Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 55,784
- 90,545
Magufuli alikoroga
> Maandamano makubwa kumpinga leo
na Abdallah Khamis na Chalila Kibuda
WABUNGE wa mkoa wa Dar es Salaam, wameuomba uongozi wa juu wa nchi kumuonya na kumkemea Waziri wa Ujenzi Dk. John Pombe Magufuli kutokana na kauli yake na maamuzi mabaya ya kupandisha nauli ya kivuko cha Kigamboni ambayo itawaumiza wananchi.
Aidha wabunge hao wamemtaka waziri huyo kuwaomba radhi hadharani wakazi wa jijini la Dar es Salaam, hususan waishio Kigamboni kutokana na matamshi yake ambayo yamewachukiza wengi.
Akitoa taarifa ya kikao cha wabunge hao, Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtenvu, alisema serikali imekuwa ya kwanza kuwakemea wamiliki wa vyombo binafsi vya usafirishaji wanapopandisha nauli kiholela, lakini imekaa kimya bila kumkemea waziri wake anayefanya maamuzi ya kuwaumiza wananchi.
Wabunge hao wa mkoa wa Dar es Salaam waliiomba pia serikali iwaachie muda wa wiki mbili wasimamie mapato katika kivuko hicho, ili kumthibitishia Magufuli kuwa kuna ufisadi wa kutisha na usimamizi mbaya unaofanywa na watendaji wake.
Walieleza kusononeshwa kwa kiwango kikubwa na lugha ya ubabe aliyoitoa Magufuli juzi alipozungumza na wakazi wa Kigamboni juu ya ongezeko la nauli ya kivuko.
Mtemvu alisema lugha ya waziri huyo aliyoitoa akiwataka wakazi wa Kigamboni wasiokubaliana na nauli mpya iliyotangazwa na serikali wazungukie Kongowe au wajifunze kupiga mbizi haikutakiwa kutolewa na kiongozi mwenye hadhi na heshima kama Magufuli.
"Mnajua ni wazi kabisa hata sisi wa mjini tuna maneno mengi na tunaweza kuongea lugha za kuudhi zaidi ya kauli za Magufuli isipokuwa tumefunzwa kuwa na adabu kwa kila mmoja," alisema Mtemvu ambaye ni Mbunge wa Temeke (CCM).
Mtemvu alisema maamuzi ya Dk. Magufuli katika sula la Kigamboni yamekuwa ya jazba na hakutaka kuwashirikisha wananchi kama serikali inavyojinadi siku zote.
"Dhamira ya serikali ya CCM ni kuona wananchi wanapata unafuu katika maisha, sasa hili la waziri kukurupuka na bila kutolea ufafanuzi na kujibu barua mbali mbali zilizofikishwa kwake, haileti sura nzuri kwa wananchi na mbaya zaidi anatumia lugha ya kuudhi kwa mbunge mwenzie," alisema mbunge mmoja akiungwa mkono na wenzake.
Dk. Faustine Ndugulile, Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, alisema Magufuli anawadanganya wananchi kwa kusema hajafikishiwa taarifa za maboresho ya kivuko, na kueleza namna alivyomuandikia barua ya kwanza Januari 19, 2011, juu ya changamoto mbalimbali za kufanyiwa kazi ili kuomgeza ubora wa huduma na mapato kwa serikali badala ya kuzidisha nauli.
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni kuongeza kivuko kingine kwa ajili ya kukabiliana na wingi wa watu wanaotumia kivuko hicho, pamoja na kuongeza njia ya kutokea na kuingilia kwa ajili ya kurahisisha vivuko kufanya kazi kwa haraka.
Ushauri mwingine ni wa kuondoa kituo cha teksi na kudhibiti uuzwaji wa tiketi pamoja na kuondoa baadhi ya vibarua ambao hawana umuhimu katika kituo hicho.
Alisema licha ya kumuandikia barua hiyo ya Januari mwaka jana, alimwandikia nyingine mwezi Desemba mwaka huo huo, lakini Waziri Magufuli hakuonyesha kujali wala kutoa majibu ya mapendekezo hayo hadi walipoamua kupandisha nauli hizo.
John Mnyika Mbunge wa Ubungo na Katibu wa Wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam, alisema kwa kuwa kazi ya Bunge kwa mujibu wa ibara ya 63 ni kuishauri, kuisimamia serikali pamoja na kutunga sheria, watamtaka Dk. Magufuli awaeleze alichukua hatua gani baada ya kushauriwa juu ya maboresho ya kivuko hicho kabla ya kupandisha nauli hiyo.
Alisema Magufuli ameyatumia kibabe mamlaka yake kwa kuamua jambo ambalo linapingana na sehemu nyingine ya sheria, kwa kuwa sheria mama ya nchi ambayo ni Katiba inatoa fursa ya watu kujadiliana katika mambo ya msingi.
"Tatizo la Waziri Magufuli ni kusoma sheria moja na kwa kuwa sheria zetu zingine ni mbovu yeye anatumia udhaifu huo kufanya maamuzi ya kibabe ikiwa ni pamoja na kutoa lugha ya kuudhi kwa wabunge na wananchi.
"Tunataka ajue hana tofauti na sisi kwa kuwa wote tumechaguliwa na yeye amepata dhamana ya kuwa waziri tu, pia ajue magari na ofisi anayotumia ni mali ya hao wananchi anaowataka wapige mbizi kwa ajili ya kuvuka," alisema Mnyika.
Mbunge wa Ilala Musa Azzan "Zungu" alisema lengo la serikali ni kusaidia wajasiriamali wadogo hivyo kuwapandishia gharama hizo kutaathiri mfumo mzima wa maisha yao kwa kile alichoeleza kila inapoongezeka gharama ya aina yoyote katika maisha ya kawaida anayeathiriwa ni mtumiaji wa mwisho ambaye ni mlalahoi.
Alisema katika mtazamo wa kawaida watu watafikiri kuwa kinachopingwa ni ongezeko la sh 200 toka 100, pasipo kuangalia athari la tukio zima kwa kuwa hata mwendesha guta itambidi aongeze nauli ya kusafirishia mizigo ya wafanyabiashara ambao nao wataongeza bei itakakayomgusa moja kwa moja mtumiaji wa bidhaa hizo.
Zarina Madabida Mbunge wa Viti Maalum, mkoa wa Dar es Salaam alisema si watu wote watakaokuwa na uwezo wa kulipa ongezeko hilo jipya na kubainisha watakaoathirika kwa kiasi kikubwa watakuwa wanawake kwa kile alichoeleza ndiyo wahangaikaji wa shughuli ndogo ndogo za biashara.
Anjela Kairuki anayewakilisha viti maalum mkoa wa Dar es Salaam, alisema Wizara ya Ujenzi inatengeneza hali ya ubaguzi kwa kukiuka Katiba ya Tanzania inayomtambua mtoto mdogo kuwa ni yule aliye chini ya miaka 18.
"Tangazo lao linasema watoto chini ya miaka 14 watavuka bure na wale wenye sare za shule watalipa sh 50 kwani wakiwa katika nguo za nyumbani ndiyo utoto unawatoka," alihoji Kairuki.
Mbunge wa Viti Maalum Temeke Mariam Kisangi, alisema katika suala hilo la kivuko Magufuli anajitengenezea chuki kwa wananchi wa kawaida na kujiongezea marafiki kwa upande wa mafisadi walio katika wizara yake wanaosimamia biashara ya Kivuko.
Maandamano ya kumpinga leo
Wakati hayo yakijiri, taarifa zimebainisha kuwa maandamano makubwa ya kumpinga Waziri Magufuli yatafanyika leo na kuwashirikisha wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu kikiwemo Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya chuo hicho zimesema kuwa tayari jeshi la polisi limearifiwa juu ya kuwepo kwa maandamano hayo na tayari wanafunzi wa vyuo, sekondari na wale wa shule za msingi ambao bado wako majumbani, wamekwishatangaziwa kushiriki maandamano hayo.
Hata hivyo, juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, kuthibitisha kama wameruhusu maandamano hayo, hazikufanikiwa baada ya simu yake ya kiganjani kuita muda mrefu bila kupokelewa.