Magufuli na mradi wa laptop kwa kila mwalimu,hivi tatizo ni ukosefu wa laptops?

Status
Not open for further replies.
CCM hawajajua watanzania wanataka nini.
Uchaguzi huu Magufuli hajajipanga na hajui aongee nini.
Hivi kiuhalisia walimu walishawahi wana shida ya laptop?
Ina maana hao CCM hadi leo hawajui walimu wanahitaji nini?
CCM ijipange, uchaguzi wa mwaka huu watu watawahoji ahadi zao kama realistic, la sivyo wataona kama wanapotezewa muda tu.
 
Dr. Magufuli aahidi laptop kwa kila mwalimu na mil.50 kwa kila kijiji kukuza uchumi!!
KUPATA VICHEKESHO ZAIDI TOKA CCM. tuma neno VICHEKESHO kwenda namba 157337.

Acha unafiki mbona na wewe husemi ahadi ya mgombea wenu " kubwa la makapi na fisadi " lowassa alipowaambieni kuwa akiwa rais kila mtanzania atamjengea nyumba nzuri ya kuishi? Anakotoka tu huko monduli wapiga kura wake wengi ni masikini waliokithiri na makazi yao yalivyo mabaya na ya shida yanatumika kuvutia watalii wetu hapa Tanzania. Si bora magufuli kasema atatoa laptop kwa kila mwalimu na ni kitu ambacho kinawezekana na kinaiingia akilini sasa huyo lowassa wenu ameshatuambia atatujengeaje hizi nyumba? Watanzania tunadanganywa wazi wazi na lowassa halafu tunamshabikia.
 
Ameanza kwa kufeli, nchi hiii ccm hiii kweli kaingizwa choo cha kike pale dodoma, kibaya zidi hajui sera zaidi ya kujipendekeza kwa mkubwa wake, sasa yy ndio anatakiwa ajinasibu kama mkuu hapo domo zege. CCM wamechemka wamepeleka biashara ya pilipili kwa wanafunzi wa msingi lazima idode.

Una mpa laptop mwalimu anaeishi kwenye nyumba za mbavu za mbwa?
 
Kwanza miundombinu ya majengo, umeme, mishahara bora kwa Walimu na mtandao wa mkongo wa Taifa kila shule, projector za kutosha, wakiweza haya waanze kufikiria kugawa laptop. Ni dhahiri CCM wamekosa sera makini msimu huu!
 
Dah, afadhari alete tu hizo laptop nimfungulie kasteshenari mke wangu aache kufundisha kabisaaa
 
Anawachukulia wamu kama watoto vile yani ntakunulia pipi ukinisalimia! Hahahaha ikiisha utamu wewe upate heshima na sisi tubaki vilevile! SHAME

Hata mkimtoa kafara jike hampati dola mwaka huu, hamna pa kutokea
 
Ahadi za hivi bora usiahidi
isitoshe kampeni kisheria bado, hii ya kuahidi wananchi na vijiji kaitoa wapi?
Nimekumbuka ahadi za hivi kweli zinapatikana CCM tu na si kwingineko duniani
Acha unafiki mbona na wewe husemi ahadi ya mgombea wenu " kubwa la makapi na fisadi " lowassa alipowaambieni kuwa akiwa rais kila mtanzania atamjengea nyumba nzuri ya kuishi? Anakotoka tu huko monduli wapiga kura wake wengi ni masikini waliokithiri na makazi yao yalivyo mabaya na ya shida yanatumika kuvutia watalii wetu hapa Tanzania. Si bora magufuli kasema atatoa laptop kwa kila mwalimu na ni kitu ambacho kinawezekana na kinaiingia akilini sasa huyo lowassa wenu ameshatuambia atatujengeaje hizi nyumba? Watanzania tunadanganywa wazi wazi na lowassa halafu tunamshabikia.
 
Acha unafiki mbona na wewe husemi ahadi ya mgombea wenu " kubwa la makapi na fisadi " lowassa alipowaambieni kuwa akiwa rais kila mtanzania atamjengea nyumba nzuri ya kuishi? Anakotoka tu huko monduli wapiga kura wake wengi ni masikini waliokithiri na makazi yao yalivyo mabaya na ya shida yanatumika kuvutia watalii wetu hapa Tanzania. Si bora magufuli kasema atatoa laptop kwa kila mwalimu na ni kitu ambacho kinawezekana na kinaiingia akilini sasa huyo lowassa wenu ameshatuambia atatujengeaje hizi nyumba? Watanzania tunadanganywa wazi wazi na lowassa halafu tunamshabikia.

mimi ni mwalimu. na nimemsikia magufuli akiapa kuwa lazma atashinda. kwa kuwa ana uhakika na hilo nakuomba umshauri agawe kabisa hizo laptop na pesa.
 
Karibu huyu atawaambia polisi watafanya doria kwa helkopita.Alyotabiri prof Jay yaanza kujitokeza.Watachanganyikiwa sana mwaka huu.Si wawalipe madai yao kwanza?
 
Ki Mun

Hapo ndipo tunaposema ccm wana uwezo mdogo wa kufikri,,haingii akilini kwamba kila mwalimu akipata laptop itasaidia kiwango cha Elimu kupanda,, ni upumbavu tu.Laptop,je umewawekea internet ya kutosha kusurf material? Acha wawndelee kutoa ahadi za kitoto ili waje wapotee vizuri
 
Last edited by a moderator:
Wameishiwa sera.

Natafuta picha yule mwalimu wa Kijijini ambako hakuna Umeme hiyo Laptop ataitumiaje!!!!

Waalimu wanataka maslahi yeye anaahidi Laptop!!!!

Niliahidi.jpg

J. K..jpg

Thinking.jpg

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Wanafunzi wanakaa chini hawana madawati wengine wanasomea chini ya miti laptop zitasaidia nn? Walimu wanahitaji mishahara mizuri na mazingira bora ya kazi na kulipwa madeni yao ya miaka chungu nzima sio laptopb. Hilo la mil.50 kila kijiji naliacha kama swali Tanzania kuna vijiji vingapi Mara mil.50 ni trillion ngapi? Zitapatikana wap? Kwa nn zisitolewe cku zote ili kusaidia akina mama wanaojifungulia chini?mamilioni ya JK Yaliondoa kimaskini??
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom