Magufuli na mradi wa laptop kwa kila mwalimu,hivi tatizo ni ukosefu wa laptops?

Status
Not open for further replies.
Katika gazeti la Raia Mwema toleo no.418 ipo habari ya Mgombea Urais wa CCM kuwa eti atawapatia walimu wote laptops ili kuinua kiwango cha elimu,na labda kwa fikra zake,kuondoa umaskini nchini...

Nikiwa mwalimu,ahadi hii inanikera,hivi anafikiri sisi ni wapuuzi kiasi hicho cha kufikiri kuwa tutaipigia CCM kura kwa ahadi ya laptops?Na OK,ni lini katika madai ya msingi ya walimu kwa serikali kwamba kukosa laptops kumewahi kuwa tatizo?Na hivi katika ilani ya uchaguzi ya CCM kugawa laptop ndicho kipaumbele?Na basi tukubaliane kuwa tunataka laptops,zitasaidia vp kuinua kiwango cha ufundishaji?Iko wapi miundombinu ya ku-support hiyo project?Mradi wa JK wa Tanzania & Beyond uko wapi?

Kwa ufupi,mradi wa laptop umekwama Kenya na ulikwishakwama Nigeria...Mh.Magufuli kama hakujiandaa kugombea urais au kama mafuriko ya UKAWA yanamchanganya basi atangulie tu jehanamu,moto umewaka...waalimu hatuna mpango na CCM na kama haelewi basi aendelee kubwabwaja na mradi wake wa laptop

Huyu hafai kabisa! Lini walimu walidai kuwa wana shida na lap top?
Kura za walimu zishaenda ukawa!
 
Mbona fisadi Lowassa alisema anataka kila mwananchi awe kama Bakheresa na Mengi.

Tofautisha kati ya Natamani na Nitatoa Laptop na milioni 50....Hii ya magufuli ni Kampeni hasa....Na hatutakubali....
 
Video yake tafadhali ili ushahidi ukamilike then tumburuze yeye na Luuva Mahakamani
 
huku umeme hakuna walimu hawana makazi mazuri ya kuishi... aiseee ajipange upya aisee



LAPTOP DUH !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Lowasa kawashika ccm pabaya. hakuna namna nyingine oct wafunge virago wachape lapa. muda wa mabadiliko ndio sasa.
 
Laptop Ili Tuzifanyie Nini Ilihali Nyumba Ninayokaa Hapa Kijijini Ni Ya Miti Na Inavuja Na Hakuna Umeme! Sasa Hy Laptop Itanisaidiaje? MI NAHITAJI USAWA KATIKA MISHAHARA, DAKTARI MWENYE BACHELA NA MWALIMU MWENYE BACHELA TULIPWE VIWANGO SAWA. MWALIMU NAE NI DAKTARI WA VICHWA VYA WATOTO, ANAKARABATI BONGO ZAO.HVY WALIPWE MISHAHARA SAWA PAMOJA NA POSHO. HIYO NDIYO SHIDA YA WAALIMU WALA SIYO LAPTOP. Laptop Nitanunua Kwa Pesa Yangu Iwapo Utanilipa Mshahara Mzuri.
 
alisema lini na wapi wewe punga. weka picha tuone. usilete propaganda za kigamba.
Wewe Chadema akademia bora ukaye kimya wenzako wanajua alisema wapi ndiyo maana wapo kimya wewe nyumbu unatokwa na povu.
 
Hawa maccn wameshaanza kuchanganyikiwa kabisa .maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi?hawa ccm wanafunzi wanakaa chini madawati hamna hizo Laptop Magufuli anazosema anawadanganya walimu bure
 
No offence but it is a pathetic idea....je laptops zitalipa madeni yao yaliyosababishwa na kucheleweshwa kwa mishahara...yote tisa kuna shule hazina huduma muhimuu....kama vyoo au ndo mpango wa kuwa facebook walimu😕
 
Wewe Chadema akademia bora ukaye kimya wenzako wanajua alisema wapi ndiyo maana wapo kimya wewe nyumbu unatokwa na povu.

Mshazoea kudanganya uma wa watz na mwaka huu mtaisoma namba. bora kuwa nyumbu kuliko kutumika na mafisadi wa ccm wanaoitafuna nchi mchana kweupe. vijana atudanganyiki 2015 lowasa ndio rais na ujiandae kisaikoljia bwana mdogo Ritz haya.w.ani
 
wameshindwa kujenga mahabara kazi kuchangisha wananchi michango lukuki, wameshindwa kutengeneza madarasa na madawati, wameshindwa kutatua kilio cha walimu cha muda mrefu kupewa posho ya mazingira magumu, wameshindwa kujenga nyumba bora za walimu, wameshindwa kuwapa wanafunzi na walimu vitabu na vitendea kazi. Leo lijitu linakuja na sound ya Laptop na 50mill huu si uwizi kabisa. tena ananza uwizi mapema kabla ya kupewa nchi, je akipewa watakuja na zile tabia zao za kiburi cha madaraka, zero usikivu, ushauri hawataki na kuja na hoja za udanganyifu.
Watanzania tumeshtukia, tunataka mabadiliko. na mabadiliko yatatokea chini ya serekali ya ukawa itakayoongozwa na mzee wa mamuzi Edward Lowasa.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom