Kilimanjaro: Padri Soka aliyedaiwa kubaka Watoto ashinda kesi 3 za Ubakaji, sasa yupo huru rasmi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Padri Sosthenes Soka (42) wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi, sasa yuko huru, baada ya kupangua kesi zote tatu za ubakaji zilizokuwa zikimkabili mbele ya mahakimu watatu tofauti katika Mahakama ya Hakimu Mkazi na Wilaya ya Moshi.

Hii ni baada ya kuachiwa huru leo Septemba 29, 2023 katika kesi ya jinai namba 349 ya mwaka 2022 kati ya kesi tatu za ubakaji zilizokuwa zikimkabili ambapo alikuwa akishtakiwa kwa kosa la ubakaji wa mtoto mwenye umri wa miaka 13, katika kanisa alilokuwa akihudumu.

Padri Soka ambaye alikuwa akitoa huduma katika Parokia teule ya Mtakatifu Dionis Aropagita ya Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi, alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza, Septemba 26, 2022 na kufunguliwa kesi tatu tofauti za kubaka watoto watatu zilizosomwa kwa mahakimu watatu tofauti.

Katika kesi ya kwanza ya jinai namba 44 ya mwaka 2022 iliyokuwa ikisikilizwa na hakimu mkazi Jenipha Edward, Mahakama ilimuachia huru Septemba 22, mwaka huu baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha shtaka la ubakaji na ulawiti wa mtoto wa miaka 12 lililokuwa likimkabili.

Septemba 25, mahakama hiyo pia ilimuachia huru Padri Soka katika kesi ya jinai namba 45 ya mwaka 2022 ya ubakaji wa mtoto mwenye umri wa miaka 12, ambayo ilikuwa ikisikilizwa na Hakimu mkazi mwandamizi wa Mahakama hiyo, Herieth Mhenga.

Kama ilivyokuwa katika kesi namba 44 na 45 za mwaka 2022, ndivyo imekuwa katika kesi namba 349 ambapo Padri Soka ameachiwa huru leo Septemba 29 baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha shtaka kwa viwango ambavyo sheria inataka.

Katika hukumu hiyo ambayo imetolewa leo Septemba 29 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Moshi, Erasto Philly aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, alielezwa kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha shtaka kwa kiwango ambacho sheria inataka na kwamba kulikuwa na utofauti mkubwa kati ya shahidi na shahidi na hati ya mashtaka.

Mbali na kutofautiana kwa maelezo yaliyotolewa na mashahidi wa upande wa mashitaka ilielezwa sababu nyingine za kuachiwa huru kwa padri huyo ni kuwa kesi hiyo upelelezi wake haukufanywa kwani kulitofautiana kati ya hati ya mashtaka iliyoeleza mtoto alifanyiwa tukio hilo siku moja huku maelezo ya mtoto yakionyesha alifanyiwa tukio hilo zaidi ya mara moja.

Akielezea hukumu hiyo, wakili wa upande wa utetezi, Edwin Silayo alieleza kuwa baada ya mahakama kufuatilia mwenendo wa kesi pamoja na kusikiliza mashahidi wa pande zote upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha tuhuma zilizokuwa zikimkabili padri huyo.

Alidai baada ya upande wa mahakama kupitia maelezo ya pande zote mbili kulikuwa na mashaka mengi upande wa mashtaka na hivyo mahakama ikaweza kuthibitisha kuwa Padri Soka hakuwa na hatia katika kesi hiyo.

"Leo ilikuwa ni hukumu kati ya kesi tatu zilizokuwa zikimkabili Padri Soka, Mahakama baada ya kufuatilia mwenendo wa kesi na yote yaliyojiri na kusikiliza mashahidi wa pande zote wamekuta hana hatia kwa kuwa upande wa mashtaka walishindwa kuthibitisha kesi hii," amesema.

"Leo hii tunashangalia na tunafuraha kubwa kwa kuwa mahakama imeweza kuthibitisha katika kesi zote kwamba Padre Soka hakuhusika kwa namna yoyote katika tuhuma ambazo zilikuwa zikimkabili," amesema.
 
1. Ni keli hakubaka? au legal technicalities zimemtoa?

UKWELI ANAUJUA MUNGU NA NAFSI YAKE PADRE
 
Kwa hizi "Sorry" kibao zinazotolewa na Vatican Kuna asilimia 120 huyu mbuzi kazibua watoto(na mostly huwa ni alter boys)Mi nashauri Hawa watu wapimwe Akili kabla ya kukabidhiwa kanisa,au waoe tu au ikishindikana wahasiwe,Kwa sababu sijaona kwann wanahitaji nguvu za kiume kama wanavitumia tu kukojolea
 
Back
Top Bottom