- Thread starter
- #41
Nimesikiliza hiyo hotuba na ni kweli ametamka kuwa kinachohitajika sio haya mavyama ya siasa bali maendeleo! Nilichokiona kutoka katika hotuba yake ikiwa ni pamoja na lugha ya maneno na ya mwili (body language), ni kweli JPM anayosema anayesama kwa dhati, ana nia nzuri lakini HANA uelewa wa kutosha kutambua na kukubali kuwa chama chake, CCM, ndicho kilisababisha hayo anayoyaita 'mambo ya hovyo kabisa' aliyoyakuta na kwamba bila vyama vya upinzani kupaza sauti kali leo hii tungekuwa na Maembe na hayo anayoyaita ya hovyo yangekuwa business as usual! JPM anahitaji mshauri makini wa siasa au niseme sayansi ya siasa na anayemwamini na kumheshimu ili ampige msasa kwamba asikandamize wala kubeza upinzani (ninafikiri anaposema hawataki mavyama, anamaanisha upinzani) kwani ndio unampa nafasi aliye madarakani kujua wapi amejikwaa ama ameteleza katika juhudi zake za kutaka kuwaletea wananchi maendeleo.
Amekiri kwa uwazi kuwa amekuwa serikali kwa muda wa miaka 20 na anaposema kuna uozo anajua anachosema. Sasa kama aliuona huo uozo, kwa nini asijiulize kwa nini hakuthubutu hata kutoa pendekezo ya kuuondoa? Ni kwa sababu kwa utamaduni wa utawala wetu, ukiwa sehemu ya utawala huwezi kumkosoa mkubwa wako hata kama unaona anayofanya hayafai. JPM anakiri utawala wa awamu ya nne ulifanya mengi ya hovyo lakini asingeweza kufanya lolote. Ni mpinzani tu ambaye ana nafasi ya kumnyooshea mtawala kidole, tena hii imehalalishwa kikatiba. JPM anahitaji kasemina-elekezi ka faraghani ili aache kuwa anajishusha kiasi anachofanya linapokuja suala na siasa za upinzani. Siasa za upinzani (mavyama ya siasa) ni NGUZO kuu ya kuwaletea wananchi maendeleo, Mr President!
Correct mkuu, uelewa mdogo sana