Tindikali
JF-Expert Member
- Mar 26, 2010
- 2,014
- 2,664
Umar Farouk Abdulmuttalab.
Nilidhani huyo kijana aligundulika baada ya suruali yake kuanza kuwaka moto na kuunguza ukuta wa ndege. Mwenyewe alijipindua kama Mpakistan wa Times Square). Au wewe hebu tueleze polisi jamii ilifanikiwa vipi kumnasa Umar?
[FONT=Verdana, sans-serif]Dhana ya polisi jamii haina maana kuwa suala la kukamata wahalifu wanaachiwa wananchi. Hata huko kwa wenzetu, kazi ya kukamata na kufanya uchunguzi bado ni ya polisi. Kinachofanyika ni kuwa jamii inashiriki katika kutoa taarifa n.k. Jamii isiyokuwa na imani na polisi ni mara chache wanakuwa tayari kutoa taarifa zinazoweza kusaidia uchunguzi wa matukio ya uhalifu. Unachanganya polisi jamii na sungusungu. Sungusungu ndiyo walitegemewa kufanya kazi ya polisi. Katika polisi jamii, mamlaka na wajibu wa kukamata wahalifu unabaki wa polisi
Jibu hili swala, usizunguke mibuyu: Nani ana jukumu, na nani awajibike, na nani anaweza kuwa na taarifa zaidi, idara ambayo kazi yao ni uchunguzi wa ujambazi au raia ambae hana nyenzo, ujuzi, muda wala malipo? Jibu.[/FONT]
Wewe mwenyewe umesema uhalifu huko kwa wenzetu upo kwa viwango kama vya kwetu ... Kitu kingine usichojua ni kuwa pamoja na wao kuendelea lakini kero za uhalifu ni kama kwetu, mauaji, vibaka, uuzaji wa madawa ya kulevya n.k Hukudai hivyo? Huishi kujifunga funga. Na usiite ujambazi uhalifu wa kipuuzi. Labda kama unaishi kwenye ahera-salama huko kwa wenzenu ndio unaweza kuwa na moyo mkavu kiasi cha kuita ujambazi hapa kwetu ni upuuzi. Ni janga linalotuua kila siku! Usiwe nje ya mguso.Mafanikio si kutokomeza uhalifu. Hata nchi zenye sheria kali bado zina uhalifu. Mafanikio ni kupunguza uhalifu kwa kiasi kikubwa. Na huko kwa wenzenu, katika maeneo mengi uhalifu wa kipuuzi umepungua sana. Lakini bado kuna sehemu ambako uhalifu bado uko juu. Mara nyingi katika maeneo haya polisi anachukuliwa kama adui na hamna kitu kibaya kama kuwa "snitch".
Na si kweli kwamba sehemu zilizojaa uhalifu huko kwa wenzenu kuna uhusiano na wambea kuchukiwa. Viwango vya uhalifu huko vinaendana na milinganyo ya hali ya uchumi wa miji na maeneo, elimu na ajira. Si kwa sababu ya mafanikio ya polisi jamii. Usipotoshe.
Wewe mwanzoni ulipoongelea kwa wenzenu ulianisha ni Uingereza? Kumbe Uingereza ndio polisi wanatembea mitaani kusogoa na Wananchi wakisakanya dodoso za majambazi? Basi Magharibi niliyoiona mimi hilo hakuna! Askari akichoka doria anaenda kula mandazi sukari yenye matobo, ndo sifa waliyonayo, haendi kuvinjari na porojo katini mwa wananchi. Wananchi hawana muda huo barabarani.Kwa wenzenu wapi ulikoenda? Dhana ya polisi kufanya patrol kwa kutembea iko uingereza.
Watoto na Wafanya biashara wana kazi pia, hawana mda wa kusogoa na polisi kwenye beats.! Watalii hawajui majambazi ya jamii, wengi wao ni watembezi wageni. Vikongwe huko kwa wenzenu vingi vinafungiwa ndani ya nyumba za wakunga na si kuzurura kwenye polisi jamii.Si wananchi wote wana ari na kasi katika maisha yao. Kuna watoto wadogo, vikongwe, wenye biashara ndogo ndogo, watalii n.k. Wote hawa wanapokuwa na shida ndogo ndogo kimbilio lao ni polisi...
Kwa hiyo beats hawakusanyi taarifa za majambazi. Na ulisema beats wanasimama kuongea na wananchi. Kumbe maongezi haya ya nini, matokeo ya Azam FC na Yanga? Nini maana ya hizi beats na polisi jamii kama hazitusaidii kiuchunguzi? Kwenye kurasa za nyaraka ya polisi uliotubandikia hapa wamesema msingi mmoja wa polisi jamii ni uchunguzi wa siri kung'amua matatizo kwenye jamii, Intelligence-led identification of community concerns... Sasa kama hizo beats hazikusanyi taarifa zozote basi usizipigiea chapuo kama kielelezo cha polisi jamii....Wanaofanya uchunguzi wa matukio ya uhalifu mara nyingi si askari wanaokuwa kwenye beats. Uchunguzi unafanywa na askari kanzu (CID).
...e hiyo Witness Protection Program ... si ndiyo sehemu ya polisi jamii?
Na ni kielelezo cha utisho wa jambazi kwa raia. Raia anaogopa jambazi ndo maana akimshuhudia yabidi alindwe. Sisi mnatuambia tukashuhudie kichwa kichwa eti majambazi wanatuogopa, tafadhali!
Fundi Mchundo, umefanya utafiti kung'amua kwamba wakati wenu uhalifu wa kipuuzi ulikuwa chini? Umefanya uchunguzi kugundua kwamba sababu ya tofauti hizo za enzi ni kwa vile mlikuwa mnanyukwa viboko na jirani? Na kama hayo ni kweli, basi inawezekana ni kwa sababu ya kuiga hayo mambo ya kwa wenzetu. Maana hatuishi kuchambua jambo bila kuiga ya kwa wenzetu. Halafu uhalifu wa kipuuzi ni upi? Tunaongelea ujambazi hapa. Usidogoeshe uzito wa janga la wananchi tafadhali.... Sisi wakati tunakuwa uhalifu wa kipuuzi ulikuwa chini. Na sababu kubwa ilikuwa ukionekana unaiba embe basi utacharazwa bakora na ukishitaki kwa mzazi wako atakuongezea. Kulikuwa na zero tolerance na upuuzi kama huo. Leo ukijaribu kumsema tu mtoto wa jirani ...
Sehemu gani, huku kwa wenzetu wapi kaka? Nilidhani ni wenzenu wewe, unanichenjia kibao? Usiwateme wenzenu bana... hahahaaaaaa.Na huko kwa wenzenu sehemu kama hizo zipo.
Hili somo la mtapanyiko wa ufuatiliaji wa sheria baina ya majimbo na shirikisho la Marekani apa linatusaidia nini? Nilipoongelea FBI ukasema uhalifu mwingi unashughuliwa na local police. Nikwambia hata FBI nao wanahusika kwa kiasi kikubwa tu. Sasa unasema FBI wanahusika na usafirishaji bangi majimboni, kwani huo sio uhalifu? Kwa nini ulisema nisiwaongelee FBI?Marekani kuna sheria za State na sheria za nchi nzima. FBI wanashughulikia uvunjaji wa sheria za nchi. Kwa mfano, ukikamatwa unauza bangi, utashitakiwa na kushughlikiwa na mamlaka za state. Lakini ukikamatwa unasafirisha bangi kutoka State moja kwenda Nyingine, utashughulikiwa na FBI pamoja na polisi wa state husika.
Kama anafanya kazi kitengo cha uhalifu wa silaha Vingunguti anatakiwa aelewe hali na mandhari nzima ya Vingunguti. Atasemaje yeye mgeni wazazi wake wanatoka Magu? Arudi akafanye kazi Magu basi, anakokuelewa. Eti polisi ni wageni, sisi ndio tunajua wezi wa maeneo yetu, nyinyi ndio mnalipwa, mnafundishwa, mna muda, mna nyenzo za kusakanya majambazi, fanyeni kazi yenu....Sasa kama mzazi wa polisi yuko Magu au Tarime wakati yeye mwenye anafanya kazi vingunguti itasaidia nini katika kuwakamata wahalifu wa vingunguti?
He! Kwa hiyo Fundi Mchundo unatuambia kwamba majambazi yameshamiri kwa sababu yanakubalika na jamii? Msikieni huyu mja. Kuwageuka? Wanaogopa jamii kuwageuka, ina maana kwa sasa wana jamii wako upande wa majambazi? Tukiwageuka wataacha! Jambazi halitegemei raia awe upande wake, ndo maana linamuua!Hamna kitu ambacho jambazi wanaogopa kama jamii kuwageuka. ... Polisi jamii itasaidia kuwa hata kabla ya tukio jambazi atajua kuwa hakubaliki na jamii itamtosa akifanya upuuzi wake.
Nini tofauti ya polisi posti na vituo vya polisi?]Polisi posti zinafanya polisi kuwa karani na kungojea aletewe taarifa na mwananchi...Vituo vya polisi vitakuwepo.
...Akitoa taarifa kwenye kituo cha polisi kwa simu basi wao ndio watamuagiza polisi aliyekaribu na tukio kwenda kutoa msaada.
Hilo la simu ni kwetu au la kwa wenzetu? Tanzania hakuna namba ya polisi ya dharura itakayoleta askari papo hapo. Tulikamata mwizi mtaani miezi michache iliyopita nikapiga simu, polisi walipofika jamaa keshafika kuzima kitambo. Wakaanza kutuhoji sisi kuhusu anaejua ubini wa marehemu. Nikawaambia kwa nini hamkuwahi kuja kumhoji mwenyewe? Zamani tulikuwa na 999, siku hizi tunapewa namba ya mkononi ya Kamanda Kova. Usiwe nje ya mguso.
Na akipita atatugongea mlangoni? Kila mtu ana zake mtaani, hakuna mwenye mda kukaa gengeni kusubiri askari apite amweleze matatizo yake. Au kilabuni? Na tunaongelea ujambazi hapa, sio swala la kawaida la kusubiri askari apite.Kama mwananchi atakuwa na swala la kawaida linalomuhitaji polisi basi atamsubiri mtaani maana ni lazima atapita.
Mfano huu nimetumia kukujibu ulipodai kuwa wananchi wanogopa majambazi kwa sababu wanabeba SMG. Hakuna mahali nilipotetea uchukuaji wa sheria mikokoni
Kama wananchi hawaogopi SMG majambazi yanawezaje kuweka kitongoji kizima chini ya ulinzi? Umati wa watu wenye mawe unafua dafu kwenye shaba za m-gobole? Sasa unataka kujifanya Kinjekitile mamboleo.
Hiyo nyaraka inakuonya kwenye dibaji kwamba usiisome kama kilelezo cha ufanisi wa polisi jamii. Kwa sababu, kwanza, inasema ni picha ya haraka ya mpango majaribio wa awali, na yabidi tusubiri mpango mzima ukamilike ndani ya miaka mitatu; The report provides a snapshot of the evidence as it stood after the first year of national implementation, and should not be read as a definitive account of whether neighbourhood policing works. Such an assessment can only be made after the end of the three-year programme, when neighbourhood policing should be implemented in full. Moja, la pili, ripoti inaongelea aina za uhalifu wa huko kwa wenzenu, ambao ni tofauti kabisa na halifu za hapa kwetu. Huwezi niwekea ki-ripoti cha kwa wenzenu wa Liverpool ukadai kitusaidie kuelewa umuhimu wa polisi jamii Vingunguti. Tatu, nipe vielelezo vilivyoandikwa na watafiti huru, sio dondoo ya askari hukusu mafinikio ya mpango wa askari, iliyoandikwa na idara ya askari!
Polisi jamii ni ukingu unaowapa polisi kisingizio wanapolegalega kwenye majukumu yao kulinda raia.
Wewe ndo ulisema ni bora ninyamaze, ufikiri wangu mfupi. Sasa unanipa ruhsa ya kusema. Basi ngoja nimalizie kwa kusema Zidumu Fikra za Fundi Mchundo... Ziduuum!Ni kweli upeo wako wa kufikiri ni mdogo. Hii haikuondolei haki yako ya kutokubaliana na chochote nitakachokisema.