Magufuli ang'aka tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka

Gwalihenzi

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
5,125
1,300

• NAGU, MEDEYE WAO WAJITETEA

na Mwandishi wetu
WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, jana aling'aka akidai kuwa mwenye majibu kuhusiana na tuhumu zilizoelekezwa kwake na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, juzi za kutumia vibaya madaraka yake na kutisha wananchi ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Dk. Magufuli alitoa majibu hayo alipotakiwa na Tanzania Daima kutoa maelezo juu ya tuhuma hizo alizotupiwa pamoja na mawaziri wenzake watatu.

Wakati mawaziri wenzake wakitoa maelezo yao nje ya ukumbi wa Bunge kwa nyakati tofauti, Dk. Magufuli alikuja mbogo baada ya kuulizwa na kisha kujibu kwa mkato kuwa akaulizwe Waziri Mkuu.
"Sina la kukujibu, suala hilo kamuulize Waziri Mkuu kwani ndiye aliyeulizwa jana,'' alisema.

Juzi, Mbowe akiuliza swali la papo hapo kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aliwalipua mawaziri John Maghufuli, Dk. Mary Nagu, Stephen Wassira na Goodluck ole Medeye kwa madai kuwa wamekuwa wakitoa kauli za kibaguzi na vitisho kwa wananchi waliowachagua wagombea wa upinzani wakati wa kampeni.

Mbowe alimtaka Pinda atoe tamko rasmi ikiwa ndilo agizo na maamuzi ya serikali na kujua yalitolewa lini na katika kikao gani.

Hata hivyo, hoja hiyo ilimchefua Pinda ambaye kwanza alikana kuwepo kwa kauli hizo na kisha kueleza kusikitishwa kwake na hatua ya Mbowe kutoa matamshi hayo akiwa kama mmoja wa viongozi wakuu wa kisiasa nchini.
Kiongozi mkuu akijitetea, Waziri Nagu alishindwa kukubali au kukataa na kuelezea kuwa alichozungumza kilikuwa ni siasa.

"Arumeru tulikuwa kwenye mapambano, hivyo kila mmoja anatumia silaha yake na wala sikutumia gari la uwaziri," alisema Nagu ambaye ni mbunge wa Hanang. Nagu alisema alikwenda katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki kukisaidia chama chake na hasa ikizingatiwa kuwa jimbo hilo liko jirani na lake.

Pamoja na majibu hayo, alimshauri Mbowe kuachana na maneno yanayotolewa wakati wa kampeni, kwani yanakuwa mengi na kwamba yakifuatwa yanaweza kusababisha kutoweka kwa amani nchini. Hakufafanua.

Kwa upande wake, Medeye alidai hakumbuki kama aliwahi kutoa kauli hizo na kueleza kwamba kama Mbowe ana ushahidi aupeleke bungeni.

"Sikumbuki kutoa kauli kama hiyo, lakini kama Mbowe ana ushahidi wa mikanda ya video alete bungeni ili ukweli ujulikane,'' alisema.

Hata hivyo, alisema kuwa tangu alipoteuliwa kuwa Naibu Waziri amekuwa akifanya kazi bila upendeleo na hata kuyatembelea majimbo ambayo yanaongozwa na upinzani.

Juzi Mbowe alisema mawaziri hao na viongozi wengine wa CCM wamekuwa wakitoa kauli za kuwatisha wananchi kuwa wakichagua vyama vya upinzani maeneo yao hayatapatiwa fedha za maendeleo.

Alisema Nagu alitoa kauli hiyo Arumeru, Medeye aliitoa Arusha na Magufuli wakati wa kampeni Igunga.


My take; Mheshimiwa kamanda Mbowe amefanikiwa Kuuanika unafiki wa serikali ya CCM na Magufuli wao.
 
Inakuwaje mtuhumiwa ndiye anang'aka?!!! yale yale ya Mukama!
Huyu ndiyo watu wanampigia chapuo eti awe Rais. Magufuli, hana hizo character kabisa za kutumikia taifa kwenye cheo kikubwa kama cha Rais akijitahidi sana labda apewe uwaziri mkuu ili akiropoka hovyo, Rais arekebishe. Huwa anakurupuka tu yeye na kauli zake, hana muda wa kufikiria kwanza madhara ya anachokisema au kukisimamia.
 
Magufuri nafasi ya urais si saizi yake. Ni mtu wa kukariri sheria zinasemaje na kuwa na jazba kubwa katika maamuzi yake. Phd yake inamsaidia kuweka data kichwani mwake tu, lakini public relations hana kabisa ni ZERO.
 
Magufuli awe RAISI? Mnakumbuka zile kauli za: Chagua la Mungu,sijui huyu ni handsome boy, kijana mwenzetu etc etc. matokeo yake nyote ni mashahidi. Tukumbuke daima: Si kosa kufanya kosa, kosa kuridia kosa. Hawa jamaa (magamba), 2015 tuwaonyeshe ushindi wa ki-Tsunami unavyokuwa.
 
Hata huo uwaziri anaudhalilisha kwa unafiki na ukurupukaji - sembuse uRais!
 
Magufuri nafasi ya urais si saizi yake. Ni mtu wa kukariri sheria zinasemaje na kuwa na jazba kubwa katika maamuzi yake. Phd yake inamsaidia kuweka data kichwani mwake tu, lakini public relations hana kabisa ni ZERO.
Well said! Yu masti bi jiniasi.
 
Kuna kipindi niliweka thread kuhusu uongo wa magufuli wanajamvi wakaniandama kwa mitusi mizitomizito nikaishia kupata ban ya siku 90 lakini ukweli magufuli hafai hata ujumbe wa nyumba kumi hata phd yake hai relate na kazi yake anayofanya.
 
Magufuli ndiye mtu pekee anayeweza kubadilisha mwenendo wa uchumi Tanzania. Tatizo la Tanzania ni utanzania tunamhitaji mtu kama Magufuli.
 
Magufuli ndiye mtu pekee anayeweza kubadilisha mwenendo wa uchumi Tanzania. Tatizo la Tanzania ni utanzania tunamhitaji mtu kama Magufuli.
Sio kweli, watanzania hatumuhitaji mtu ambaye hawezi kusimamia kauri yake, mtu mroho anayeweza kuuza raslimali(nyumba za serilikali) kwa manufaa yake!
 
Akingia magufuli rasmi madarakani 2015 namisha ukoo wangu tunamia malawi, labda bi' banda atatufaa na ukoo wangu
 
Mkuu magufuli ni muongo mno pia anapenda sifa na vyombo vya habari

Magufuli ni mchapakazi asiyependa kupindisha mambo, sio muongo, sifa ni asili ya binadamu. Ndiyo maana ulipokuwa unafanya vizuri ktk mtihani shule ya msingi ulikuwa unapewa sifa kwa kuitwa mbele, unapewa mkono na mwl mkuu na unapigiwa makofi. Sioni kama sifa ni tatizo.
 
Sio kweli, watanzania hatumuhitaji mtu ambaye hawezi kusimamia kauri yake, mtu mroho anayeweza kuuza raslimali(nyumba za serilikali) kwa manufaa yake!

Kauli kama zipi? nyumba alisimamia sera ya serikali, iliyokuwa imepitishwa na baraza la mawaziri. Huo ndo uzuri wa mtu kama Magufuli anayefuata utawala wa sheria, unaisimamia sheria kama ilivyo wenda ni mbaya ama nzuri.

Viongozi binadamu wanaongozwa na sheria kutenda jambo, hawaongozwi na akili zao nzuri kutenda. Binadamu yeyote anayetenda kwa mjibu wa sheria ndiye kiongozi anayefaa, haijalishi sheria ni nzuri ama mbaya maadamu sheria imepitishwa na vyombo mlivyovichagua ninyi kutenda kazi hiyo.
 
Back
Top Bottom