Paul Alex
JF-Expert Member
- Jul 14, 2012
- 4,240
- 9,527
Sio nia yangu kurudia yaliyotokea kwenye uchaguzi ulioisha, maana yamesemwa sana na yamesemwa na wengi.
Natamaani tutafakari kwa pamoja hili swali; kwanini viongozi wa nchi nyingi duniani wanakuwa na uhusiano wa karibu na watu tajiri?
Kwanini rais wetu anawachukia watu matajiri?
Au ni kwasababu tu ya ile dhana ambayo watu wengi masikini tunakuwa nayo kwamba, ili mtu awe tajiri lazima afanye mambo fulani ambayo sio halali? Tunadhani kuwa tajiri yeyote lazima au amedhulumu watu, au ametumia ushirikina au amefanya mbinumbinu tu ambazo sio halali na zilozopelekea kuumia kwa mtu au watu wengine.
Dhana kuwa tajiri akitaka ukaribu na kiongozi wa nchi basi huyo ni mpiga dili ni dhana ya kishamba sana.
Kati ya vitu ambavyo vinamuwezesha mtu kumiliki mali na kuikuza basi ni discipline.
Discipline ya matumizi, discipline ya kufuata sheria, discipline ya utendaji uliotukuka, discipline ya maisha ya familia,n.k
Sio lazima matajiri wote wawe kwenye kundi hilo hapo juu, ila kuwaweka wote kwenye kapu la wapiga dili sio sawa.
Marais wengi duniani ukiacha tu huyu wa kwetu, wanaona kuwa karibu na matajiri kama jukumu lao la msingi, na kimsingi ni sehemu ya uongozi.
Jamii yeyote ina makundi mbalimbali ya watu yenye mahitaji tofauti tofauti.
Kwanza kuwa karibu na kundi fulani haina maana ya kutokuwa karibu na kundi jingine.
Ni sehemu tu ya uongozi kuwa kiongozi wa wote na kuangalia mahitaji ya wote.
Ni mara ya tatu ndani ya mwaka mmoja 2017, rais wa urusi anakitana na watu matajiri urusi.
Kati ya mambo wanayojadili ni matatizo ambayo matajiri hawa wanapata kwa kuwekeza katika nchi nyingine na namna gani serikali yao inaweza kuwasaidia.
Wanajadiloana pia vipaumbele vya uwekezaji wa ndani, changamoto na jinsi ya kusonga mbele.
Mheshimiwa yeye anataka hawa wakwetu waishi kama mashetani.
These are people with connections, risking their money everyday to create jobs,pay taxes,bring in foreign currency. And the list you could do is stay close to them.
Kiukweli mimi naona uhusiano wa rais na 'watanzania masikini' unalenga zaidi kura ambazo ni maslahi binafsi ya rais. VS uhusiano wa rais na watu matajiri ungeongeza ajira, uwekezaji na kodi vitu ambavyo viko kwa maslahi mapana ya watanzania wote.
[HASHTAG]#Ugua[/HASHTAG] pole Tundu Antipas Lisu.