sajo
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 3,034
- 5,268
Leo tarehe 28.01.2022 Mahakama Kuu ya Tanzania chini ya majaji watatu wakiongozwa na Jaji Mgeta, imetupilia mbali kesi ya kikatiba Na 2 ya 2022 iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi, Francis Mbatia dhidi ya aliyekuwa Spika wa bunge, Job Ndugai.
Mahakama imeeleza kuwa kesi hiyo haina mashiko kwa kuwa hakuna ukiukwaji wa Katiba uliofanywa. Mahakama imetambua barua iliyotolewa mahakamani na Wakili mkuu wa Serikali kuonesha kuwa Ndugai aliandika barua ya kujiuzulu kwenda kwa Katibu wa Bunge na nakala kwa Katibu Mkuu wa CCM ni halali na hivyo alifuata taratibu zote.
Nakala ya barua iliyotambuliwa na Mahakama ni hii hapa.
Pia soma
- James Mbatia amkingia kifua Spika Ndugai, kwenda mahakamani kuzuia mchakato wa kutafuta Spika mpya (07/01/2022)
- Ndugai amefuata utaratibu wa kujiuzulu Uspika kwa mujibu wa Katiba. Mbatia hayupo sahihi na kesi yake haina mashiko (08/01/2022)
- Kutoka Mahakama Kuu: Kesi ya James Mbatia kupinga mchakato wa Job Ndugai kujiuzulu Uspika (27/01/2022)