Magufuli aponda dhana ya polisi jamii dhidi ya majambazi : Waziri Masha na Mwema mpo!

Mimi ninavyoelewa Polisi jamii ni jitihada za kuwaweka polisi kuwa karibu na jamii. Hii inatokana na ukweli kuwa jamii ndiyo inataarifa zaidi kuhusu uhalifu kuliko polisi. Jamii ikiwa na imani na polisi na kushirikiana nao basi hao majambazi watakosa mahali pa kukimbilia. Kwa wenzetu wanaita "neighbourhood policing". Hata siku moja si dhana ya kuwakumbatia majambazi.

Kama kweli waziri alisema aliyoyasema basi hastahili nafasi ya uongozi maana haouwezi kushabikia kuwa mtuhumiwa ( hata huyo tunaemwita jambazi ni mtuhumiwa mpaka hapo atakapopatikana na hatia mbele ya Pilato) atolewe ngeu kabla hata hajafikishwa mahakamani ni hatari tupu. Mapolisi wetu wanatakiwa wawekewe breki kwanza badala ya kusisitiza kuwa waendeleza ubabe kwa wananchi. Na, naam, mtuhumiwa nae ni mwananchi na anastahili kulindwa na sheria badala ya kutolewa ngeu.

Amandla......
 
Fundi Mchundo ni kweli kabisa dhana ya polisi jamii ni kama ulivyoieleza. Lakini inavyoletwa na kutekelezwa hapa kwetu ni tofauti.

Hapa kwetu polisi wanadhani kuwa polisi jamii maana yake ni wananchi kujilinda wenyewe kwa marungu, mapanga na silaha zinazofanana na hizo dhidi ya majambazi yenye silaha nzito nzito za kivita kama SMG and LMG.

Sasa ukiangalia polisi jamii inasaidia kupambana na vibaka wadogowadogo tu na siyo majambazi waliokubuhu kama wale wa Tarime ambao walikuwa na guts za kuteka kituo cha polisi na kuiba ng'ombe baada ya kuvurumisha risasi mfululizo kwa masaa mawili.

Hivyo nakubaliana kimsingi na Magufuli kuwa majambazi ya aina hii hayahitaji polisi jamii yanataka mkakati maalumu wa polisi kupambana nao na kuwatokomeza. Na kwa taarifa zako ukitoa taarifa za majambazi polisi unakuwa unahatarisha maisha yako kwani hawa polisi wako kwenye payroll za majambazi.
 
tatizo vitendea kazi ni hafifu, na polisi wenyewe ni wachache. Inabidi serikali iajili polisi kama mara 10 hivi waliopo saizi na wapewe nyezo za uhakika. Hakuna kutongozana na jambazi. Polisi atembee kama polisi kwamba mda wowote anaweza kutoana manundu na jambazi.
Na si kutembea na suruali za kaki utafikiri wanafunzi wa sekondari ya bagamoyo
 
JK of course anaprefer kina Pinda-mtoto wa mkulima kina Shein, Lau Masha watu ambao ni dormant kwakweli in so many ways. Anyone who has better education than him and is actually smarter (sio foji foji za mzumbe) na ana charisma jamaa anamuogopa. Salim anaakili lakini hana charisma ya Magufuli. Of course nae ni mjanja mjanja (dont be fooled) alikua anataka uPM sikunyingi infact mpaka sasa anaona mtandao wanamchafulia.. 2015 lazima akaze sema saivi kabanwa hana jinsi inabidi awe mdogo tuu..

Umenena.
Hats off Dr. Magufuli!

JK hamna kitu pale.
Kwenye Wizara nyeti (zenye ulaji au zinazoweza kusikika sana) JK anateua kwa USHIKAJI TU.
Mfano utendaji wa 'washkaji' kwenye Wizara hizi: Ulinzi (Mwinyi), Mambo ya ndani (Masha), Nishati (Ngeleja), Mambo ya nje (Membe), Fedha (Mkullo), Utumishi (Ghasia), Miundombinu (Kawambwa) Siyo kabisaaaaaa.
Anapenda ma-dormant na akina 'ndiyo mzee'.
Afadhali jk mwenyewe ANGEKUWA NA UWEZO WA KUWASIMAMIA, ila na yeye ndiyo DUH! Anahitaji KUSIMAMIWA.
 
Fundi Mchundo ni kweli kabisa dhana ya polisi jamii ni kama ulivyoieleza. Lakini inavyoletwa na kutekelezwa hapa kwetu ni tofauti.

Hapa kwetu polisi wanadhani kuwa polisi jamii maana yake ni wananchi kujilinda wenyewe kwa marungu, mapanga na silaha zinazofanana na hizo dhidi ya majambazi yenye silaha nzito nzito za kivita kama SMG and LMG.

Sasa ukiangalia polisi jamii inasaidia kupambana na vibaka wadogowadogo tu na siyo majambazi waliokubuhu kama wale wa Tarime ambao walikuwa na guts za kuteka kituo cha polisi na kuiba ng'ombe baada ya kuvurumisha risasi mfululizo kwa masaa mawili.

Hivyo nakubaliana kimsingi na Magufuli kuwa majambazi ya aina hii hayahitaji polisi jamii yanataka mkakati maalumu wa polisi kupambana nao na kuwatokomeza. Na kwa taarifa zako ukitoa taarifa za majambazi polisi unakuwa unahatarisha maisha yako kwani hawa polisi wako kwenye payroll za majambazi.

Kumbe ndiyo hivyo! Yale yale ya sungusungu! Kama ni hivyo basi kweli ni dhana potofu. Polisi hawawezi kukwepa majukumu yao kwa kuwasukumizia wananchi.

Amandla.........
 
...Hii inatokana na ukweli kuwa jamii ndiyo inataarifa zaidi kuhusu uhalifu kuliko polisi... na polisi na kushirikiana nao basi hao majambazi watakosa mahali pa kukimbilia. .

Upotoshaji, tena wanautumia polisi, na sasa wananchi washapikwa na kuiva.

Polisi kazi yao maalum, moja ya kazi yao mahususi, ni kuchunguza ujambazi, uhalifu kwa ujumla. Hivi mimi mpara miwa wa Vingunguti kwa Mnyamani nitajuaje nyeti za ujambazi kuliko vitengo vya CID vya polisi kaka?

Unaongelea polisi wanavyofanya kazi huko kwa wenzenu, hivi unataka kunambia huko wananchi wanajua zaidi nyeti za Al Qaida wa USA kuliko FBI na National Security Agency?

Kama ambavyo jambazi anajificha kwa polisi ndo hivyo hivyo anajificha kwa raia wema, si kwamba wanajulikana mtaani. Na jambazi hawawezi kukosa kwa kukimbilia kwa kuogopa raia, yeye ana SMG mwananchi ana nini, mdomo? Na ndo maana huko kwa wenzenu vyombo vya dola huhimiza kulinda wananchi watoa siri na shahidi za uhalifu hata kuwahamisha (witness protection program) maana wanajua raia mwenye mdomo mrefu mtaani hafui dafu kwa jambazi hatari, atakatwa ngebe.

Kwa nini sisi tuwajue wao wasiwajue? Kina Kova wanatuambia Majambazi wanatokea kati ya wananchi, mitaani, kwani polisi wanatoka wapi, mwezini kati ya nyota?
 
Hivi hii nadharia ya polisi jamii anayotuelezea huyu Dr Magufuli ikoje jamani...............nafikiri intaka zaidi ushirikiano kutoka kwa wananchi dhidi ya wahalifu.........na sio kukumbatia wahalifu...............au?
 
Upotoshaji, tena wanautumia polisi, na sasa wananchi washapikwa na kuiva.

Polisi kazi yao maalum, moja ya kazi yao mahususi, ni kuchunguza ujambazi, uhalifu kwa ujumla. Hivi mimi mpara miwa wa Vingunguti kwa Mnyamani nitajuaje nyeti za ujambazi kuliko vitengo vya CID vya polisi kaka?

Unaongelea polisi wanavyofanya kazi huko kwa wenzenu, hivi unataka kunambia huko wananchi wanajua zaidi nyeti za Al Qaida wa USA kuliko FBI na National Security Agency?

Kama ambavyo jambazi anajificha kwa polisi ndo hivyo hivyo anajificha kwa raia wema, si kwamba wanajulikana mtaani. Na jambazi hawawezi kukosa kwa kukimbilia kwa kuogopa raia, yeye ana SMG mwananchi ana nini, mdomo? Na ndo maana huko kwa wenzenu vyombo vya dola huhimiza kulinda wananchi watoa siri na shahidi za uhalifu hata kuwahamisha (witness protection program) maana wanajua raia mwenye mdomo mrefu mtaani hafui dafu kwa jambazi hatari, atakatwa ngebe.

Kwa nini sisi tuwajue wao wasiwajue? Kina Kova wanatuambia Majambazi wanatokea kati ya wananchi, mitaani, kwani polisi wanatoka wapi, mwezini kati ya nyota?

Wakati mwingine ni heri kunyamaza kuliko kujibu kitu usichoelewa. Hivi unadhani nani walimchomea yule kijana aliyetaka kujilipua nyeti zake? Si ndugu zake? Huko Marekani wana kipindi kinaitwa " America's Most Wanted" ambamo picha za wahalifu hatari wanaotafutwa zinarushwa kwenye luninga . Kipindi hicho kinaandaliwa na watu binafsi na sio serikali lakini majambazi wengi wamekamatwa kutokana na taarifa zinazotolewa na wananchi! Kitu kingine usichojua ni kuwa pamoja na wao kuendelea lakini kero za uhalifu ni kama kwetu, mauaji, vibaka, uuzaji wa madawa ya kulevya n.k. Lakini kwa wenzetu wameanzisha neighbourhood policing ambapo polisi wanajitahidi kujenga imani ya jamii. Polisi wao hawakai polisi posti bali wanakula beat kuzunguka maeneo yao. Wakati wa beat wanaongea na wananchi na wanatoa misaada pale inapowezekana. Kutokana na huo ukaribu wao wananchi wanakuwa tayari kutoa taarifa pale uhalifu unapofanyika. Si kila mtoa taarifa anawekwa chini ya witness protection program. Wengi wa waalifu wasumbufu ni hao vibaka na small time drug dealers. Anonymous calls zinatosha kuwaondoa mitaani. Uhalifu mwingi unashughulikiwa na local police wala hamna haja ya kuingiza vyombo kama FBI!

Kutegemea polisi tulionao watawajua wote ni mawazo potovu. Mara nyingi katika maeneo mengi polisi hao ni wageni lakini wahalifu ni watoto wetu. Ni kwa kuwazibia macho na kungojea ati polisi waje kuwashughulikia ndiko kunako watia kiburi. Kingine ni huo mtindo wa kuwajengea polisi post ambamo sasa mapolisi badala ya kuingia mtaani wanashinda na kujifanya mamangi meza! Unazungumzia SMG. Ni mara ngapi majambazi wameuawa kwa kupigwa mawe na umati wa watu wenye hasira pamoja na kuwa ameshika SMG?

Usijibu ili mradi kujibu tu. Fikiri kwanza.

Amandla......
 
Fundi Mchundo

Nakuunga mkono kabisa, dhana ya Polisi Jamii haijaeleweka kabisa katika Tanzania. Waziri Magufuli hajaielewa, utaona maoni ya wengi hapa mpaka kuwa na wao hawaielewa.

Kwa wale wanaopenda kuelewa (sio kushabikia) ufafanuzi alioutoa Fundi Mchundo umekamilika vizuri. Dhana ya Pilisi Jamii ni ushirikiano baina ya Polisi na Jamii na sio Polisi kuelimisha au kukumbatia Majambazi.

Kwa kuongezea, silaha namba moja dhidi ya Majambazi na uhalifu wa aina yoyote ni Jamii.
 
Wakati mwingine ni heri kunyamaza kuliko kujibu kitu usichoelewa. Hivi unadhani nani walimchomea yule kijana aliyetaka kujilipua nyeti zake? Si ndugu zake? Huko Marekani wana kipindi kinaitwa " America's Most Wanted" ambamo picha za wahalifu hatari wanaotafutwa zinarushwa kwenye luninga . Kipindi hicho kinaandaliwa na watu binafsi na sio serikali lakini majambazi wengi wamekamatwa kutokana na taarifa zinazotolewa na wananchi! Kitu kingine usichojua ni kuwa pamoja na wao kuendelea lakini kero za uhalifu ni kama kwetu, mauaji, vibaka, uuzaji wa madawa ya kulevya n.k. Lakini kwa wenzetu wameanzisha neighbourhood policing ambapo polisi wanajitahidi kujenga imani ya jamii. Polisi wao hawakai polisi posti bali wanakula beat kuzunguka maeneo yao. Wakati wa beat wanaongea na wananchi na wanatoa misaada pale inapowezekana. Kutokana na huo ukaribu wao wananchi wanakuwa tayari kutoa taarifa pale uhalifu unapofanyika. Si kila mtoa taarifa anawekwa chini ya witness protection program. Wengi wa waalifu wasumbufu ni hao vibaka na small time drug dealers. Anonymous calls zinatosha kuwaondoa mitaani. Uhalifu mwingi unashughulikiwa na local police wala hamna haja ya kuingiza vyombo kama FBI!

Kutegemea polisi tulionao watawajua wote ni mawazo potovu. Mara nyingi katika maeneo mengi polisi hao ni wageni lakini wahalifu ni watoto wetu. Ni kwa kuwazibia macho na kungojea ati polisi waje kuwashughulikia ndiko kunako watia kiburi. Kingine ni huo mtindo wa kuwajengea polisi post ambamo sasa mapolisi badala ya kuingia mtaani wanashinda na kujifanya mamangi meza! Unazungumzia SMG. Ni mara ngapi majambazi wameuawa kwa kupigwa mawe na umati wa watu wenye hasira pamoja na kuwa ameshika SMG?

Usijibu ili mradi kujibu tu. Fikiri kwanza.

Amandla......

Mchundo
Kingine niliona hapa, jamaa ubwa wake sijui alimuudhi nini akamtoa akamweka ktk bakoni na kumwaadhibu vikali kwa makofi yule mbwa, sasa bibi yake wa kufikia akamchukua picha akimuadhibu umbwa na baada ya hapo bibi kaenda polisi na jamaa akapigwa jela miaka 3

Kingine
Kwetu inabidi watu wawe wanajisajili sehemu unapoishi, hata kama ni kwako lazima kuwe na ofsi za kujisajili na kama hujasajililiwa kulala ktk nyumba hiyo huruhusiwi kulala ktk nyumba hiyo.Na akija mgeni kwako inabidi ukamsajili kwa mda.

Mahotelini inabidi wawe na database za picha na documents zinazotambulika, akifika mgeni apigwe picha na kukabidhi documents kama hana documents asilale ktk nyumba ya wageni.

nne
wale wanajeshi wa kujenga taifa na jeshi la wananchi, Ktk siku za karibuni hatutarajii dharula ya vita. wale wanajeshi wote wawe polisi waongezwe tu mshahara kama 50 na magari yao yawe ma karandiga ya polisi.
 
Ukiangalia uingereza (tofauti na marekani) si polisi wengi wanaobeba silaha za moto. Wao wanakitu kinaitwa Armed Response Vehicles ambazo zinatumika panapohitajika utumizi wa silaha. Miji mingine imeamua kuwa na patrol za Polisi waliobeba silaha katika vitongoji ambapo matukio ya uhalifu wa kutumia silaha za moto umekithiri. Polisi wenyewe hawapendi kubeba silaha. Kwanza wanaamini inawatenganisha na jamii, hasa ukizingatia msingi wa polisi uingereza ni "beats" yaani polisi kuzunguka eneo husika kwa miguu. Sababu nyingine ni hofu ya kutokea matukio ya kuuuawa kwa wananchi kwa bahati mbaya. Na nyingine ni kuwa kutokana na tamaduni hiyo basi wengi wa wahalifu uingereza hawatumii silaha za moto katika shughuli zao. Uingereza, "Bobby" wa kiingereza ni sehemu ya jamii. Mafanikio haya ndiyo yanayofanya nchi kama Marekani nao waangalie upya uhusiano kati ya jamii na polisi. Ndiyo maana juhudi zinafanyika kuajiri polisi kutoka kila sehemu ya jamii ( weusi, latino, korea, wachina n.k.)ambao wataweza kukubalika kirahisi katika maeneo ambao wengi wa asili yao wanaishi. Yote haya ni katika kujaribu kuwa karibu na jamii.

Amandla........
 
Hivi Bajeti ya hili Jeshi letu iliongezeka walau?............maana hawa jamaa zetu............ni msoto kwa kwenda mbele...................no wonder kumsikia Dr. Magufuli anasema mapolisi wanawakumbatia majambazi eti "polisi jamii"................
 
Swali zuri, Mkuu!
Inabidi tuangalie swala la police quarters. Kwa kuwaweka kwenye makambi ambayo tunashindwa kuiyahudumia tunazidi kuwatenga na jamii. Hii inatokana na dhana kuwa wajibu wao ni kuwashikisha adabu umma! Wapewe mshahara mzuri utakaowawezesha kuishi uraiani. Ni kama vile ambavyo hatuwaenzi walimu halafu tunashangaa quality ya elimu yetu inavyozidi kudumaa! Inabidi polisi wawe sehemu ya kuzuia uhalifu kuokea badala ya kutumika tu pale uhalifu kishafanyika. Hatutaweza kufanikisha hili kama tutaendelea kuwatenga na jamii.

Amandla....
 
...Hivi unadhani nani walimchomea yule kijana aliyetaka kujilipua nyeti zake? Si ndugu zake? Huko Marekani...
Kijana gani huyo kaka? Si vichwa vyote vya habari vya huko Marekani vinatufikia. Ungenifafanulia kijana huyo alifanya nini tuweze kuoanisha.

... kipindi kinaitwa "America's Most Wanted" ambamo picha za wahalifu hatari wanaotafutwa zinarushwa kwenye luninga . Kipindi hicho kinaandaliwa na watu binafsi na sio serikali ….
"[FONT=Verdana, sans-serif]Na sio serikali." Umesema mwenyewe, "na sio serikali." Hizo juhudi za watu binafsi hazifanywi na wananchi kwa niaba ya serikali, mzigo wa kukamata wahalifu bado hajatupiwa mwananchi anaeangalia maonyesho ya kipindi hicho. Serikali ndio ina vyanzo na nyenzo za kupambana na ujambazi, polisi jamii ni dhana ya ukingu wa kukwepa wajibu.[/FONT]

... Kitu kingine usichojua ni kuwa pamoja na wao kuendelea lakini kero za uhalifu ni kama kwetu, mauaji, vibaka, uuzaji wa madawa ya kulevya n.k. Lakini kwa wenzetu wameanzisha neighbourhood policing ambapo polisi wanajitahidi kujenga imani ya jamii. ..
[FONT=Verdana, sans-serif]Anhaa, sawa, asante kunijuvya. Kumbe huko "kwa wenzenu" uhalifu na ujambazi ni kama hapa kwetu? Walahi ibilisi kasambaa kila mandhari. Sasa mbona ulijaribu kutujengea hoja hapa kwamba polisi jamii huko "kwa wenzenu" imefaninikiwa? Naona kama unajifunga funga. Labda tueleze tena.[/FONT]

Polisi wao hawakai polisi posti bali wanakula beat kuzunguka maeneo yao. Wakati wa beat wanaongea na wananchi na wanatoa misaada pale inapowezekana.
[FONT=Verdana, sans-serif]Huo si ukweli Mkuu, nimepata bahati ya kwenda warsha ndogo ndogo huko "kwa wenzenu" na sijaona polisi wakiwa katika "beat" eti wanasimama kuongea na wananchi. Kwanza wananchi wengi huko "kwa wenzenu" wanakuwa na miendo ya kasi kali na ari kali na nguvu kali, sijaona mtu anaacha zake, anasimama eti kuongea na polisi barabarani kumpa dodoso za majambazi! Ha ha haha haaaaa! Sijaona...! Askari wa huko "kwa wenzenu" wanapokuwa doria wanakuwa wamekunja ndita wakisoma lugha za mwili nyusoni mwa watu, hawafanyi uchunguzi wa ujambazi wanapokuwa doria, wanalinda doria![/FONT]

Si kila mtoa taarifa anawekwa chini ya witness protection program.
[FONT=Verdana, sans-serif]Nani kasema watoa taarifa wote wanawekwa chini ya mpango huo? Nilionyesha jinsi majambazi yanavyoweza kuwa tishio wa watoa taarifa, maana ulijaribu kutuambia kwamba majambazi huwa hawana pa kujificha kama wananchi wanawataja. Nikakuonyesha jinsi mwananchi ndio anaweza akawa hana pa kujificha bila mpango maalum wa kumlinda.[/FONT]

Uhalifu mwingi unashughulikiwa na local police wala hamna haja ya kuingiza vyombo kama FBI!
[FONT=Verdana, sans-serif]Na uhalifu mwingi unashughulikiwa na hao FBI pia. [/FONT][FONT=Verdana, sans-serif]Kama "hamna haja ya kuingiza FBI" kwa nini kuna FBI? [/FONT]

Mara nyingi katika maeneo mengi polisi hao ni wageni lakini wahalifu ni watoto wetu.
[FONT=Verdana, sans-serif]Si umesema polisi yabidi wawe karibu na jamii, na ndo msingi wa polisi jamii? Kama ndo hivyo basi polisi hawawezi, hawatakiwi, kuwa wageni! Wakiwa karibu hawawezi kujitoa kwenye majukumu yao kwa kujisema wao wageni. Kwamba polisi hawajui wahalifu kwa sababu wao ni wageni, wahalifu ni watoto wetu, polisi ni watoto wa nani? Polisi wa Vingunguti wanatoka wapi, huko kwa wenzenu?[/FONT]

[FONT=Verdana, sans-serif]Na hata kama kisingizio cha polisi kutofanya kazi ya kusakanya majambazi eti kwa vile hawawajui kwa ugeni wao, bado tunarudi kwenye ukweli kwamba wao ndo wanafanya uchunguzi, ndo kazi yao, mwananchi hafanyi uchunguzi. Hilo mbona hulijibu? [/FONT]

Ni kwa kuwazibia macho na kungojea ati polisi waje kuwashughulikia ndiko kunako watia kiburi.
[FONT=Verdana, sans-serif]Mkuu, hiyo ndio kazi ya polisi![/FONT]

[FONT=Verdana, sans-serif]Na jambazi akijua kwamba anaemfuatilia ni raia asiye na nyenzo, mafunzo wala malipo, hataogopa, jambazi linaogopa askari kuliko mtu baki. Ndo maana wanafunga mtaa mchana kweupe wanateka, wanaua, wanaondoka. Tutumie jeshi la polishi.[/FONT]
Kingine ni huo mtindo wa kuwajengea polisi post ambamo sasa mapolisi badala ya kuingia mtaani wanashinda na kujifanya mamangi meza...
Si umesema unataka polisi karibu? Vituo vidogo vya askari posti vilijengwa kusogeza polisi karibu. Sasa mwananchi akiwa na swala linalohitaji polisi aende kumngoja barabarani?

Ni mara ngapi m?ajambazi wameuawa kwa kupigwa mawe na umati wa watu wenye hasira pamoja na kuwa ameshika SMG...
[FONT=Verdana, sans-serif]Mtume! [/FONT]

[FONT=Verdana, sans-serif]Yani polisi jamii kumbe ni haki umati ya mwiiiziii....chomaaa... uaa! Labda kweli wote, na Magufuli, na Said Mwema mwenyewe, hatuelewi polisi jamii ni nini. [/FONT][FONT=Verdana, sans-serif]Badala ya kutetea utawala wa sheria unatetea haki umati?[/FONT]

Usijibu ili mradi kujibu tu. Fikiri kwanza.
[FONT=Verdana, sans-serif]Upeo wangu wa kufikiri mdogo, ndio , lakini sijakubaliana na baadhi ya uloyasema hapo.
[/FONT]
 
Kijana gani huyo kaka? Si vichwa vyote vya habari vya huko Marekani vinatufikia. Ungenifafanulia kijana huyo alifanya nini tuweze kuoanisha.

"[FONT=Verdana, sans-serif]Na sio serikali." Umesema mwenyewe, "na sio serikali." Hizo juhudi za watu binafsi hazifanywi na wananchi kwa niaba ya serikali, mzigo wa kukamata wahalifu bado hajatupiwa mwananchi anaeangalia maonyesho ya kipindi hicho. Serikali ndio ina vyanzo na nyenzo za kupambana na ujambazi, polisi jamii ni dhana ya ukingu wa kukwepa wajibu.[/FONT]

[FONT=Verdana, sans-serif]Anhaa, sawa, asante kunijuvya. Kumbe huko "kwa wenzenu" uhalifu na ujambazi ni kama hapa kwetu? Walahi ibilisi kasambaa kila mandhari. Sasa mbona ulijaribu kutujengea hoja hapa kwamba polisi jamii huko "kwa wenzenu" imefaninikiwa? Naona kama unajifunga funga. Labda tueleze tena.[/FONT]

[FONT=Verdana, sans-serif]Huo si ukweli Mkuu, nimepata bahati ya kwenda warsha ndogo ndogo huko "kwa wenzenu" na sijaona polisi wakiwa katika "beat" eti wanasimama kuongea na wananchi. Kwanza wananchi wengi huko "kwa wenzenu" wanakuwa na miendo ya kasi kali na ari kali na nguvu kali, sijaona mtu anaacha zake, anasimama eti kuongea na polisi barabarani kumpa dodoso za majambazi! Ha ha haha haaaaa! Sijaona...! Askari wa huko "kwa wenzenu" wanapokuwa doria wanakuwa wamekunja ndita wakisoma lugha za mwili nyusoni mwa watu, hawafanyi uchunguzi wa ujambazi wanapokuwa doria, wanalinda doria![/FONT]

[FONT=Verdana, sans-serif]Nani kasema watoa taarifa wote wanawekwa chini ya mpango huo? Nilionyesha jinsi majambazi yanavyoweza kuwa tishio wa watoa taarifa, maana ulijaribu kutuambia kwamba majambazi huwa hawana pa kujificha kama wananchi wanawataja. Nikakuonyesha jinsi mwananchi ndio anaweza akawa hana pa kujificha bila mpango maalum wa kumlinda.[/FONT]

[FONT=Verdana, sans-serif]Na uhalifu mwingi unashughulikiwa na hao FBI pia. [/FONT][FONT=Verdana, sans-serif]Kama "hamna haja ya kuingiza FBI" kwa nini kuna FBI? [/FONT]

[FONT=Verdana, sans-serif]Si umesema polisi yabidi wawe karibu na jamii, na ndo msingi wa polisi jamii? Kama ndo hivyo basi polisi hawawezi, hawatakiwi, kuwa wageni! Wakiwa karibu hawawezi kujitoa kwenye majukumu yao kwa kujisema wao wageni. Kwamba polisi hawajui wahalifu kwa sababu wao ni wageni, wahalifu ni watoto wetu, polisi ni watoto wa nani? Polisi wa Vingunguti wanatoka wapi, huko kwa wenzenu?[/FONT]

[FONT=Verdana, sans-serif]Na hata kama kisingizio cha polisi kutofanya kazi ya kusakanya majambazi eti kwa vile hawawajui kwa ugeni wao, bado tunarudi kwenye ukweli kwamba wao ndo wanafanya uchunguzi, ndo kazi yao, mwananchi hafanyi uchunguzi. Hilo mbona hulijibu? [/FONT]

[FONT=Verdana, sans-serif]Mkuu, hiyo ndio kazi ya polisi![/FONT]

[FONT=Verdana, sans-serif]Na jambazi akijua kwamba anaemfuatilia ni raia asiye na nyenzo, mafunzo wala malipo, hataogopa, jambazi linaogopa askari kuliko mtu baki. Ndo maana wanafunga mtaa mchana kweupe wanateka, wanaua, wanaondoka. Tutumie jeshi la polishi.[/FONT]
Si umesema unataka polisi karibu? Vituo vidogo vya askari posti vilijengwa kusogeza polisi karibu. Sasa mwananchi akiwa na swala linalohitaji polisi aende kumngoja barabarani?

[FONT=Verdana, sans-serif]Mtume! [/FONT]

[FONT=Verdana, sans-serif]Yani polisi jamii kumbe ni haki umati ya mwiiiziii....chomaaa... uaa! Labda kweli wote, na Magufuli, na Said Mwema mwenyewe, hatuelewi polisi jamii ni nini. [/FONT][FONT=Verdana, sans-serif]Badala ya kutetea utawala wa sheria unatetea haki umati?[/FONT]

[FONT=Verdana, sans-serif]Upeo wangu wa kufikiri mdogo, ndio , lakini sijakubaliana na baadhi ya uloyasema hapo.
[/FONT]

.......Duuuhhh!!............aisee..........kazi ipo........."The great sinkers"..................kwi kwi kwi kwi kwi kwi..........haya bana!!
 
Kijana gani huyo kaka? Si vichwa vyote vya habari vya huko Marekani vinatufikia. Ungenifafanulia kijana huyo alifanya nini tuweze kuoanisha.

Umar Farouk Abdulmuttalab.

“[FONT=Verdana, sans-serif]Na sio serikali.” Umesema mwenyewe, "na sio serikali." Hizo juhudi za watu binafsi hazifanywi na wananchi kwa niaba ya serikali, mzigo wa kukamata wahalifu bado hajatupiwa mwananchi anaeangalia maonyesho ya kipindi hicho. Serikali ndio ina vyanzo na nyenzo za kupambana na ujambazi, polisi jamii ni dhana ya ukingu wa kukwepa wajibu.[/FONT]

Dhana ya polisi jamii haina maana kuwa suala la kukamata wahalifu wanaachiwa wananchi. Hata huko kwa wenzetu, kazi ya kukamata na kufanya uchunguzi bado ni ya polisi. Kinachofanyika ni kuwa jamii inashiriki katika kutoa taarifa n.k. Jamii isiyokuwa na imani na polisi ni mara chache wanakuwa tayari kutoa taarifa zinazoweza kusaidia uchunguzi wa matukio ya uhalifu. Unachanganya polisi jamii na sungusungu. Sungusungu ndiyo walitegemewa kufanya kazi ya polisi. Katika polisi jamii, mamlaka na wajibu wa kukamata wahalifu unabaki wa polisi.

Anhaa, sawa, asante kunijuvya. Kumbe huko “kwa wenzenu” uhalifu na ujambazi ni kama hapa kwetu? Walahi ibilisi kasambaa kila mandhari. Sasa mbona ulijaribu kutujengea hoja hapa kwamba polisi jamii huko “kwa wenzenu” imefaninikiwa? Naona kama unajifunga funga. Labda tueleze tena.

Mafanikio si kutokomeza uhalifu. Hata nchi zenye sheria kali bado zina uhalifu. Mafanikio ni kupunguza uhalifu kwa kiasi kikubwa. Na huko kwa wenzenu, katika maeneo mengi uhalifu wa kipuuzi umepungua sana. Lakini bado kuna sehemu ambako uhalifu bado uko juu. Mara nyingi katika maeneo haya polisi anachukuliwa kama adui na hamna kitu kibaya kama kuwa "snitch".

Huo si ukweli Mkuu, nimepata bahati ya kwenda warsha ndogo ndogo huko “kwa wenzenu” na sijaona polisi wakiwa katika “beat” eti wanasimama kuongea na wananchi. Kwanza wananchi wengi huko “kwa wenzenu” wanakuwa na miendo ya kasi kali na ari kali na nguvu kali, sijaona mtu anaacha zake, anasimama eti kuongea na polisi barabarani kumpa dodoso za majambazi! Ha ha haha haaaaa! Sijaona...! Askari wa huko “kwa wenzenu” wanapokuwa doria wanakuwa wamekunja ndita wakisoma lugha za mwili nyusoni mwa watu, hawafanyi uchunguzi wa ujambazi wanapokuwa doria, wanalinda doria!

Kwa wenzenu wapi ulikoenda? Dhana ya polisi kufanya patrol kwa kutembea iko uingereza. Si wananchi wote wana ari na kasi katika maisha yao. Kuna watoto wadogo, vikongwe, wenye biashara ndogo ndogo, watalii n.k. Wote hawa wanapokuwa na shida ndogo ndogo kimbilio lao ni polisi. Kwa mfano mtu ukipotea njia, mtu wa kukimbilia ni polisi. Doria haina maana uchunguzi wa matukio. Doria maana yake ni kuepusha matukio ya uhalifu na kutoa taarifa pale yanapotokea. Wanaofanya uchunguzi wa matukio ya uhalifu mara nyingi si askari wanaokuwa kwenye beats. Uchunguzi unafanywa na askari kanzu (CID).

Nani kasema watoa taarifa wote wanawekwa chini ya mpango huo? Nilionyesha jinsi majambazi yanavyoweza kuwa tishio wa watoa taarifa, maana ulijaribu kutuambia kwamba majambazi huwa hawana pa kujificha kama wananchi wanawataja. Nikakuonyesha jinsi mwananchi ndio anaweza akawa hana pa kujificha bila mpango maalum wa kumlinda.

Sasa unadhani wanawekwa kwenye hiyo Witness Protection Program kama hawakushirikiana na polisi kwa kuwa tayari kutoa ushahidi? Hii si ndiyo sehemu ya polisi jamii? Kwa mtazamo wako si wangenyamaza tu na kuwaachia polisi wenyewe wakatoe ushahidi? Sisi wakati tunakuwa uhalifu wa kipuuzi ulikuwa chini. Na sababu kubwa ilikuwa ukionekana unaiba embe basi utacharazwa bakora na ukishitaki kwa mzazi wako atakuongezea. Kulikuwa na zero tolerance na upuuzi kama huo. Leo ukijaribu kumsema tu mtoto wa jirani anapotaka kufanya ujinga,, utaipata. Uhalifu mwingi unaanzia na mambo ya kijinga. Uvumilivu wetu kwenye mambo haya ndiyo unaruhusu uhalifu unaohitaji mashahidi wapewe ulinzi wa serikali. Na huko kwa wenzenu sehemu kama hizo zipo.
Na uhalifu mwingi unashughulikiwa na hao FBI pia. [FONT=Verdana, sans-serif]Kama "hamna haja ya kuingiza FBI" kwa nini kuna FBI[/FONT]

Marekani kuna sheria za State na sheria za nchi nzima. FBI wanashughulikia uvunjaji wa sheria za nchi. Kwa mfano, ukikamatwa unauza bangi, utashitakiwa na kushughlikiwa na mamlaka za state. Lakini ukikamatwa unasafirisha bangi kutoka State moja kwenda Nyingine, utashughulikiwa na FBI pamoja na polisi wa state husika.

Si umesema polisi yabidi wawe karibu na jamii, na ndo msingi wa polisi jamii? Kama ndo hivyo basi polisi hawawezi, hawatakiwi, kuwa wageni! Wakiwa karibu hawawezi kujitoa kwenye majukumu yao kwa kujisema wao wageni. Kwamba polisi hawajui wahalifu kwa sababu wao ni wageni, wahalifu ni watoto wetu, polisi ni watoto wa nani? Polisi wa Vingunguti wanatoka wapi, huko kwa wenzenu?

[FONT=Verdana, sans-serif]Na hata kama kisingizio cha polisi kutofanya kazi ya kusakanya majambazi eti kwa vile hawawajui kwa ugeni wao, bado tunarudi kwenye ukweli kwamba wao ndo wanafanya uchunguzi, ndo kazi yao, mwananchi hafanyi uchunguzi. Hilo mbona hulijibu? [/FONT]

Ukaribu hakuna maana ya kuishi pamoja tu. Polisi kuwa karibu ni kujenga imani ya wananchi. Wakati vibaka, mateja n.k. mara nyingi wanatoka katika au karibu na maeneo ambayo wana ndugu au jamii, polisi si lazima. Kibaka, teja n.k. wa vingunguti mara nyingi ana watu wanaomfahamu katika maeneo hayo. Sasa kama mzazi wa polisi yuko Magu au Tarime wakati yeye mwenye anafanya kazi vingunguti itasaidia nini katika kuwakamata wahalifu wa vingunguti? Ndiyo maana polisi wanatakiwa kufanya juhudi za ziada ili kupata imani ya wananchi.

Si ndiyo maana nilikuambia huelewi unachozungumzia. wapi nimesema wananchi ndio wanaopaswa kufanya uchunguzi? Wananchi hawastahili kufanya uchunguzi maana ni taaluma pekee. Kuna namna ya kukusanya ushahidi bila kuathiri kesi. Mwananchi hawezi kujua haya. Uchunguzi ni kazi ya polisi. Wanachohitaji ni msaada wa wananchi kutoa ushahidi au taarifa zinazoweza kusaidia uchunguzi. Kwa mfano kama kuna tukio la mauaji limetokea sehemu, wananchi wanaweza kusema kuwa walimsikia fulani ambae sifa yake si nzuri akizungumza usiku eneo hilo. wananchi wanaweza kusema kuwa marehemu alikuwa jhaelewani na fulani, au marehemu alikuwa kibaka kwa hiyo bila shaka aliuawa akiwa kazini n.k. Atakaeunganisha taarifa zote hizi na kujenga kesi ni polisi na sio mwananchi.

Mkuu, hiyo ndio kazi ya polisi!

[FONT=Verdana, sans-serif]Na jambazi akijua kwamba anaemfuatilia ni raia asiye na nyenzo, mafunzo wala malipo, hataogopa, jambazi linaogopa askari kuliko mtu baki. Ndo maana wanafunga mtaa mchana kweupe wanateka, wanaua, wanaondoka. Tutumie jeshi la polishi.[/FONT]

Hamna kitu ambacho jambazi wanaogopa kama jamii kuwageuka. Bado unachanganya mambo. Polisi jamii haina maana kuwa mwananchi amnyemelee jambazi. La hasha. Polisi jamii itasaidia kuwa hata kabla ya tukio jambazi atajua kuwa hakubaliki na jamii itamtosa akifanya upuuzi wake.

Si umesema unataka polisi karibu? Vituo vidogo vya askari posti vilijengwa kusogeza polisi karibu. Sasa mwananchi akiwa na swala linalohitaji polisi aende kumngoja barabarani?

Polisi posti zinafanya polisi kuwa karani na kungojea aletewe taarifa na mwananchi. Polisi jamii ingawa inasisitiza ushirikiano wa jamii kama kutoa taarifa lakini zaidi inasisitiza kuwa polisi aonekane katika jamii. Kuonekana huku ni kuwa anazunguka katika maeneo wanayoishi wanachi. Vituo vya polisi vitakuwepo. Mwananchi si kazi au wajibu wake KUMFUATA polisi (kama tulivyozoea nyumbani) tukio likitokea bali ni yeye kutoa taarifa na polisi amfuate. Akitoa taarifa kwenye kituo cha polisi kwa simu basi wao ndio watamuagiza polisi aliyekaribu na tukio kwenda kutoa msaada. Kama mwananchi atakuwa na swala la kawaida linalomuhitaji polisi basi atamsubiri mtaani maana ni lazima atapita.

Mtume!

[FONT=Verdana, sans-serif]Yani polisi jamii kumbe ni haki umati ya mwiiiziii....chomaaa... uaa! Labda kweli wote, na Magufuli, na Said Mwema mwenyewe, hatuelewi polisi jamii ni nini. [/FONT][FONT=Verdana, sans-serif]Badala ya kutetea utawala wa sheria unatetea haki umati?[/FONT]

Mfano huu nimetumia kukujibu ulipodai kuwa wananchi wanogopa majambazi kwa sababu wanabeba SMG. Hakuna mahali nilipotetea uchukuaji wa sheria mikokoni
mwao.

Upeo wangu wa kufikiri mdogo, ndio , lakini sijakubaliana na baadhi ya uloyasema hapo.

Ni kweli upeo wako wa kufikiri ni mdogo. Hii haikuondolei haki yako ya kutokubaliana na chochote nitakachokisema.

Kama una nia ya kujua zaidi, soma hapa;http://rds.homeoffice.gov.uk/rds/pdfs08/rdsolr0108.pdf
Amandla.....
 
Salim 2015?

Salim huyo mzee ameanza uongozi alivyo balehe tu, alikuwa ubalozini mwaka 1961 akiwa na miaka 19, niko vidudu huyu mzee waziri mkuu, mpaka leo wa nini hawa kina babu hawa?

Magufuli nae anachemsha kama Mrema.
Ha ha ha ha ha kwani kati ya watz million 40 ni hao hao kamati kuu ya ccm wa kutuongoza? wako watu very proffessional na ethical bwana tatizo hawawezi fitina za kisiasa. We angalia Mpondela na Yanga alivyosema jamani hii iwe kampuni vibabu vilimuendea mpaka bagamoyo, sasa mbona imekua kampuni kimtindo kwa ujanja wa Manji kuwapa pilau (Siasa Tumbo hizo)
 
Back
Top Bottom