Mabadiliko makubwa yanaletwa na MAgufuli sio hili genge la nzige na mafisadi waliojikusanya na kuanza kutuhadaa kwa maneno matamu yasiyo na vitendo hata vya kufikirika,watanzania tumeamka natunafahamu kuwa ni nani anatufaa katika kuongoza taifa letu.
Kaka Kiiza, tarehe 25 October, Magogoni ni Lowassa!, ila....!.
P.
Hapa ndipo ninapokumbuka maoni ya Mkandara kwenye moja ya post huku JF
Vyama hivi sasa ni vigumu kuona tofauti yao...hatuoni tofauti ya itikadi wala Sera...hujui chama kipi kinaamini kipi na kinasimamia lipi
Tabu zaidi ni kuwa CCM kama chama mama tulitarajia kiwe way ahead of vyama vya upinzani...kuanzia kwene ubunifu mpaka kwenye itikadi na kauli mbiu za kukitofautisha na hivi vyama pinzani na vichanga
Kwa sasa CCM ni kama think-tankers wao wameshafikia ukomo wa ubunifu na wana kazi ya ku-copy na ku-paste toka upinzani
Nilianza kuona waki-copy na ku-paste Lowassa Mabadiliko Mabadiliko-Lowassa wakigeuza kuwa Mabadiliko-Magufuli Magufuli-Mabadiliko
Sasa na hii ya M4C nayo wameiga....
Naanza sasa kuwaza kimyakimya kuwa..."If I am to choose between a copy and the original, I will choose the original one as it has the root and the how's of the vision and it will never fade in a little while"
Mimi napata shida kidogo nikiona hii slogan ya M4C - Movement for Change ambayo inaonekana kuuzika sana kiasi cha wapinzani wa Chadema kuanza kutaka kuitumia kwa kupachika viji-maneno vyao. Hivi hii kitu inakuwa vipii NEC wanafumbia macho. Chama flani kinauza slogan inakubalika then mengine yaje tu kuitumia kwa ajili ya kuchanganya watu. Ingawa najua hata kama tukiwaachia tunazo nyingi na ni rahisi kuuzika, mfano mzuri ni Mabadiliko - Lowasssa.
M4C Magufuli for change,iko njema
Nimesikia huu ni mkakati uliopangwa wa kuchanganya watu akili kama wasipokuwa makini wampigie kura Magufuli wakidhani wanawapigia Chadema. Kaa chonjo!!