Mahakama Kisutu yapiga stop mkutano wa Yanga wa Oktoba 23, 2016

Wonderful

JF-Expert Member
Apr 8, 2015
7,348
5,977
Mkutano Mkuu wa Yanga uliokuwa umepangwa kufanyika kesho Jumapili, Oktoba 23, 2016 unadaiwa kuota mbawa baada ya Mahakama kuupiga ‘stop’ kufuatia kesi iliyofunguliwa na baadhi ya wanachama kupinga mkutano huo wa dharura unaodaiwa kukiuka taratibu na uhalali wa siku za uitishwaji wake.

Mmoja wa wanachama hao ni Frank Chacha ambaye amethibitisha kufungua kesi hiyo, akizungumza kupitia ktuo kimoja cha redio nchini, amesema mkutano wa kwanza ulikuwa una makosa na mkutano wa pili pia umeitishwa kwa makosa na huku mkataba ukiwa umeshasainiwa na wakati huu sio wa kwenda kuujadili.

“Ni Kweli mkutano ulikuwa umepangwa kufanyika tarehe Oktoba 23, 2016 ambapo agenda zaidi ya 13 zingepaswa kujadiliwa lakini tumeiomba mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa amri ya kuahirisha huo mkutano.

Ombi hili lilitolewa kupitia kesi namba 293 (2016) kesi ndogo namba 214 (2016) kati ya Frank Chacha muombaji wa kwanza na Magoma mwombaji wa pili huku walalamikiwa wakiwa ni Bodi ya Udhamini ya klabu ya Yanga na kampuni ya Yanga Yetu.”

“Katika maombi yetu ya dharura tuliomba mambo yafuatayo, Mkutano wa Oktoba 23, uzuiliwe kwasababu ni mkutano batili ambao haujafata taratibu za kisheria kwasababu notisi imekuja nje ya utaratibu pia makabrasha yalitakiwa yatolewe siku saba kabla ya mkutano kitu ambacho hakijafanyika,” ameongeza Chacha.

Ameongeza kuwa maombi mengine ni kusitishwa kwa utekelezaji wa mkataba kati ya Yanga Yetu na Bodi ya wadhamini uliosainiwa mnamo Oktoba 3, 2016.

Hatimaye Mahakama hiyo mbele ya Mheshimiwa Mwambapa, ikatoa amri ya kuzuia mara moja mkutano huo usifanyike na tayari tumeshaipa taarifa Bodi ya Wadhamini na Klabu ya Yanga kuwa mkutano huo usifanyike na mabango mengine kuhusiana na order hiyo tayari yameshabandikwa kwenye uwanja wa Kaunda.
IMG-20161021-WA0028.jpg
IMG-20161021-WA0030.jpg
 
Mmh tunarud kulee kwenye yanga asili na yanga kampun...
Ila naona kama manji alitaka kuwakurupua tu yanga japokua ana malengo mazur...
 
Tunashukuru kama ni kweli. Huyu mkodishaji anataka apige dili gani kupitia yanga. Ndugu wanayanga kuifunga simba sio mafanikio Bali ni wajibu wa yanga na kiongozi yeyote wa yanga analitambua hill.
Yanga daima mbele.
 
Naanza kuona harufu ya migogoro yanga....labda Ule usemi " kwenye udhia penyeza rupia" unaweza kuinusulu
 
Kwani bangachori hawezi ijengea yanga uwanja mpaka aikodi?
aijengee Yanga uwanja ili iweje? umesikia wapi kuwa Barrick Gold / Acacia wanachimba dhahabu wanaiacha Tanzania? au gesi ya Mtwara inatolewa bure kuzalisha umeme wa Tanesco??
 
Wanayanga wenzangu njoo muone mbagala kuu huyo ni diwani wetu alikuja na mipango kibao yote hewa ametelekeza kata yake toka uchaguzi hajawahi kukanyaga ardhi ya Mbagala kuu tuwe makini nae wapanga sera wake wapiga dili hawana lolote
 
Back
Top Bottom