Magufuli alikoroga, Maandamano makubwa kumpinga leo

Asante Mkuu!
Kwa ufupi wakazi wa jiji ni moja kati ya wananchi walio hovyo na kimsingi wao ndio wanaochelewesha maendeleo ya nchi yetu. Wao ndio wakwanza kulia linapotokea tatizo. Angalia tv, sikiliza redio, wanaharakati. Ni walalamikaji wazuri. Halafu ni wote, hadi wabunge wao! Inapofika uchaguzi, wao ndio wanaipendezesha na kuichagua ccm. Acha watukanwe labda watapata akili. Wabunge wao walisha ambiwa wanatumia makalio kufikiri. Labda matusi na kudhalilishwa ndio kutawafungua macho. Hovyo kabisa!


Aaahh kamanda hukumbuki kwamba tupo wapiganaji hata kama ni wachache!?

Ukisema ni wote hata wale wa kawe na ubungo waliosimama imara hadi kikaeleweka. Nadhani ni sahihi kusema wengi wao na si wote.
 
Wabunge wa Dar mnatafuta umaarufu! Sina tatizo na ongezeko la nauli kutoka 100 kufikia 200. Tatizo langu ni kauli aliyoitoa Magufuli " Atakayeshindwa kulipa 200, avuke kwa kupiga mbizi". Hii ni kauli ya dharau kwa walipakodi(wananchi) ambao wanamfanya atembelee shangingi na kumlipa posho, marupurupu na mshahara wa kila mwezi. Kama Magufuli ulimi limteleza awaombe radhi wananchi, ila kama alitamka maneno hayo kwa kudhamilia basi apotezee.
 
Mnang'ang'ania nini uko kigamboni? kwanza kumeshauzwa na mnatakiwa kuhama, akufukuzae hakwambii toka kaka, chura upenda maji lakini c ya moto! jifunzeni kuogelea, mia mbili mnaandamana? hacheni upuuzi, mbona watu toka mbezi ya kimara mpaka town wanalipa nauli ya 1000 na watu wamekaa kimya? kivuko cha misungwi watu wanalipa nauli ya 300, kamanga sh 800 mpaka 1000, kupandishiwa mia tu mnapiga makeleleeee! kama vp amieni masaki au upanga. mkiandamana tu virungu na mtakomaje!

Kaka samahani, shkamoo! Huyu simba aliyepakatwa kwenye avatar yako kapakatwa na Yanga?

Poleni wakazi wa kigamboni kwa kukumbana na ongezeko la gharama za kitu kwa mara ya kwanza kwenye maisha yenu. Najua litaathiri ushiriki wenu katika kucheza bao ng'ambo ya huku, loh!

Lkn tukiacha utani, serikali haikuwa na sababu ya kupandisha gharama za vivuko. Mapato ya hiyo hiyo mia inayoonekana haitoshi yanaishia kwenye mifuko ya watumishi. Walipoweka zile mashine za kupanchi walizihujumu mpk zimekufa ili waendelee kukatsha tiketi kwa mikono waweze kuiba. Nyie wachunguzeni utagundua kama hujamwangalia vizuri tiketi hawachani, wanarudisha dirishani kuuza tena. Sasa badala ya kidhibiti mapato, inaongezwa nauli, boh!

Kwanza wenzetu kule Likoni (kivuko cha Mombasa) wavuka bureeee! Watoka zako Shika Adabu Primary School wajijaza chomboni tu mwapelekwa, bila hata bob moja. Sasa hapa ni nini?
 
Watanzania wengi ni wavivu wa kufanya miradi midogomidogo. Mnaishi kwa kutegemea mishahara tu ndiyo maana ikitokea tatizo dogo la kuongeza hata shs 50 mnaanza kulialia kama vinyau. Acheni kutegemea vimishahara na anzeni kufanya biashara nyingine nyie.
 
Tatizo mama ni uzembe wa serikali kutojenga daraja kigamboni(nakisia halizidi 600 metre) kwa zaidi ya miaka hamsini. Inasikitisha umahiri wetu umeishia katika kuandaa sherehe kubwa kubwa za hasara zinazo andamana na ubunifu wa kupamba kijani na njano.
 
Mkuu nadhani hujasoma vizuri malalamiko ya watu wa kigamboni, na kama umeyasoma hujayaelewa.
Pamoja na kulipa 200 ya kivuko bado wanalipa nauli za mabasi kwenda sehemu mbalimbali, na hata huyo wa kimara kama anafanya kazi kigamboni atalipia kivuko.

Ukilinganisha nauli ya kamanga ferry na kigamboni usisahau kutaja na urefu(umbali) wa kusafiri vivuko hivyo viwili.

Usisahau kuna issue ya ubadhirifu wa fedha za vivuko, kama hali ingedhibitiwa hizo gharama za uendeshaji unaotajwa ungekuwa ndani ya uwezo wao.

Lakini angalia na hili, nauli ya guta na bajaji kupanda toka sh.300 hadi sh.1,800 wakati gari ndogo nauli imepanda toka sh.1,000 hadi sh.1,500 hapo kuna uwiano sawa?

Hapo kwenye red naomba kuuliza: hivi na zile bajaji za wajawazito zilizotolewa JK ambazo mama analazwa humo kama yuko kwenye kijeneza nazo zimepanda au ziko exempted?

Pamoja na udhaifu wa magamba, I can see kwa nini PM alimpiga ban kwa mikauli yake ya kutishia wananchi nchi nzima kubomoa nyumba zao ambazo ziko pembezoni mwa barabara.
 
Mkuu, msome Zungu vizuri hapa:



Tusisahanu pia wapo wananchi wanaoishi kigamboni na kufanya kazi huku 'bara' au wanaishi huku 'bara' na kufanya kazi kigamboni na wengi tu wana magari, baiskeli na pikipiki ambazo zote zimepandishiwa nauli. Kwa hiyo pressure haitokani na hiyo 200 peke yake!

Hata hivyo sikatai kwamba hawa wote mwisho wa siku na 'wafanyasiasa' tu!
Tatizo sio nauli ya kivuko.........Tatizo ni 2015.......

Hakika tutayaona na kuyasikia mengi.....Na hili la wabunge wa CCM Dar kumvaa Magufuli ni sehemu ya hayo mengi....
 
Mnang'ang'ania nini uko kigamboni? kwanza kumeshauzwa na mnatakiwa kuhama, akufukuzae hakwambii toka kaka, chura upenda maji lakini c ya moto! jifunzeni kuogelea, mia mbili mnaandamana? hacheni upuuzi, mbona watu toka mbezi ya kimara mpaka town wanalipa nauli ya 1000 na watu wamekaa kimya? kivuko cha misungwi watu wanalipa nauli ya 300, kamanga sh 800 mpaka 1000, kupandishiwa mia tu mnapiga makeleleeee! kama vp amieni masaki au upanga. mkiandamana tu virungu na mtakomaje!

Chonka iwe okabakisi? mhhhh wakiboine!!!! Dar mia ni ngumu kinoma.
 
Wana Dar es salaam is about time mjifunze kupiga mbizi, haiwezekani mnaishi kwenye jiji lenye bahari alafu hamjui kupiga mbizi.Magufuri kaliona hilo ndio anajaribu kuwakumbusha.Magufuri uko Juu sana wana Dar(Kigamboni)wajifunze kupiga mbizi.Na wabunge wa Dar waache ku-politicizing ktk kila jambo kwa kigezo cha kudai wana watetea ordinary wananchi kwani huo ni unafaki, mbona nauli za other means of transport zinapanda kila kukicha na hatuwasikii wakiongea, ama kwasababu magufuri kasema?
 
watanzania hawapendi kuambiwa ukweli, na hii mibunge ya dar ni mikenge tu, hio nauli ya 100 ni ya miaka 14 iliyopita, je gharama za maisha zimepanda kwa kiasi gani? Km wanakigamboni wameshindwa kulipa 200 wahamie ubena zomozi au km alivyosema Magufuli wapige mbizi kuja kivukoni, mbona huko bara vivuko bei inaanzia 300 wao hawasemi?. We mtemvu na wenzako mbona posho ilivyoongezwa hamkusema na watumishi waongezwe mishahara pia kwani maisha magumu?, achei ubinafsi huo, kwenye ukweli lazima mikiri sio kuleta siasa.Magufuli endelea hivyo hivyo achana na hao *******.
 
mimi hapo naona waheshimiwa wabunge wetu wa dar wanatafuta pa kutokea au cheap popularity,naomba ni wachallenge je kwanini wasitoe pendekezo la kutoa sehemu ya posho zao za ubunge kama ruzuku ya kufidia ongezeko hilo la nauli ya kivuko kama kweli wana huruma na wanachi wa dar es salaam lengo likiwa ni kuwapunguzia mzigo wananchi at the same time kuchangia gharama za uendeshaji wa kivuko?

hebu just imagine nauli ya sh.100 pale kivukoni imedumu kwa miaka mingapi bila kupanda huku serikali ikijifunga mkanda kuboresha huduma pale ikiwamo kununua kivuko kipya kile kikubwa,leo kuomba wananchi wachangie sh 200 wala sio 500 wabunge wanakuja juu wakati wao wanapokea mamilioni ya posho!!!! magufuli ningekua mimi ningekomaa tu acha waandamane na hao wabunge wenye matumbo makubwa mpaka yanataka kupasuka na hawaridhiki kutwaa kudai posho wanazitumia wapi?

Hawa Wabunge mbona walikuwa kimya wakati wananchi wanaangamia kwa mafuriko hapa Dar?

Nadhani Maghufuli alikuwa akiwatania tu manake yeye Msukuma na Dar ni ya Wazaramo. Wasukuma na Wazaramo ni watani na Maghufuli anapenda utani wakati mwingine manake huwa anamtania hata JK!
 
Mkuu, msome Zungu vizuri hapa:



Tusisahanu pia wapo wananchi wanaoishi kigamboni na kufanya kazi huku 'bara' au wanaishi huku 'bara' na kufanya kazi kigamboni na wengi tu wana magari, baiskeli na pikipiki ambazo zote zimepandishiwa nauli. Kwa hiyo pressure haitokani na hiyo 200 peke yake!

Hata hivyo sikatai kwamba hawa wote mwisho wa siku na 'wafanyasiasa' tu!

Huyu Zungu yeye anataka kula Ubuyu Bonde la Jangwani!!
 
au hawa wanaoandamana ndio hawawezi kupiga mbizi?

inawezekana ikawa hvyo!!
Gharama ya 200 bdo ni ndogo sana,kama wananchi wanalalamika kwa +200 basi hli ni mbaya mno.Kwa ongezeko hlo halina utata ni lazima waungwana walipe bla ya utata.
Lakini mzee magufuli hanapaswa kuomba radhi wananchi kwa matapishi aliyotoa kwa wananchi.
 
wakazi wa kigamboni wengi wanatoka enzi far as kimbiji,kibada and vijibweni,..kutoka huko nauli ni kama 400/=*2+200*2 na wengi wao ni wauza samaki ferry,..faida kwa siku ni 2000
 
Mkuu
Serekali nzima imekosa mikaati na Ubunifu wa kuendesha mambo mengi, nina hakika upo uwezekano wa hicho kivuko kutoa huduma bure. Kuna sekta nyingi zinazopoteza Pesa wachilia mbali zinazoibiwa katika Wimbi la Ufisadi na Rushwa.

Serekali ya Jiji itakuwa na vitega uchumi chungu tele na vitakuwa havina uongozi na usimamizi mzuri hivyo Pesa nyingi Hupotea ambazo zingeweza kuendesha huduma hiyo muhimu bila kuwalipisha Wananchi ambao tayari wanakabiliwa na Malipo kila Kona.

Kinachoudhi zaidi ni Viongozi Kukosa Lugha ya kistaarabu kwa Waajiri wao (Wananchi) Na hii hutokea hasa kiongozi akishapewa sifa mbili tatu basi Anapanda kichwa na kusahau alikwenda mikono nyuma akitoa Shkamoo mpaka kwa walio wadogo kwake wakati akiomba kura.

Magufuli anaingia katika kundi hilo, wapo wengi, Jihadarini tutawaumbua Uchaguzi unapiga hodi....................!

Kwa kuongezea, inasadikika mapato mengi sana (50M) yanapotea pale kutokana na wafanyakazi wasio waaminifu, walichoshauri ufanyike uchunguzi na kubaini hayo mapungufu waone kama kuna uwezekano wa kupandisha hiyo nauli.

Kingine nadhani watu wasing'ang'anie sana kuhusu nauli ya mtu, kuna nauli za Gutter na magari zimepanda maradufu na ndio zinazopeleka na kuleta bidhaa kutoka na kwenda Kigamboni ambazo nazo zitapanda bei na kupafanya kigamboni kuwa mahari ghali sana kuishi. Nadhani wabunge wana hoja mbali na kauli za bwana misifa!!!!
 
Magufuli sasa nakuunga mkono,
Komaa hivyo hivyo, kwanza ikiwezekana nauli iwe Tsh 500 kama vivuko vingine huko mikoani
Watu wa Dar wanapenda sana bwerere, na hawa wabunge wao wengine wanatafuta tu misifa ya kijinga
Kama vipi nyie waDaslaam wanyimeni kura CCM tuone, maana pekee yenu hamtakagi mabadiliko
 
Siasa za kipuuzi kabisa.. unaweza kuona ni jinsi gani ilivyo ngumu kuikomboa nchi yetu na siasa za maji taka, huu mi nauita uwendawazimu wa wabunge wa DSM, Hivi Mnyika na Mdee nao wameshiriki katika huu upuuzi wa kumvua nguo magufuli? ni utaahira wa hali ya juu sana kufanya maandamano eti kwa sababu mmepewa ukweli ambao ni mchungu...Tanzania ya leo inahitaji watu kama magufuli amabao hawacheki na kima kwani ukicheka na kima lazima uvune mabua.. Tunahitaji mtu anayeweza kufanya maamuzi magumu by all means hata kama ni kutukana au lugha zinazoudhi lengo ni kufika tunakotaka kwenda.

Sasa kuna watu wanaleta uswahili wa kijinga kwenye mambo ambayo yanataka umakini.. chukulia mfano kauli ya Mtemvu eti tumezaliwa hapa mjini na sio kule Kato" this is stupid! ndio yale yale ya zungu kupinga watu kutoka mabondeni mapaka mauti zimewakuta huko huko mabondeni.. hao wabunge kwa nini hawakukutana kupinga tamko la Anne makinda kuhusu posho? au hizo posho haziadhiri mtanzania wa kawaida?

Mbunge wangu Mnyika naomba msimamo wako katika hili kwani nawe nimeona ulikuwepo kwenuye hicho kikao
 
Nayakaribisha sana maandamano haya. Huenda ukawa ndio mwanzo wa maandamano mengine makubwa zaidi juu ya mambo mbalimbali yanayolisibu TAIFA hili. Mfano:
-Nchi kuongozwa na mafisadi, wezi, walafi na waroho wa madaraka.
-Tukadai zaidi ya bilioni 60 zilizotumika kwenye sherehe za UHURU wa TANGANYIKA ambayo haipo.
-Huduma mbovu za jamii kama ELIMU na AFYA.
-Mchakato mbovu wa kuiandika upya KATIBA yetu
-Uendeshaji ghali sana wa SERIKALI na BUNGE letu.
-Upandaji holela wa BIDHAA na HUDUMA.
-nk., nk.
 
Dr Magufuli nyumba za serekali uliuza lakini bado ukapeta kutokana na mfumo wet mbovu suala la kivuko sijui kama utatoka na suala la uRais mwaka 2015 ndiyo kabisa usitegemee kama utapona.
 
Back
Top Bottom