Makungu alikiri kuwa ni shitaka la muda mrefu lakini si busara kuondoshwa mahakamani kwa kushtukiza bali inapaswa kutolewa muda zaida kwa upande wa mashtaka ili kujipanga zaidi.

Jaji Mkuu, alitoa muda wa mwisho kwa upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo, na endapo hadi Oktoba 3, mwaka huu utashindwa kukamilisha ushahidi wake, ameahidi kuliondoa shauri hilo mahakamani.

Kesi hiyo ilifunguliwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo Aprili 5, mwaka jana na mshitakiwa huyo alisomewa shtaka la kuua kwa makusudi kinyume na vifungu vya 196 na 197 vya kanuni ya adhabu sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar.

Siku hiyo mshitakiwa huyo akiwa mbele ya Mrajis wa Mahakama Kuu, George Joseph Kazi, alidaiwa kumuua kwa makusudi Padri Evaristus Mushi.

Tukio hilo la mauaji lilitokea saa 12:50 asubuhi, Februari 17, mwaka jana 2013 Beit Ras, nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Na Salma said / 06/09/2014
 
Kama Uamsho wameshadhibitiwa kesi ifutwe tu.
Wafu hafufuki na wala haki haimfuati kaburini.

FBI watamchoraje mtu kwa hadithi eti wanamkamata mtu?

Ni sawa na kujidai kujua sura ya Yesu kwa picha ya kubuni
 
Mnapenda kumtaja yesu wetu..... Nahisi na nyinyi mmekili kuwa no mwana wa mungu..... Mana alfanya maajabu ya kufa na kufufuka bas kushangaa mnaona aibu.... Shangaen yule n mwana was mungu.
 
Back
Top Bottom